Tafuta

Vatican News
Huo ni msululu wa wapiga kura nchini Botswana ambapo tangu asubuhi na mapema 23 Okotba 2019  nchi nzima inafanya inafanya uchaguzi mkuu Huo ni msululu wa wapiga kura nchini Botswana ambapo tangu asubuhi na mapema 23 Okotba 2019 nchi nzima inafanya inafanya uchaguzi mkuu  (AFP or licensors)

Ni nani atakuwa mshindi wa chama tawala nchini Botswana?

Kati ya idadi ya watu milioni 2.2 wa Botswana,watu 924,000 waliosajiliwa kupiga kura watawachagua wawakilishi 57 wa bunge la taifa na 490 wa serikali za mitaa.Mgombea wa chama kitakachoshinda ndiye atakuwa rais mpya.Duma Boko,kiongozi wa chama cha UDC (Umbrella for Democratic Change),anatumaini kukiondoa chama cha BDP cha Rais Mokgweetsi Masisi.

Nchini Botswana, tarehe 23 Oktoba 2019 wapo katika  uchaguzi mkuu wa upigaji kura ambapo Chama kitakachoshinda kitahitajika kuimarisha haraka uchumi, ambao tangu uhuru wake kutoka kwa Waingereza kunako mwaka  1966 umekua kwa asilimia 8 tu kila mwaka na kuwa moja ya mataifa yenye mafanikio makubwa kabisa ya Afrika, japokuwa kwa sasa linakabiliwa na kitisho kwa sababu ya kutegemea rasilimali moja kwa muda mrefu yaani madini ya almasi.

Wagombea kuahidi kuimarisha uchumi wakati wa kampeni

Katika uchaguzi mkuu unatarajiwa kutoa ushindani wa kwanza halisi kwa chama tawala cha Botswana Democratic – BDP katika miongo yake mitano ya udhibiti wa taifa hilo. Huku akiahidi kuimarisha uchumi wakati wa kampeni zake, Duma Boko, kiongozi wa chama cha Umbrella for Democratic Change, anatumaini kukiondoa chama cha BDP cha Rais Mokgweetsi Masisi. Hata hivyo anaungwa mkono na rais wa zamani Ian Khama, ambaye alimkabidhi madaraka Masisi mwaka 2018, lakini sasa amejikuta katika mvutano mkali wa madaraka na rais huyo.

Rais wa zamani Ian Khama anaunga mkono chama cha upinzani

Kati ya idadi ya watu milioni 2.2 wa Botswana, watu 924,000 waliosajiliwa kupiga kura watawachagua wawakilishi 57 wa bunge la taifa na 490 wa serikali za mitaa. Mgombea wa chama kitakachoshinda kisha atakuwa rais mpya. Masisi anajinadi kutokana na rekodi yake ya kupambana na rushwa, kama vile kufanya iwe lazima kwa maafisa wote wa sekta ya umma kutangaza mali zao na kupunguza urasimu kwa biashara ndogondogo. Khama, mtoto wa rais mwanzilishi wa taifa hilo Seretse Khama, aligombana na Masisi kuhusu nyadhifa za uwaziri na hatua tata ya rais mpya ya kufuta marufuku ya uwindaji wa tembo mwezi Mei, ambayo Khama alikuwa ameitangaza miaka minne iliyotangulia. Ndovu hata hivyo hawajawa suala kuu katika kampeni hizi.

Wasiwasi wa Botswana katika ukosefu wa ajira

Wasiwasi mkuu kwa Wabotswana wanasema ni kiwango cha ukosefu wa ajira kuzungukia karibu na asilimia 20 na ukosefu mkubwa wa usawa licha ya hali ya ugavi sawa katika matumizi ya afya na elimu. Ili kupambana na hayo mshindi atahitaji kuchukua hatua zaidi za kuutanua uchumi ili kukidhi haja hizo nchini humo. Na kuhusu uchimbaji wa Almasi wanasema umeshuka kwa moja juu ya tano  la Pato lake kwa ujumla  ndani katika mwaka wa 2018, ikilinganishwa na nusu katika miaka ya 1900, japokuwa lakini bado inaunda robo tatu ya mapato ya fedha za kigeni, hata wakati sekta za benki na utalii zikinyakua sehemu kubwa ya mazao.

23 October 2019, 12:14