Tafuta

Utupaji wa taka hovyo unaharibu afya ya umma,mazingira na hali ya hewa,lakini teknolojia na ununifu wa sasa unaweza kubadili taka kuwa gharama nafuu. Utupaji wa taka hovyo unaharibu afya ya umma,mazingira na hali ya hewa,lakini teknolojia na ununifu wa sasa unaweza kubadili taka kuwa gharama nafuu. 

Taka zinaleta madhara ya afya na mazingira:kuna zama za Sayansi na teknolojia!

Katika kilele cha Siku ya Makazi Duniani (UN-habitat) ifanyikayo kila Jumatatu ya kwanza ya mwezi Oktoba ambapo 2019 imengukia tarehe 7,ujumbe unasema kuwa taka zinaweza kuleta madhara makubwa kwa afya ya umma,mazingira na hali ya hewa,lakini katika zama hizi sayansi,teknolojia na ubunifu wa hali ya juu vinaweza kuleta suluhisho la gharama nafuu katika changamoto hiyo.

Katika kilele cha Siku ya Makazi duniani (UN-habitat) ifanyikayo kila  Jumatatu ya kwanza ya mwezi Oktoba ambapo mwaka 2019 imengukia  tarehe 7 ujumbe wake unasema kwamba taka zinaweza kuleta madhara makubwa kwa afya ya umma, mazingira na hali ya hewa, lakini katika zama hizi sayansi, teknolojia na ubunifu wa hali ya juu vinaweza kuleta suluhu ya gharama nafuu katika changamoto hiyo ya taka na kuisaidia miji na jamii kuziona taka kama ni fursa ya biashara.

Kaulimbiu ya mwaka  2019 ya siku ya makazi imejikita katika udhibiti wa taka lakini pia  kuhamasisha kuzitumia kama fursa ya kipato na kiuchumi. Katika ujumbe wake maalum wa siku hii Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Antonio Guterres amesema, “ni lazima tupunguze kiwango cha taka tunachozalisha na wakati huo huo tuanze kuziona taka hizo kama ni rasilimali ya thamani ambayo inaweza kutumiwa tena na tena ikiwemo katika kuzalisha nishati.” Sanjari na maazimisho ya hayo Shirika la Umoja wa Mataifa la makazi UN-HABITAT limezindua Kampeni ijulikanayo kama “Waste Wise Cities” ili kushughulikia changamoto zinazoongezeka za kushughulikia tatizo la taka. Na kama sehemu ya kampeni hiyo miji inaalikwa kuthibitisha ahadi zao za kutekeleza mikakati iliyoafikiwa na ambayo ni pamoja na kutathimini kiwango na aina ya taka, kuboresha ukusanyaji wa taka, kuhakikisha mazingira ya miji ni salama na kutekeleza miradi ya kubadili taka kuwa nishati.

Bwana Guterres amesema kampeni hiyo imebaini kwamba suala la taka linatumia bajeti kubwa ya miji na kwamba udhibiti wa taka haufadhiliwi kiasi cha kutosha. Lakini “teknolojia za kisasa zinaweza kutoa majibu ya suala hilo na kwa gharama nafuu ya jinsi ya kusafisha miji yetu.” Teknolojia hizo ni pamoja na akili bandia (AI) ambayo ikitumika kwa pamoja na teknolojia zingine inaweza kusaidia kurejesha matumizi ya vitu kwa ufanisi zaidi. Suluhisho nyingine ni kama vifungasho salama vinavyo jali mazingira, kutumia teknolojia kupunguza kiasi cha chakula kinachotupwa na teknolojia mpya bunifu ambazo zinaweza kubadili taka kuwa nishati endelevu na mbolea. UN-HABITAT imesema teknolojia pia inatoa fursa kwa miji mipya na inayokua kwa kasi katika nchi zinazoendelea kuipita miji ya zamani kwa kutumia fursa ya teknolojia ya sasa na kuepuka njia za zamani ambazo hazina ufanisi wa kutosha. Kwa kutumia vyema nyenzo zilizopo za kisasa Katibu Mkuu amesema, kunaweza kusaidia kujenga mustakabali mzuri uliopangika na unaoweza kudhibitiwa kwa miji yetu ambamo utahamasisha  ukuaji jumuishi na maendeleo yasiyo chafua mazingira. Hata hivyo Umoja wa Mataifa unasisitiza kwamba nyenzo hizo mpya ni lazima ziende sambasamba na será bora, kuzisaidia nchi kutotumbukia katika janga lingine na kupunguza gharama za kiuchumi na kijamii za masuala ya teknolojia.

Siku ya UN-Habitat duniani: Ikumbukwe kuwa Siku ya Makazi Duniani, (UN-HABITAT )iliwekwa na Umoja wa Mataifa kufanyika kila Jumatatu ya kwanza ya Mwezi Oktoba ambapo kwa mwaka 2019 imeagukia tarehe 7Oktoba. Siku hiyo iliwekwa na  Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa azimio  40/202 na kuadhishwa kwa  mara ya kwanza kunako mwaka 1986. Lengo ni kutaka kutafakari juu ya Makazi yetu katika miji, juu ya haki ya kuishi katika makazi salama na yaliyo bora. Kila mwaka Umoja wa Mataifa huchagua mada kulingana na hali halisi inayozungukia masuala ya makazi. Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa mataifa la Makazi katika tovuti yao wanaonesha mada ya  2019 inayo turudisha katika hali halisi  ya sasa kuhusu maendeleo ya kiteknolojia kama moja ya zana za ubunifu na zinazobidili taka kuwa utajiri. Ni katika uendeshaji wa ubunifu na endelevu ambao ni muhimu kwa ajili ya kufikia hata Maendeleo endelevu.

Katika kufanya miji na makazi ya watu kuwa ya pamoja, salama, ya kudumu na endelevu, taka ni mojawapo ya changamoto ambazo bado ni wazi na lengo, na  lake bado halijafanikiwa ili miji yetu iweze kuwa ya kuishi vema zaidi kwa mujibu wa taarifa. Aidha wanabainisha kwamba taka zinazotokana na shughuli za kibinadamu kama vile (ngumu, za maji, ndani ya nyumba, viwandani na kibiashara), kiukweli zinaendelea kuwa na athari mbaya juu ya mabadiliko ya tabianchi, afya ya umma na mazingira.

09 October 2019, 12:50