Tafuta

Mwaka 2020 umeanzia pale ulipoachoia mwaka 2019 kwa matukio mabaya ya hali ya hewa na mabadiliko ya tabianchi. Kwa mfano wa nchi ya Australia ambapo moto uanedelea kuteketeza nchi hiyo Mwaka 2020 umeanzia pale ulipoachoia mwaka 2019 kwa matukio mabaya ya hali ya hewa na mabadiliko ya tabianchi. Kwa mfano wa nchi ya Australia ambapo moto uanedelea kuteketeza nchi hiyo 

Mwaka 2019 umekuwa wa joto kubwa hivyo ni dharura ya kidunia!

2019 unaelekzwa kuwa mwaka wa joto zaidi mbali na mwaka 2016.Shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO amesema viwango vya joto ni sehemu tu ya hadithi hii.Mwaka uliopita na muongo uliopita imeelezewa kuwa ni ya kuyeyuka kwa barafu,kuongezeka kwa kiwango cha kina cha baharí,ongezeko la joto baharini,ongezeko la tindikali kwenye maji na majira mabaya ya hali ya hewa.

Kumekuwa na mazungumzo ya miongo kadhaa ya mabadiliko ya tabianchi, lakini mbiu zimeanza kuongezeka tangu miaka ya 1980. Leo ni kati ya ajenda za kisiasa, mivutano ya kimataifa, mikakati ya kiuchumi na uhamasishaji wa watu.Kwa wa sababu hii Shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO leo limesema mwaka 2019 unashika  rekodi ya pili ya kuwa na joto zaidi duniani ukiachana na lile la mwaka 2016.

Tangazo la tarehe 15 Januari 2020 limefuatia tathimini ya kina ya ahali ya joto kwa mwaka 2019 na WMO inasema wastani wa joto katika kipindi cha miaka mitano iliyopita (2015-2019) na miaka kumi iliyopita (2010-2019) vipindi na viwango vya joto vilikuwa vya juu katika historia. Tangu miaka ya 1980 kila muongo umekuwa wa joto Kali kuliko uliotangulia. Na mwenendo huu unatarajiwa kuendelea kwa sababu ya ogezeko la joto hewani linalotokana na gesi ya viwandani

Kwa mujibu wa wastani wa seti za takwimu zilizokusanywa na kutumiwa kutoa tathimini hii kiwango cha joto cha kimataifa kwa mwaka 2919 kilikuwa nyuzi joto 1.1°C zaidi ya kiwango cha wastani kilichokuwa katika ya miaka 1850-1900, ambacho ndyio kilitumika kuelezea wastani wa kiwango cha joto katika nyakati za kabla ya mapinduzi ya viwanda.

Shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO inasema “Mwaka 2016 kunasalia kuwa ndio mwaka uliokuwa kiwango cha juu zaidi cha joto katika historia kwa sababu ya mchanganyiko wa matukio makubwa ya El Niño ambayo huwa yanaambatana na wimbi la joto Kali na mabadiliko ya muda mrefu ya tabianchi.” Katibu mkuu wa WMO Petteri Taalas amesema “Wastani wa kiwango cha joto duniani umeongezeka kwa takribani nyuzi joto 1.1°C tangu nyakati za kabla ya mapinduzi ya viwanda na kiwango cha joto baharini kimefikia rekodi ya juu zaidi. Na kwa mwendelezo wa sasa wa utoaji wa hewa chafuzi ya ukaa tunaelekea kwenye ongezeko la joto la nyuzi joto 3°C  hadi 5°C ifikapo mwisho wa karne hii.”

Mkuu  wa Shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO amesema viwango vya joto ni sehemu tu ya hadithi hii . Mwaka uliopita na muongo uliopita imeelezewa kuwa ni ya kuyeyuka kwa barafu, kuongezeka kwa kiwango cha kina cha baharí, ongezeko la joto baharini, ongezeko la tindikali kwenye maji na majira mabaya ya hali ya hewa.

Shirika hilo linasema haya yote yamesababisha athari mbaya kwa afya ya ustawi wa binadamu na mazingira. “Mwaka 2020 umeanzia pale ulipoachoia mwaka 2019 kwa matukio mabaya ya hali ya hewa na mabadiliko ya tabianchi. Australia ilishuhudia mwaka wenye joto kupindukia na kwenye ukame wa hali ya juu 2019 na kuwa mfano wa moto mkubwa wa nyika ambao  bado unaendelea hadi leo kuathiri watu, mali zao, wanyama pori, mfumo wa maisha na mazingira . Ni wakati sasa wa kutazama nini na wapi tunaelekea amesema Bwana. Taalas.

16 January 2020, 16:08