Tafuta

Tarehe 12 Februari ni siku ya kimataifa ya kupinga matumizi ya watoto kama askari Tarehe 12 Februari ni siku ya kimataifa ya kupinga matumizi ya watoto kama askari 

Siku ya kimataifa ya kupinga matumizi ya watoto kama askari!

Ingawa watoto hawana jukumu kubwa katika vita,mamilioni ya watoto miongoni mwao wanajikuta katikati ya machafuko ambayo sio watazamaji bali walengwa.Wamesema hayo Umoja wa Mataifa wakati ukizindua muongozo wa kuwalinda watoto katika hali za vita kwenye kilele cha siku ya ya kimataifa ya kupinga matumizi ya watoto kama askari tarehe.

Katika uzinduzi uliofanyika tarehe 12 Febrari 2020 katika siku ya kimataifa ya kupinga matumizi ya watoto kama askari kwenye kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kilichojikita na ujumuishwaji wa ulinzi wa watoto katika michakato ya amani Katibu Mkuu wa Umoja huo Antonio Guterres amesema watoto wapatao milioni 250 wanaishi katika nchi zilizoathirika na migogoro. Ameongeza kuwa watoto wa umri wa chini ya miaka 18 ni zaidi ya asilimia 50 ya watu wote walioko katika nchi zilizoathirika na vita, wako katika hatari na hawawezi kujilinda na athari za vita hivyo.

Mwaka 2018 zaidi ya watoto 12,000 waliuawa au kujeruhiwa katika vita ikiwa ni idadi kubwa Zaidi kurekkodiwa tangu mwaka 1996 wakati Baraza Kuu lilipoanzia jukumu la mwakilishi maalum kuhusu watoto na mizozo ya silaha. Visa hivyo viliorodheshwa na kuthibitisha Zaidi ya matukio 24,000 ya ukiukwaji iikilinganishwa na 21,000 mwaka 2017.” Amesema Bwana Guterres.

Shirika la kimataifa la misaada la Save the Children pia tarehe 12 Februari  limetoa wito  kwa serikali za ulimwengu kuchukua hatua zaidi za kuwalinda watoto kutokana na athari za vita na machafuko, baada ya ripoti mpya kueleza kuwa idadi kubwa ya watoto wanaishi kwenye maeneo yenye mizozo. Save the Children limesema vita vimeendelea kuwa hatari kwa watoto, ambao wanakabiliwa na kuongezeka kwa kitisho cha kufariki na kujeruhiwa, kupewa mafunzo na makundi ya wanamgambo wenye silaha ama unyanyasaji wa kingono.

Tangu mwaka 2005, karibu watoto 95,000 walirekodiwa kuuawa ama kujeruhiwa, maelfu ya watoto kutekwa na mamilioni kushindwa kupata elimu ama huduma za afya baada ya hospitali zao kushambuliwa. Shirika hilo limesema karibu mtoto mmoja kati ya sita miongoni mwa watoto milioni 415 ulimwenguni walikuwa wanaishi kwenye maeneo ya mizozo mwaka 2018, idadi hiyo ikiwa ni mara mbili zaidi ya iliyorekodiwa mwaka 1995.

13 February 2020, 17:54