Tafuta

Wasiwasi wa Shirika la Kimataifa la Saidia watoto kufuatia na hatari ya karibia milioni 7 ya watoto kukumbwa na baridi kwa mwaka 2020 Wasiwasi wa Shirika la Kimataifa la Saidia watoto kufuatia na hatari ya karibia milioni 7 ya watoto kukumbwa na baridi kwa mwaka 2020 

Dharura ya baridi:karibia watoto milioni 7 watakumbwa na baridi 2020!

Baridi sana inazidi kukumba watoto karibia milioni 7 ambao kwa mwaka 2020 watakuwa nje ya nyumba zao wakitafuta namna ya kuondokana na hatari ya maisha kwa sababu ya kushuka sana kwa kiasi cha joto na kuanza baridi kali. Taarifa hizo ni kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Saidia watoto (Save the Children).

Ni milioni 6.9 za watoto ambao wanalazima kumaliza mwaka huu wakiwa nje wamerudikana na mbali na nyumba zao kwenye mahema mepesi, ni wakimbizi na zaidi hata katika maeneo yaliyo wazi huku wakihatarisha maisha yao kutokana na hali ya joto  kushuka hadi kifikia nyuzi 0. Hii ni dharura ambayo imetolewa tamko lake  tarehe 30 Desemba 2019 kwa mujibu wa Save the Children, Shirika la Kimataifa la Saidia watoto ambalo kwa miaka 100 linajikita kusaidia watoto ambao wako hatarini na kuwahakikishia wakati wao bora ujao na zaidi katika mkesha huu wa kufungua mwaka mpya.

Mamilioni ya watoto wamekimbia kutokana na migogoro ya kutisha na vurugu,huku  wakitafuta usalama. Lakini licha ya hayo katika maeneo mengine, kipindi cha baridi kinahatarisha tena maisha yao na kukosa mahali pa kukimbilia tena. Kipindi cha baridi mwaka jana  kwa wa Rachael Cummings, mhusika wa huduma ya Afya ya Save the Children amesema  wiki chache hali halisi ya hewa ilikuwa ya baridi sana na kuleta ugumu sana hadi kufikia watoto 15 nchini Siria kufariki dunia na ambao walikuwa wamekimbia vita kwa mujibu.

Watoto wanazidi kubeba gharama na kukumbwa na madhila wakati mizozo ikiendelea kushuhudiwa duniani, kwa mujibu wa ripoti ya shirika la kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa,UNICEF.  Aidha ripoti iliyotolewa tarehe 30 Desemba inasema tangu mwanzo wa muongo huu, Umoja wa Mataifa umethibitisha zaidi ya visa 170,000 vya ukiukaji mbaya wa haki za watoto sawa na zaidi ya visa 45 vinavyotokea kila siku kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita.

Idadi ya nchi zinazokumbwa na mizozo ni ya juu zaidi tangu kutiwa saini mkataba wa haki za watoto mwaka 1989, huku mizozo hiyo ikikatili maisha ya watoto hao na kuwalazimisha kuhama makwao. Mwaka 2018 Umoja wa Mataifa ulithibitisha zaidi ya visa 24,000 vya ukiukaji wa haki za watoto ikiwemo mauaji, dhuluma  za kingono, utekaji, kukosa huduma za msingi za binadamu, kuwaajiri watoto jeshini na mashambulizi hospitalini na shuleni.

Naye Mkurugenzi mtendaji wa UNICEF Henrietta Fore amesema, "vita vinavyoshuhudiwa kote duniani hivi sasa vinadumu kwa muda mrefu zaidi na kusababisha umwagaji damu mkubwa huku vikikatili maisha ya maelfu ya watoto na barubaru. Mashambulizi dhidi ya watoto yanaendelea bila kukoma wakati pande kinzani zikikiuka moja ya sheria za msingi kabisa za vita, kuwalinda watoto. Ingawa kila kitendo cha ukatili dhidi ya watoto kinachogonga vichwa vya habari kusababisha wito wa kulaani na kutaka hatua zichukuliewe, lakini bado kuna watoto wengi ambao hawalindwi.

31 December 2019, 16:43