Tafuta

Vatican News
2018-02-06 donne africane 2018-02-06 donne africane 

Sitisha ukeketaji kwa wanawake,nchi 30 bado zinakabiliwa na janga hili!

Katika siku ya Kimataifa ya kupinga ukeketeji duniani Umoja wa mataifa kupitia mashirika yake unabainisha juu ya hatari iliyopo.Hata leo hii kuna waathirika wengi karibia nchi 30 za Bara la Afrika,Asia lakini hata katika nchi ambazo wameingia wahamiaji. Kwa mfano Ulaya.Nchi 26 Barani Afrika na Mashariki ya kati zimeweka sheria ya wazi dhidi ya ukeketaji,pamoja na nchi 33 zenye wahamiaji kutoka nchi zenye vitendo vya ukeketaji.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Wakati wa kuchukua hatua ni sasa ili kutokomeza ukeketaji au FGM, ifikapo mwaka 2030 kuwa sufuri wanawake na wasichana.  Kwa mara nyingine tena ni  wito wa pamoja umetolewa tarehe 6 Februari 2020 wakati wa kuadhimishwa siku ya kimataifa ya kupinga ukeketaji na wakuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa: la idadi ya watu UNFPA, Dk. Natalia Kanem, la kuhudumia watoto UNICEF, Henrietta Fore na la linaloshughulika na masuala ya wanawake UN Women, Phumzile Mlambo-Ngcuka na  la Afya Duniani (WHO ) Dk Tedros Adhanom Ghebreyesus.

Wanawake milioni 4 kwa mwaka huu wako hatarini

Kwa mujibu wa taarifa kutoka mashirika haya wanathibitisha kwamba karibia milioni 200 ya wanawake na watoto wamepata janga la ukeketaji: na mwaka huu kuna hatari ya wasichana milioni 4; na 68 milioni ya wasichana wadogo na wanawake kuwa hatarini kufikia mwaka 2030. “Ni sasa kutimiza ahadi tulizojiwekea ili kufikia zero katika suala la ukeketaji kufika 2030. Pamoja na hayo yote pia shirila la afya duniani WHO limesema kitendo hicho kinadhoofisha uchumi pamoja na nguvu kazi. 

Ukeketaji unaathiri wasichana na wanawake na gharama ya matibabu ni dola bilioni 1.4 kwa mwaka kimataifa

Shirika la Afya Duniani WHO limesema siyo tu kwamba ukeketaji ni ukiukaji wa haki za binadamu lakini unaathiri afya kimwili na kiakili kwa mamilioni ya wasichana na wanawake na pia kutumia raslimali nyingi muhimu za nchi na kwamba uwekezaji zaidi unahitajika kumaliza ukeketaji na madhala unaosababisha. Kwa mujibu wa makadirio mapya gharama ya matibabu kutokana na athari za ukeketaji huenda ikafika dola bilioni 1.4 kimataifa kwa mwaka iwapo mahitaji yote ya kiafya yatashughulikiwa. Katika nchi binafsi, gharama hii inakaribia asilimia 10 ya matumizi ya mwaka mzima ya afya kwa wastani ambapo katika baadhi ya nchi idadi hii huenda ikafika asilimia 30.

Wasichana na wanawake wanakabiliwa na hatari ya afya

Aidha WHO imesema wanawake na wasichana waathirika wa ukeketaji wanakabiliwa na hatari kubwa katika afya yao na uzima, hii ni pamoja na athari pindi tu baada ya kukeketwa ikiwemo: maambukizi, kuvuja damu nyingi au kiwewe pamoja na magonjwa ya muda mrefu ambayo huenda yakatokea maishani. Pia wanawake ambao wamekeketwa wana uwezekano mkubwa wa kupata tishio la kupoteza maisha wakati wa kujifungua, kukabiliwa na magonjwa ya akili na maambukizi ya muda mrefu. Pia huenda wakahisi uchungu wakati wa siku zao za mwezi, wakienda haja ndogo au wakati wa kitendo cha kujamiana. Inabidi iwe ni kwa kutangaza kwenye radio au televisheni au kuzungumzwa na watu wote kwamba ujumbe ni kutokomeza ukeketaji, iwapo hatutatokomeza kitendo hicho basi vizazi vijavyo vitaendeleza ukeketaji. Ni lazima tuusitishe hapa.

Tangu mwaka 1997 hatua zimepigwa katika kutokomeza ukeketaji kupitia kazi ndani ya jamii

Kwa kutumia takwimu za nchi 27 zilizo na visa vingi vya ukeketaji, makadirio ya kiuchumi yanaonesha faida za wazi za kiuchumi kufuatia kutokomeza ukeketaji. Iwapo kitendo hicho kitatokomezwa zaidi ya asilimia 60 kutokana na gharama za kiafya zingeweza kuokolewa. Tangu mwaka 1997 hatua zimepigwa katika kutokomeza ukeketaji kupitia kazi ndani ya jamii, utafiti na marekebisho katika sheria na sera. Nchi 26 Barani Afrika na Mashariki ya kati zimeweka sheria ya wazi dhidi ya ukeketaji, pamoja na nchi 33 zilizo na wahamiaji kutoka nchi kunakofanyika vitendo vya ukeketaji. Ukeketaji unatambulika kama ukiukaji wa haki za binadamu na hauna faida zozote za kiafya na unasababisha madhara. WHO inashikilia msimamo wake kwamba ukeketaji haupaswi kutekelezwa waka

06 February 2020, 17:04