Tafuta

Vatican News
Mji wa New York umepokea barakoa kutoka Umoja wa Mataifa kwa ajili ya wahudumu. Mji wa New York umepokea barakoa kutoka Umoja wa Mataifa kwa ajili ya wahudumu.  (ANSA)

New York, Marekani wapokea msaada wa barakoa 250,000 kutoka umoja wa mataifa!

Umoja wa Mataifa umetoa msaada wa barakoa 250,000 zilizo kwenye maduka ya Umoja wa Mataifa mjini New York kwa serikali ya Marekani kusaidia wahudumu ambao wako mstari wa mbele katika harakati za janga hili jijini humo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Antonio Guterres tarehe 28 Machi 2020 ametangaza kwamba pamoja na balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Kelly Craft wametoa msaada wa barakoa 250,000 zilizo kwenye maduka ya Umoja wa Mataifa mjini New York kwa serikali ya Marekani.

Katika taarifa iliyotolewa na msemaji wake Bwana  Guterres amesema barakoa hizo ambazo ni za ziada baada ya kutimiza mahitaji ya Umoja wa Mataifa zitagatolewa kwa wahudumu wa afya mjini New York ambao wamejikita kwa sasa katika kazi kubwa ya ujasiri, na kujitoa bila kuchoka katika kukabiliana na kusambaa kwa mlipuko wa virusi vya Corona yaani COVID-19 katika mabara zote za mji huo  na ambapo ni matumaini kuwa zitasaidia hata kama ni kiasi kidogo kuokoa maisha.

Katibu Mkuu amesema wanaongea kwa sauti moja kuonyesha mshikamano wao kwa mji huo mzuri na watu wake. Kwa upande wao New York sio tu kwamna ni nyumbani kwao au makao makuu ya Umoja wa Mataifa balo ni  mji mashuhuri wa kimataifa ambao kupitia mji huo dunia unawasiliana , kujadiliana, kufanya biashara na kushamiri. Kwa niaba ya jumuiya ya Umoja wa Mataifa na wanadiplomasia ni matumaini yao kuwa mchango huu mdogo utaleta mabadiliko. Umoja wa Mataifa na wafanyakazi wa ubalozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa kwa sasa wanashirikiana na ofisi ya meya wa jiji la New York kuhakikisha kwamba vifaa hivyo vya msaada vinafikishwa kwa njia nzuri na salama kwenye vituo vya afya katika maeneo yote ya mji wa New York.

Na  Mratibu maalum wa Umoja wa Mataifa katika mchakato wa amani ya Mashariki ya Kati Nikolay Mladenov amepongeza ushirika baina ya mamlaka ya Palestina na Israel katika kukabiliana na mlipuko wa virusi vya Corona, COVID-19. Bwana Mladenov ametoa pongezi hizo wakati wa mazungumzo kwa njia ya simu na wajumbe wengine wa kundi la pande nne la upatanisho wa  Mashariki ya Kati ujulikanal kama Quartet. Kundi hilo linajumuisha Muungano wa Ulaya, Urusi, Marekani na Umoja wa Mataifa .

Katika mazungumzo hayo kwa njia ya simu yaliyofanyika alhamisi  26 Machi Bwana Mladenov alitoa maelezo ya kina kuhusu mpango wa Umoja wa Mataifa dhidi ya COVID-19 ukijikita zaidi Gaza ambako kuna hatari kubwa ya kusambaa kwa ugonjwa huo. Katika taarifa iliyotolewa Ijumaa 27 Machi 2020  uratibu na ushirikiano ulioanzishwa baina ya Israel na Palestina kuhusu kukabiliana na COVID-19 umeelezwa kuwa ni mzuri sana.

Israel na Palestina wanaendelea kuratibu hatua zao za pamoja kwa karibu na kwa nia njema taarifa hiyo ilisema, kitu ambacho ni suala kubwa katika mafanikio ya kudhubiti ugonjwa huo hadi sasa. Serikali ya Israel imearifu kuhusu hatua zilizoidhinishwa kudhibiti watu kutoka sehemu moja kwenda nyingine na biashara, ikiwemo kufungwa kwa shule na kupiga marufuku mikusanyiko , huku waziri mkuu wa Palestina akiripotiwa kuamuru kutotembea na kutoka nje Jumapili usiku. Tangu kuzuka kwa COVID-19 Israel imeruhusu kuingia kwa vifaa na bidhaa muhimu Gaza kwa mfano vifaa vya kukusanya vipimo kwa ajili ya kubaini COVID-19 na vifaa vingine vya maabara vinavyohitajika kwa ajili ya upimaji , na vifaa vya kujikinga kwa ajili ya wahudumu wa afya. Taarifa hiyo pia imeelezea ushirikiano wa Israel katika kuruhusu wahudumu wa afya na watu wengine wanaohusika katika kukabiliana na COVID-19 kuuingia na kutoka Ukingo wa Magharibi na Gaza.

29 March 2020, 16:00