Tafuta

Vatican News
Kila tarehe 27 ya Januari kila mwaka inkumbusha mauaji ya maangamizi makubwa katika kambi ya Auschwitz-Birkenau Kila tarehe 27 ya Januari kila mwaka inkumbusha mauaji ya maangamizi makubwa katika kambi ya Auschwitz-Birkenau  

Mshikamo wahitajika kupinga kila aina ya chuki dhidi ya Wayahudi

Katika kufanya maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 75 tangu kukumbolewa kambi ya maangamizi makuu ya huko Auschwitz-Birkenau, ambayo imekuwa ishara ya kiyahudi. Papa Francisko amekumbusha kusali na kupinga vikali jambo hilo lisirudiwe tena.Wakati huo katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amehimiza,mshikamano wakati huu ambao kuna ongezeko la chuki dhidi ya wayahudi.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Mbele ya janga hili lisilo la kibinadamu, amesema Papa haikubaliki zile sintofahamu na hivyo ni muhimu kufanya kumbu kumbu. tarehe 27 Januari kila mmoja anakumbushwa  kusali kwa hilo huku akipinga suala hili lisirudiwe tena . Zaidi ya watu 200 walionusurika katika mauaji ya wayahudi pamoja na ujumbe kutoka nchi 50 wanakutana katika eneo ilikokuwa kambi ya mateso dhidi ya Wayahudi wakati wa utawala wa Wanazi, ya Auschwitz-Birkenau kwa ajili ya kumbukumbu ya miaka 75 ya kukombolewa kambi hiyo.

Lango kuu la kifo

Hafla kuu ya kumbukumbu ya Auschwitz-Birkenau imefanyika mbele ya kile kilichofahamika kama “Lango la Kifo,” ambalo liliwaingiza wahanga katika kambi kubwa kabisa ya kuwaangamiza Wayahudi. Rais wa Poland Andrej Duda ameongoza hafla hiyo, lakini hotuba kuu zimetolewa na walionusurika katika kambi hiyo. Katika taarifa iliyotolewa kabla ya kumbukumbu hiyo, Rais Duda alisema lazima tuangalie mustakabali wa dunia kwa kuelewa kwa undani kilichotokea miaka 75 iliyopita katikati ya Ulaya. Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeir na Rais wa Israel Reuven Rivlin walikuwa miongoni mwa wawakilishi wa zaidi nchi 50 na taasisi kadhaa za kimataifa ambao wametoa heshima zao kwa waliouawa Auschwitz na pia kwa wafungwa wa kambi hiyo.

Katibu Mkuu ametembelea sinagogi huko New York

Hata hivyo naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametembelea sinagogi, na kutoa heshima kwa waathirika wa mauaji ya maangamizi makuu Jumamosi tarehe 25 Januari 2020, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametembelea sinagogi la Park East mjini New York Marekani ambako ametoa heshima kwa waathirika wa mauaji ya maangamizi makuu yaani Holocaust. Hotuba ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenye sinagogi imekuja wakati huu ili kuendana na siku ya kimataifa ya kukumbuka mauaji ya maangamizi makubwa ambayo inaadhimishwa kila tarehe 27 ya mwezi Januari kila mwaka. Katika siku hii mnamo mwaka 1945, kambi ya Auschwitz ambayo pia ilifahamika kama Auschwitz-Birkenau ilikombolewa na jeshi la Sovieti. Kambi hii ilikuwa inatumika kuwafanyia ukatili mkubwa wayahudi. Akiwahutubia wale waliohudhuria katika sinagogi, Katibu Mkuu Guterres amesema, kuliko wakati mwingine wowote, mshikamano unahitaji hasa wakati huu ambao kuna ongezeko la chuki dhidi ya wayahudi na ongezeko la mashambulizi kwa wayahudi, ushirika wao na mali zao kote duniani ikiwemo New York.

Kulaani viongozi wanaochocje lugha za chuki

Aidha Katibu Mkuu ameeleza namna ambavyo unazi mamboleo unavyopata uungwaji mkono kutoka katika teknolojia ya sasa ya mawasiliano ya mitandao ya kijamii ambako chuki zinaenezwa na kueneza ubaguzi wa rangi na mambo mengine ambayo ni sumu kwa vijana wa umri mdogo. Bwana Guterres amesihi kuwa: “wanadamu kutosahau kuhusu somo walilolipata kutokana na janga kubwa na mauaji ya maangamizi makuu na zaidi wakatae lugha za chuki.” Aidha amewapinga vikali viongozi ambao wanataka umaarufu katika kutafuta mdaraka wanatumia lugha za chuki na kutengeneza mazingira ya hofu. Amesisitiza elimu itumike ili kupambana na ujinga.

27 January 2020, 14:11