Tafuta

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Antonio Guterres amesema, hakuna nchi, hakuna jumuiya ambayo peke yake inaweza kutatua matatizo magumu ya dunia yetu. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Antonio Guterres amesema, hakuna nchi, hakuna jumuiya ambayo peke yake inaweza kutatua matatizo magumu ya dunia yetu. 

Maadhimisho ya miaka 75 ya Umoja wa Mataifa yazinduliwa kwa majadiliano!

Imezinduliwa Majadiliano ya maadhimisho ya miaka 75 ya Umoja wa Mataifa, (UN75).Ni majadiliano makubwa ya pamoja kuhusu jukumu la ushirikiano wa kimataifa katika kujenga mstakabali bora kwa wote.Katika afla hiyo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa hakuna nchi,hakuna jumuiya ambayo peke yake inaweza kutatua matatizo magumu ya dunia yetu.Tunahitaji kuungana pamoja,siyo tu kuzungumza,lakini pia kusikiliza!

Tarehe 2 Februari  2020, imeshuhudiwa uzinduzi wa mkakati wa Umoja wa Mataifa wa majadiliano makubwa zaidi ya kimataifa kuhusu mstakabali wa dunia. Ni majadiliano makubwa ya pamoja kuhusu jukumu la ushirikiano wa kimataifa  katika kujenga mstakabali bora kwa wote. Mpango huo utashuhudia Umoja wa Mataifa ukichochea majadiliano katika mwaka huu  2020 kwenye mazingira tofauti duniani kote. Mijadala ya 75 ya Umoja wa Mataifa ni pamoja na ‘Uchunguzi wa dakika moja’ ambao mtu yeyote anaweza kuchukua, kupiga kura katika nchi 50 na uchambuzi wa akili bandia wa vyombo vya habari vya jadi na kijamii katika nchi 70, zitatoa data ya kulazimisha kujua sera za kitaifa na kimataifa na mjadala

Katika kutoa wito wa ushiriki, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  Bwana Antonio Guterres amesema, “hakuna nchi, hakuna jumuiya ambayo peke yake inaweza kutatua matatizo magumu ya dunia yetu. Tunahitaji kuungana pamoja, siyo tu kuzungumza, lakini pia kusikiliza. Ni muhimu pia kuwa nyote mshiriki katika mazungumzo. Tunahitaji maoni yenu, mikakati yenu na mawazo ili tuweze kuwahudumia vizuri watu wa ulimwengu ambao tunatakiwa kuwahudumia.”

Ikiwa na lengo la kuhusisha maeneo kadha katika kila mipaka, sekta mbalimbali na vizazi, timu ya UN75 inashirikiana na mtandao wa sekta ikijumuisha waratibu wakazi wa Umoja wa Mataifa, kwa ajili ya ufanikishaji wa kufikisha taarifa kote na majadiliano kufanyika katika kila nchi duniani. Katika zoezi la usikilizaji la ulimwengu, pamoja msisitizo kwa vijana na makundi ambayo hayajashirikishwa na Umoja wa Mataifa, mkakati wa UN75 unalenga kuelewa matarajio  ya ushirikiano wa kimataifa katika kushinikiza changamoto za ulimwengu. Maoni na mawazo ambayo yatatolewa, yatawasilishwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa viongozi wa Ulimwengu na maafisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa kunako tarehe 12 Septemba 2020, katika hafla ya ngazi ya juu ya kuadhimisha miaka 75 ya Umoja wa Mataifa.

02 January 2020, 16:01