Tafuta

Vatican News
Mlipuko wa COVIDI-19 ni janga kubwa la kidunia.Tunakiwa kufuata masharti yaliyowekwa katika kukabiliana na janga hili la maambukizi ya Virusi vya Corona. Mlipuko wa COVIDI-19 ni janga kubwa la kidunia.Tunakiwa kufuata masharti yaliyowekwa katika kukabiliana na janga hili la maambukizi ya Virusi vya Corona.  (©Romolo Tavani - stock.adobe.com)

Mtazamo katika dunia kuhusu maambukizi ya COVID-19!

Waziri Mkuu wa Italia Bwana Giuseppe Conte ametoa wito kwa Umoja wa Ulaya kutumia uwezo wao imara wa fedha ili kupambana na mlipuko wa Corona.Janga hili kuanzia kuskazini hadi kusini;Mashariki na Magharibi mwa dunia ni tishio la COVID-19.Kwa wastani maambukizi haya yameendelea kuzua hali ya wasiwasi katika mataifa yote duniani,hasa barani Ulaya na mipaka yake yote.

Maduka mengi ya kimataifa tarehe 19 Machi 2020 yamemehaidi  kutoa chanjo ulimwenguni dhidi ya Covid-19 kufikia muda kwa wastani wa miezi 12 hadi 18. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Alhamisi hiyo, nchini Italia imekuwa ni nchi yenye idadi kubwa ya vifo kuliko nchini China. Hata hivyo Nchini Uingereza pia imewaomba madaktari wastaafu kurudi kazini ili kusaidia kukabiliana na janga la Corona. Baraza la wauguzi na wakunga nchini Uingereza limewaandikia barua zaidi ya wauguzi 50,000 pamoja na madaktari 15,000 waliostaafu ili kurudi kazini kwa ajili ya kusaidia kupambana na janga la virusi vya Corona. Suala hili pia la kuwarudisha wakunga na madaktari wastaafu limefanyika nchini Italia hata wauguzi na madaktari wapya ambao walikuwa hawajapata ajira na zaidi ambao wamepata shahada hivi karibuni, wote wamealikwa kushiriki kusaidia dharura hii. Kufuatia na janga hili Waziri mkuu wa Italia Bwana Conti ametoa wito kwa Umoja wa Ulaya kutumia uwezo wake imara wa kifedha katika kupambana na janga la Corona.

Italia: Kwa sasa nchini Italia imefunga na kusimamisha shughuli katika bandari zake katika hali ya kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona. Wizara ya uchukuzi imeziagiza meli ambazo tayari ziko baharini kurudi bandarini na watu wote kufanyiwa vipimo. Jumla ya vifo vilivyotokana na Corona nchini Italia vimepita nchi ya China kufikia Alhamisi 19 Machi 2020. Kwa sasa, vifo vilivyotokana na virusi vya Corona vimefikia 3,405.

Na nchini Ufaransa, serikali imewaondolea hofu wafanyakazi kwa kusisitiza kuwa ina fedha za kutosha kuiwezesha kulipa mishahara ya wafanyakazi wake wakati huu wa janga la Corona. Waziri wa fedha Bruno Le Maire amesema hayo kupitia runinga ya LC. Kadhalika wanafunzi wanaosomea taaluma ya matibabu ambao wako mwaka wao wa mwisho pia wamepewa nafasi muhimu kutumia ujuzi wao kukabiliana na virusi hivyo.

Hispania: Jiji la Madrid, ni kitovu cha janga nchini Hispania na hivyo wamezindua , programu ya kutathmini dalili zake.Uhispania zimeungana na Italia kutangaza kusitishwa kwa shughuli za kawaida katika nchi zao, huku Austria ikiwataka raia wote wa kigeni wanaowasili nchini humo kujitenga ikiwa ni mikakati ya kupambana na virusi vya Corona. Kwa wastani maambukizi haya yameendelea kuzua hali ya wasiwasi katika mataifa mbalimbami duniani, hasa barani Ulaya na mipaka yake yote. Ikumbukwe mataifa mengi yamepiga marufuku mikusanyiko ya watu na shughuli zingine kama vile michezo ili kuepuka mikusanyiko ya watu lakini pia safari za kimataifa kusitishwa.

