Tafuta

Vatican News
Malkia Elizabeth II wa Uingereza akihutubia Umoja wa Mataifa Jumapili tarehe 5 Aprili 2020 katika  janga hili la virusi vya corona Malkia Elizabeth II wa Uingereza akihutubia Umoja wa Mataifa Jumapili tarehe 5 Aprili 2020 katika janga hili la virusi vya corona 

Coronavirus#Matumaini yaanza kuonekana kidogo nchi za Ulaya zilizoathirika sana na virusi!

Yameanza kuonekana matumaini kidogo Ulaya katika mapambano dhidi ya virusi vya corona -covid-19 na wakai huo huo Katibu Mkuu wa Umoaja wa Mataifa Bwana Guterres amezitaka serikali duniani ziwalinde wanawake zaidi katika janga la corona.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Taarifa kuhusu Mataifa ya Ulaya yaliyoathirika zaidi na virusi vya corona ni kwamaba yameanza kuona dalili ndogo za matumaini katika mapambano dhidi ya virusi vya covid-19 lakini kwa upande wa Marekani bado inaendelea kujiandaa kukabiliana na hali mbaya zaidi. Haya yanakuja wakati ambapo idadi ya vifo nchini Marekani inaelekea kufikia watu elfu kumi. Virusi vya corona vimeuathiri karibu ulimwengu mzima na kuwapelekea karibu nusu ya watu duniani kubaki majumbani na kupelekea vifo vya karibu watu sabini elfu.

Katika tukio hili  la corona naye Malkia Elizabeth II wa Uingereza, hakukosa kusikika sauti yake kwa umma ambapo tarehe 5 Aprili 2020 ametoa  hotuba yake ya nne ya dharura katika uongozi wake wa miaka 68 ambapo amewataka Waingereza na nchi za Jumuiya ya Madola kubaki kuwa kitu kimoja. Hata hivyo Juampili 5 Aprili ilikuwa na sababu ya kutoa pumzi ya matumaini katika baadhi ya sehemu Ulaya kwa mfano chini Italia ambauo iliripoti visa vichache zaidi vya vifo katika kipindi cha wiki mbili na Uhispania ikashuhudia visa vyake vya waliofariki kushuka kwa siku ya tatu mfululizo na nchiniw Ufaransa ikiwa na idadi ndogo ya atu waliokufa katika kipindi cha wiki moja.

Licha ya hayo yote, Karantini katika mataifa inaendelea kuzua matatizo mengine japokuwa yalikuwapo kuhusu manyanyaso ndani ya maisha ya wanawake na wasichana majumbani kwako, kwa wakati huu yamezidi. Kufuatana na hiyo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  BwanaAntonio Guterres amezitaka serikali kuwajumuisha wanawake katika juhudi zao za kupambana na janga la virusi vya corona. Visa vya dhuluma dhidi ya wanawake vimeongezeka duniani sana wakati serikali tofauti zimeweka marufuku ya kutotoka nje kwa ajili ya kuudhibiti kuenea kwa virusi hivyo. Akizungumza katika ujumbe alioutoa kwa njia ya video, Guterres amezitaka serikali kuwaweka wanawake katika mipango yao ya kukabiliana na virusi hivyo.

Kwa mujibu wa Tume ya kitaifa ya wanawake nchini India katika wiki ya kwanza ya marufuku kutotoka nje, nchi hiyo iliripoti mara mbili visa vya unyanyasaji wa wanawake ambavyo kawaida vinandikishwa. Na kuhusiana na uongozi nchini Ufaransa umesema visa nchini humo viliongezeka kwa thuluthi moja huku Australia ikiripoti asilimia sabini na tano ya watu waliokuwa wanatafuta njia za kuwasaidia wahanga wa dhuluma za kinyumbani kwenye mtandao wa intaneti. Katibu Mkuu anasema kuwa tatizo hilo ni katika nchi maskini na tajiri; takribani robo ya wanafunzi wa kike kwenye Vyuo Vikuu nchini Marekani wamekumbwa na ukatili wa kingono au unyanyasaji wa kingono ilhali katika nchi za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahara, ghasia kutoka kwa mpenzi ni jambo la kawaida kwa asilimia 65 ya wanawake.

Katibu Mkuu Bwana Guterres anakumbusha kwamba kuchukua hatua dhidi ya ongezeko la ghasia, inakuwa vigumu zaidi kutokana na suala kwamba taasisi zilizopo tayari zimezidiwa uwezo kutokana na kushughulikia Corona. “Watoa huduma za afya na polisi wamezidiwa uwezo na wako wachache. Vikundi vya usaidizi vya mitaani navyo vimedhoofika au havina fedha. Baadhi ya vituo ambavyo ni makazi kimbilio la manusura wa ukatili navyo vimefungwa na vingine vimejaa

Tafiti za shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO, zinaweka bayana madhara ya ukatili kwa afya ya mwili, akili na uzazi kwa mwanamke. WHO inasema kuwa wanawake ambao wamekabiliwa na vipigo au ukatili wa kingono wana nafasi mara mbili zaidi mimba kutoka na pia wana nafasi mara mbili zaidi kukumbwa na msongo wa mawazo. Katika baadhi ya maeneo, wanawake hao wana uwezo wa mara moja nusu kupata virusi vya ukimwi, VVU, na Ushahidi unaonesha kuwa wanawake waliokumbwa na ukatili wa kingono wana nafasi mara 2.3 kutumbukia katika unywaji wa pombe kupindukia.

06 April 2020, 14:26