Tafuta

Continenti  Mondo Mappa Continenti Mondo Mappa 

Dunia#coronavirus:mtazamo wa hali halisi ulimwenguni!

Mtazamo wa Janga la mlipuko wa virusi vya Corona au COVID -19 ulimwenguni:licha ya mabaya ambayo yanaendelea kuonekana duniani,vifo,njaa,uchumi lakini pia limedhihirisha umuhimu wa teknolojia ya habari na mawasiliano kwa walio wengi.Wiki ya chanjo Duniani iliyozinduliwa na WHO,mefunguliwa tarehe 24 -30 Aprili,ikiongozwa na kaulimbiu:Chanjo hufanya kazi kwa kila mtu.

Na Sr.Angela Rwezaula-Vatican

Nchi 27 za Ulaya zimekuwa na wamekubaliana  kuwa na kanuni ya mfuko wa dharura wa Jumuiya ya Ulaya, lakini bado wamegawanyika kwa upande wa ufadhili wake. Uamuzi huo umehairishwa hadi Mei. Marekani imeidhinisha karibu dola nusu bilioni katika mpango mpya wa kuuokoa uchumi, wakati huu ulimwenguni wakipambana na kutafuta mbinu za kuuokoa uchumi unaoathirika kwa janga la virusi vya corona. Mswada huo tayari ulikuwa umeidhinishwa na Baraza la Seneti, na Rais Donald Trump ameashiria kwamba atausaini haraka iwezekanavyo kuwa sheria. Mpango huo unaongeza kwa ule wa trilioni 2.2 ulioidhinishwa mwishoni mwa Mwezi Machi mwaka huu. Karibu watu 50,000 wamefariki dunia nchini Marekani kutokana na virusi vya corona, kati yao 3,100 katika masaa 24 huku idadi ya walioambukizwa ikifikia 866,646.

Kwa upande wa Ulaya 2/3  ya jumla ya vifo na  Shirika la Afya Duniani WHO inathibitisha  juu ya kuwa ni hali ya janga lisilowezekana la wanadamu. Karibu nusu ya waathirika katika bara la zamani  wamekufa katika majumba ya kutunzia wazee. Na huko Uingereza itazindua mpango mkubwa wa kupima wafanyakazi wote katika sekta muhimu, ikiunganisha pamoja na wafanyakazi wa afya, walimu na polisi.

Katika nchi za Ghuba ya Uajemi, waathirika  wa kwanza ni wafanyakazi wa kigeni ambao wanalala katika vyumba vidogo wamelundikiana sana. Hawa wanawakilisha asilimia 70-80%  chanya. Amerika ya Kati: msimu wa mvua unaogopesha kuzuka kwa janga la Dengue, katika nchi ambayo tayari zinakabiliwa na covid-19 na vituo vya afya vilivyojaa kabisa. Na kwa upande wa Sekta ya utalii imeharibiwa sana, ikiwa na asilimia  10% tu ya ndege ambazo zimeendelea kufanya kazi.

Shirika la Afya Duniani WHO:   Wiki ya chanjo ya Dunia iliyozinduliwa na WHO, mefunguliwa tarehe 24 -30 Aprili, ikiongozwa na kaulimbiu “Chanjo hufanya kazi kwa kila mtu”. Hii inakusudia kukuza utumiaji wa chanjo katika kulinda watu wa kila kizazi dhidi ya magonjwa. Chanjo huokoa mamilioni ya maisha kila mwaka na inatambulika sana kama moja wapo ya mafanikio zaidi na ya gharama ya afya kuingilia kati. Licha ya kufanya hivyo lakini, bado kuna watoto milioni 20 ulimwenguni leo hii ambao hawapati chanjo wanayohitaji.  Kwa kuzingatia kwamba Shirika la Afrya Ulimwenguni WHO imeteua mwaka 2020 kuwa  Mwaka wa wauguzi na wakunga itaweza  kuangazia wauguzi na wakunga kwa jukumu lao muhimu kama mabingwa wa chanjo ya mapema kwa wazazi wapya na wazazi watarajiwa (LINK)

Msumbiji:Chama kikuu cha upinzaji (Renamo), kinashutumu vikosi vya usalama kwa kuwauwa raia 14 tarehe 23 Aprili  katika wilaya za kaskazini ya  Cabo Delgado, lililolengwa kila mara na vikundi vya jihadi

Guinea Bissau: Jumuiya ya Uchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS) imetambua rasmi Umaro Sissoco Embalo kama rais wa nchi ya  Guinea-Bissau, baada ya miezi nne ya kudorora kwa uchaguzi baada ya uchaguzi uliofanyika. Mwezi mmoja baada ya duru ya pili ya uchaguzi wa urais uliyofanyika Desemba 29, mvutano uliendelea kujitokeza kati ya Umaro Sissoco Embalo, kutoka chama cha upinzaji, na Domingos Simoes Pereira, mgombea wa PAIGC, chama ambacho kimetawala Guinea-Bissau kwa miongo kadhaa. Na hatimaye Jumuiya ya Uchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS) baada ya hatua za kipekee kuchukuliwa za uchunguzi imefikia muafaka huo.

Armenia: Tarehe 24 Machi ni Siku ya kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari ya Armenia. Hii ni katika kukumbuka Warmeni milioni 1.5 waliouawa kati ya mwaka 1915 na 1923 nchini Uturuki. Kwa sababu ya virusi vya corona  gwaride la kiutamaduni huko Yerevan limefutwa.

Mazingira: mgomo wa hali ya hewa duniani, uliokuwa ukifanyika kila Ijumaa , kwa sasa ipo katika mpango wa siku zijazo na Mkutano wa Ulaya wa “Green future Europe”, ambao labda utafanyika kwa njia ya video.

24 April 2020, 11:12