Tafuta

Vatican News
Mauaji ya kinyama yanaendelea nchini Burkina Faso Mauaji ya kinyama yanaendelea nchini Burkina Faso  (AFP or licensors)

Burkina Faso:Shambulizi la Kanisa la kiprotestanti

Watu karibia 24 wameuawa kati yao mchungaji wa Kanisa la kiprotestanti na watu 18 wamejeruhiwa katika shambulizi la kijiji kimoja Kaskazini mwa Burkina Faso.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Waamini karibia 24 wameuwawa siku ya Jumapili tarehe 16 Februari 2020 nchini Burkna Faso na watu wenye silaha katika Kanisa la Pansy, Kaskazini mashariki mwa nchi  hiyo wakati waamini wanafanya ibada yao na mchungaji wao pia watu 18 kujeruhiwa. Janga hili linajitokeza baada ya siku chache kutekwa nyara na kuuwawa kwa mtawa mmoja na familia yake. Mashambulizi ya makanisa kaskazini mwa Burkina Faso yanadaiwa kufanywa na makundi ya kijihadi ambayo yanazidi kuongezeka siku hadi siku  katika ukanda huo licha ya uwepo wa operesheni ya kuwakabili. Hata hivyo makundi hayo yapo pia Mali na  Niger.  

Kuanzia 2018 hadi sasa mashambulizi yamekuwa takiwalenga wakristo katika ibada mbalimbali kanisani. Hata hivyo wataalam wanasema kuwa mara nyingi wakristo ambao ni wachache wamekuwa wakikabiliana na vurugu na kushambuliwa na wanajihadi ambapo Burkina Faso imekuwa na historia ya muda mrefu ya uvumilivu wa kidini ba ukosefu wa amani na migogoro imefanya wanajihadi kuweza kutawala eneo hilo.

Askofu mkuu wa  Ouagadougou amesisitiza juu ya uwepo wa soko la silaha kwamba nchini Burkina Faso, Mali na  Niger ni matatizo hayo ya kutisha yanayo sababisha na makundi yanayofanya mashambulizi. Kuna haja ya kufanya mshikamano wa kimataifa kwa ajili ya kusitisha soko la silaha linalosadia watu wengi wawaue ndugu zao bila sababu amesisitiza Askofu Mkuu kwa masikitiko makubwa.

17 February 2020, 18:01