Siku mbili nchini China bila maambukizi: Shughuli zimeanza kurudi kama kawaida nchini China, katika ishara kuwa nchi hiyo imefanikiwa kwa kiwango kikubwa kudhibiti kuenea kwa virusi vya Corona licha ya kuwa kiini cha mlipuko vya virusi hivyo, ambapo kwa siku mbili mfululizo hapakuwapo na maambukizi. Kwa wakati huu, China imeweka mikakati ya kudhibiti kusambaa kwa virusi hivyo kwa kuhamasisha umma kuhusu umuhimu wa kuvaa barakoa na pia kupima viwango vya joto mwilini kwa watu wanaoingia katika maeneo ya umma. Hata hivyo mnamo Machi 10  Rais Xi Jinping alikuwa ametangaza wakati wa ziara yake katika mji wa Wuhan ambao ulikuwa kitovu cha mlipuko wa virusi vya Corona, kuwa nchi hiyo inakaribia kupata ushindi dhidi ya janga hilo la COVID-19 huku nao wachambuzi wa kiuchumi wakisema kuwa asilimia 90 ya biashara katika eneo la Hubei zimerudia hali yake ya kawaida.

Nchini Korea Kusini imetangaza kwamba visa vya maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19 vimeongeze, baada ya kupungua kwa visa vilivyothibitishwa siku kadhaa zilizopita. Hali hiyo inajiri wakati mlipuko mpya wa janga hilo umeonekana katika kituo cha kuwahudumia watu waliostaafu huko Daegu, mji wa Kusini mwa Korea Kusini, ulioathirika zaidi na virusi hivyo. Katika taarifa yake ya kila siku, Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (KCDC) kimeripoti kesi mpya 152 zilizothibitishwa, na kufikisha jumla ya maambukizo nchini kufikia 8,565. Chini ya visa 100 vya maambukizi viliripotiwa katika siku nne zilizopita. Kati ya kesi hizo mpya, 97 zimeripotiwa huko Seoul, ikiwa ni pamoja na wagonjwa 74 katika kituo cha kuwahudumia watu waliostaafu ambao walipimwa wiki hii, Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (KCDC) kimesema

Rwanda imethibitisha kesi 11 za maambukizi ya virusi vinavyo sababisha ugonjwa hatari wa Covid-19 nchini humo. Tayari, bei ya vyakula na bidha muhimu zimeendelea kuongezeka kwenye masoko mbalimbali, na sekta ya utalii imeathirika sana. Katika kukabiliana na hali hiyo, mamlaka ya nchi hiyo imetangaza hatua kadhaa kukabiliana na kupanda kwa bei kiholela. Mojawapo ya sekta zilizoathiriwa zaidi ni sekta ya utalii. Angalau matukio 20 yaliyokuwa yamepangwa kufanyika mwezi Machi na Aprili yamesogezwa mbele, kwa hali hiyo Rwanda itapoteza euro milioni 7, kulingana na Ofisi ya kukusanya mapato ya Rwanda.

Marekani, kwa masaa 24 maambukizi yamezidi  mara dufu  na sheria ya kuwalazimisha watu wakae nyumbani ndiyo inaendelea kutolewa. Kando na Jiji la New York na Washington, California ni miongoni mwa majimbo yaliyozongwa na janga la coronavirus. Alhamisi  tarehe 19 Machi 2020 pekee yake , rekodi ya maambukizi ya Covid-19 katika Jiji la New York ilionyesha kuongezeka mara dufu na kufikia hadi watu 3,954 - ikiwa ni kubwa kuliko watu idadi ya wagonjwa wa coronavirus katika nchi nzima. Meya Bill de Blasio aliiambia CNN kuwa jimbo hilo maarufu nchini Marekani litakosa vifaa vya kimatibabu katika kipindi cha wiki tatu ikiwa mlipuko wa maambukizi utaendelea kwa kiwango cha aina hiyo. Kwa maana hiyo ameitaka serikali ya shirikisho kuisaidi New York kupata vifaa vya kusaidia kupumua 15,000, barakoa za upasuaji milioni 50  na magauni ya 45 million, na vifaa vya madaktari vya kujikinga.

