Tafuta

Vatican News
Shirika la Saidia Watoto linathibitisha kuwa katika muungano wa nchi za Ulaya,karibia milioni 23 ya watoto wako hatari ya umaskini na kubaguliwa kijamii. Shirika la Saidia Watoto linathibitisha kuwa katika muungano wa nchi za Ulaya,karibia milioni 23 ya watoto wako hatari ya umaskini na kubaguliwa kijamii.  (ANSA)

Save the Children:karibia watoto milioni 23 Ulaya wako hatari ya umasikini kijamii!

Kwa mujibu wa Shirika la Saidia watoto(Save the Children)katika Muungano wa nchi za Ulaya,watoto karibia milioni 23 wako katika hatari ya umaskini na ubaguzi wa kijamii.Kwa maana hiyo umasikini wa utoto uwe ndiyo kitovu cha sera za kisiasa katika bara la Ulaya.Hawa ni watoto na viajana wanao lazimika kuishi katika hali mbaya sana kwenye makazi na ambayo hayana hduma za msingi kama joto, umeme na chakula.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Shirika la Saidia watoto litoa ombi la moja kwa moja kwa Wakuu wa nchi na Serikali, ili kuhakikishia rasilimali kwa ajili ya watoto wa kike na kiume katika hali ya ukosefu wa umakini kijamii na kiuchumi barani Ulaya na dunia nzima kwa ujumla. Umasikini kwa upande wa watoto barani Ulaya unawakilisha dharura kubwa na ambayo lazima ikabiliwe kwa haraka na iwe ndiyo kiovu cha mjadala wa sera za kisiasa.  Katika muungano wa nchi za Ulaya, karibia milioni 23 ya watoto wako hatari ya umaskini na kubaguliwa kijamii. Hawa ni watoto na vijoli ambao wanalazimika kuishi katika hali  mbaya sana kwenye makani, na mara nyingi nyumba zikiwa hazina huduma msingi, bila joto ndani, umemem au maji ya moto, bila uwezekano wa kupata mlo kamili wenye virutubisho na ukosefu wa elimu ya viwango. Katika fursa ya Mkutano wa Baraza la Ulaya ambao umefanyika siku mbili ya tarehe 12 na 13  Desemba 2019, wameanzisha mchakato wa mazungumzo juu ya bajeti ya Muungano wa Ulaya kwa  kipindi cha mwaka 2021-2027, Kwa maana hiyo Shirika la Saidia watoto limetumia fursa hiyo kutoa wito kwa Wakuu wa Nchi na Serikali, kuanzia kwa Rais wa Baraza la Muungano wa Ulaya Bwana  Giuseppe Conte, ili haki za watoto ziwe ndiyo kutovu cha ajenda ya kisiasa.

Watoto wanakua katika hali ya umaskini

Watoto ambao wanakulia katika mazingira ya hali ya umaskini ndiyo wanapoteza hata fursa za shule na kusababisha shida wakati wanaingia katika soko la ajira, viwango vya juu vya ukosefu wa ajira, mishahara ya chini au ajira za hatari. Kwa maana hiyo ni  muhimu zaidi kuhakikisha Udhamini wa Mtoto wa Ulaya, kuanzisha hatua inayolenga kupambana na umaskini wa watoto na kutengwa kwa watoto.  Haya yamelezwa na Rais wa Tume ya Ulaya, Bi  Ursula Von der Leyen, ambaye pia ameionyesha kama malengo ya kazi kwa Tume katika miaka ijayo. Hata hivyo pendekezo la Bunge la Ulaya ni kutenga bilioni € 5.9 ya Mfuko wa Kijamii wa Ulaya pamoja  kwa mwaka 2021-2027 ambayo ni (karibu asilimia 6% ya Mfuko huo)kwa utekelezaji wa Dhamana ya Mtoto wa Ulaya kwa ajili ya kupambana na umasikini wa watoto katika nchi za Muungano Ulaya. “Hii ni ishara kwamba tunakaribisha kwa pamoja na vigezo vipya vilivyopendekezwa na Tume katika ugawaji wa fedha za Ulaya ili kupunguza utofauti katika sehemu za Ulaya na ambayo inaweza kuongeza rasilimali zilizopewa nchi yao kupambana na umaskini wa watoto”. Amesema mwakilishi wa Shirika la Saidia watoto katika kitengo cha Ulaya.

Lazima kuonyesha jitihada

Baraza la Ulaya  anasisistiza Save the Children kwamba linaalikwa kuonyesha jitihada za dhati kwa watoto na vijana ili kusitisha umaskini wa watoto huko Ulaya na ulimwenguni kote , ambayo ni ahadi kuu ya Ajenda ya 2030 na Malengo ya Maendeleo endelevu. Katika kukabiliana na ongezeko la maendeleo ya changamoto za kidunia, Jumuiya ya nchi za Ulaya ina jukumu la kuonyesha uongozi wake pia katika utetezi wa mashirika ya kimataifa, ikijitosa kimaso maso katika mstari wa mbele juu ya maswala ya misaada ya maendeleo, umasikini wa ulimwengu, ukosefu wa usawa, na kipeo cha tabia nchi. Kwa mambo hayo yote, hata hivyo, inahitaji uwekezaji kwa ujasiri na wa kisiasa unaolenga watoto, kwa kutazama siku za usoni kwa lengo la kutomwacha mtoto yeyote nyuma, amehitimisha Bi Raffaela Milano wa Save the Children.

14 December 2019, 14:55