Tafuta

Vatican News
Hatimaye mkataba wa makubalino ya kusitisha migogoro kati ya serikali ya Sudan Kusini na vyama vya upinzani imetiwa sahini na ili kuanza kutumika tarehe 15 Januari 2020 Hatimaye mkataba wa makubalino ya kusitisha migogoro kati ya serikali ya Sudan Kusini na vyama vya upinzani imetiwa sahini na ili kuanza kutumika tarehe 15 Januari 2020  (AFP or licensors)

Sudan Kusini:Hati ya Roma kwa ajili ya kusitisha misuguano ya kivita!

Hati mpya ya tamko imewakilishwa na kusahiniwa katika jumuiya ya Mtakatifu Egidio ambapo Serikali na muungano wa vyama vya upinzani vya Sudan Kusini (Ssoma) vimeahidi kufanya jitihada za kusitisha misuguano ambayo imedumu kwa muda mrefu na makubaliano hayo yanaanza rasmi tarehe 15 Januari 2020.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tarehe 13  Januari wametia sahini katika Hati mpya kati ya Serikali na Mshikamano wa vyama vya upinzani vya Sudan Kusini (Ssoma) – ambavyo vinunganisha vyama vyote ambavyo havikuwa vimekubaliana na mkataba wa amani wa Addis Abeba, huku wakifafanua juu ya jitihada za kusitisha misuguano na ambapo tangu tarehe 15 Januari 2020 mkataba huo unaanza kufanya kazi. Sahini hiyo imewekwa na wawakilishi wa vyama hivyo mjini Roma katika Jumuiya ya Mtakatifu Egidio.

Hata hivi ikumbukwe ishara ya Papa Francisko aliyepiga magoti mbele ya viongozi wa Sudan Kusini kunako tarehe 11 Aprili 2019 katika fursa ya Mkutano mara baada ya mafungo ya kiroho mjini Vatican. Papa FRancisko aliwabusi miguu viongozi hao akiwambia waweze kumaliza migongano. Ishara hii kwa dhati iliwatia moyo wa kuweza kufikia hatimaye makubaliano ya mwisho wa misuguano hiyo kwa  sahini hiyo.

Kazi ya amani imefanywa kwa miaka miwili: Hati mpya Tamko la Roma kwa ajili ya mchakato wa amani nchini Sudan Kusini kwa mujibu wa Paolo Impagliazzo, katibu Mkuu wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio kwa waandishi wa habari wakati wa kuwakilisha amesema, ni jambo lenye umuhimu sana na makini kwa sababu ni matokeo ya kazi ya kina iliyodumu kwa miaka miwili hivvi na jitihada ambazo Jumuiya ya Mtakatifu Egidio umependa kujikita nayo  kwa harahi katika kuharahisisha majadiliano ya kisiasa nchini Sudan Kusini.

Makubalinao ya amani ina maana ya kuzaliwa kwa upya nchi hiyo na uwezekano wa mazungumzo ya kisiasa katika vyama tofauti katika mzunguko wa meza bila upinzani. Papa Francisko kwa ishara yake aligusa mioyo ya wengi na kupelekea kwa hakika hatua hii  katika kutafuta njia za maridhiano ya amani katika nchi ambayo inaendelea kuteseka na hasa watu walio wadhaifu.

 

 

15 January 2020, 12:10