Iran#coronavirus:Barua kwa Papa kutoka kwa mkuu wa chuo kikuu Qom!
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican
Shukrani kubwa kwa Papa Francisko ambaye amejionesha kujali maskini na watu wenye kuhitaji katika kipindi hiki cha janga la virusi vya corona, mapendekezo ya kina na ushirikiano, ubadilishano wa uzoefu katika taasisi katoliki kwa namna ya kuunda jumuia ya dini za mbingu katika kutoa huduma kwa ubinadamu. Ndiyo ujumbe uliomo katika barua ya Ayatollah wa Iran, Alireza Arafi, Mkuu wa Chuo kikuu cha Kimataifa cha Qom, aliyo mtumia Papa kwa niaba ra wanachuo ambao ni Jumuiya ya wanafunzi wa Shiiti nchini Iran, Yeye ni kiongozi na porfesa maarufu.
Ubaya wa virusi vya corona na mateso
Ubaya wa kuenea kwa corona umesababisha mateso kwa nchi na mataifa yote, pia unasikitisha wasomi na viongozi wa dini. Waalimu wa dini na wanafunzi wao, wa Qom na nchini Iran, anaandika Ayatollah kuwa, wanaomba huruma ya Mungu kwa wote ambao wamepoteza maisha na uponyaji kwa wale ambao ni wagonjwa na wanatoa shukrani zao kwa Papa Francisko na kwa wale wote wanaojali wanyonge na wahitaji huku akisisitiza umuhimu wa kufuata mipango iliyoainishwa na mapendekezo ya wataalam na wanasayansi.
Mateso yanaleta utambuzi
Kwa mujibu wa mantiki ya dini zilizofunuliwa, ujumbe unaendelea kupitia Shirika la Habari za Kimisionari Fides kuwa, majanga ya asili ni matukio ya mshtuko ambayo yanajaribu ubinadamu na pia yanawakilisha hali ambayo hukuza mtu na kumpa uwezekano wa kufufuliwa ambamo inawezekana roho kuzaa matunda ya huruma na kujitoa bila kujibakiza.
Mbinu sahihi mbele ya janga kama hili ni lazima kuepuke uwongo kati ya sayansi na dini, na lazima pia zitoe vikundi vya uongozi wa kuhamasisha na kukuza mshikamano wa kijamii. Viongozi wa kidini na wataalimungu wana jukumu la ziada la kuimarisha misingi ya imani yao ya kulinda jamii kutokana na machafuko na migogoro, huku wakikumbuka nguvu ya milele ya Mwenyezi Mungu, katika kukuza sala na dua mbele ya Mungu, kukutana na dharura zingine za kisasa kama zile za dhuluma, ubaguzi, vikwazo vya kibinadamu, machafuko ya mazingira, vita, ugaidi, utengenezaji wa vyombo vya uharibifu.
Dhihirisho la mshikamano na uhamasishaji
Aidha Ayatollah Alireza Arafi anaongeza kuandika, katika siku hizi “tumeshuhudia dhihirisho lisiloelezeka la mshikamano maarufu na uhamasishaji ambao umeunganisha taasisi za serikali na watu wa vikundi vyote vya kidini, na umewaona wauguzi madaktari, wanafunzi, wasomi na vijana wengi, chini ya uongozi wa viongozi wakuu wa Mapinduzi ya Kiislam wakishimana na kushirikiana katika harakati za mapambano na virusi vya corona.