Afrika Kusini, kama nchi nyingine kuwa maambukizi ya virusi na hivyo   Rais wa Afrika Kusini Cyrille Ramaphosa alitangaza kusitishwa kwa safari kutokea katika mataifa yenye  tishio kubwa la Covid-19  kama Italia , Ujerumani, China na Marekani. Vile vile mtu yeyote ambaye ataeneza habari za uwongo kuhusu coronavirus sasa atakabiliwa na adhabu kubwa ya miezi sita gerezani, kulingana na sheria mpya

Zimbabwe wauguzi walalamikia ukosefu wa maandalizi kwa kitisho cha Covid-19 Ugonjwa wa Covid-19 umeendelea kuwa gumzo na kitisho kwa nchi za Kusini mwa Afrika ambazo hazijaathirika na ugonjwa huo sana , hususan Zimbabwe. Zimbabwe ambayo ni jirani na Afrika Kusini ambayo ina visa vya maambukizi zaidi ya 100, haijafunga mipaka yake na nchi hiyo. Hata hivyo Jumatatu 16 Machi 2020 rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa, alikuwa emetangaza janga la asili kufuatia mlipuko wa janga la Corona. Lakini mipaka inaendelea kuwa wazi, hali ambayo imezua wasiwasi mwingi kwa sababu Afrika Kusini, ambayo ni jirani ya Zimbabwe, tayari ina visa vya maambukizi zaidi ya 100 vilivothibitishwa.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo  DRC imetangaza visa 14 vya maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19 nchini humo. Rais wa DRC Félix Tshisekedi ametangaza hatua za kukabiliana na kuenea kwa virusi vya ugonjwa huo, ambao shirika la Afya Ulimwenguni, (WHO), limetoa kauli ya kuwa ni janga la kimataifa.

Bara la Afrika  hadi wiki iliopita ilikuwa bado imenusurika na virusi hivyo hadi kesi chache kuanza kuripotiwa. Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa WHO  limetangaza Jumatatu  16 Machi 2020 kuwa barani Afrika katika mataifa 28 ni watu 350 ndio waliokutwa na virusi vya corona baada ya kupimwa. Nchini Benin, mtu wa kwanza kukutwa na virusi hivyo ni mwanamume mwenye umri wa miaka 49  na raia wa Burkinafaso ambaye aliwasili nchini Benin kunako Machi 12.

Tanzania haikunusurika na virusi hivyo na  inaendelea kukabiliwa na ongezeko la visa vya maambukizi ya ugonjwa hatari wa Covid-19. Baada ya mtu wa kwanza, raia wa Tanzania kubainika na virusi vya ugonjwa huo. Mwanamke huyo aliyekutwa na virusi ana umri wa miaka 46 ambaye aliwasili  nchini Tanzania akitokea nchini Ubeligiji tarehe 15 Machi 20. Visa vingine vipya viwili vimeripotiwa kisiwani Zanzibar na Dar es Salaam. Hata hivyo mataifa jirani yametangaza pia kuchukuwa hatua zinazostahili  kuzuia kujipenyeza kwa virusi hivyo.

Amerika ya Kusini: Nchini Brazili nayo imezuia watu kuingia au kutoka kwenda nchi za Ulaya na Asia. Vile vile hata nchini Argentina nayo imeweka sheria ya kuzuizi kuingia na kutoka ndani na nje ya nchi na hivyo imewekwa karantini.

20 March 2020, 12:35