Tafuta

Vatican News
2019.05.16 chiesa burkina faso 2019.05.16 chiesa burkina faso 

Burkina Faso: Mlundikano wa watu; Ukosefu wa mahitaji msingi!

Karibia watu 300,000 wamelazimika kuacha makazi yao nchini Burkina Faso na kwenda kuishi katika vituo vya mapokezi wakati huo zaidi ya watu 500,000 wamekosa mahitaji msingi ya afya kutokana na mashambulizi ya makundi yenye silaha ya kijihadi

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican 

Inasadikika kuwa karibia watu 300,000 wamelazimika kuacha makazi yao nchini Burkina Faso na kwenda kuishi katika vituo vya mapokezi na zaidi ya watu 500,000 wamekosa mahitaji msingi ya afya kutokana na mashambulizi ya makundi  mbalimbali ya kisilaha na ya kijihadi. Hatari hii imetangazwa mapema wiki hii na Umoja wa Mataifa na Shirika la Msalaba Mwekundu, ambapo wanabainisha kwamba mashambulizi haya yamesababisha mkusanyiko wa kulazimishwa kwa nguvu kwa mamia elfu ya watu kwa kwa mujibu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA, pia kwamba kwa sasa karibu watu 289,000 waliohamishwa wanaishi katika vituo vya mapokezi au vituo vya wakimbizi katika mkoa wa kati-kaskazini, mashariki, kaskazini ya Ukanda wa  Sahel  na wakati huo huo wengine wengi zaidi waliohamishwa wanakimbilia  hata katika vituo vya mijini kama vile, Djibo na Dori (ukanda wa Sahel) na Kaya (katikati mwa kaskazini).

Tangu mwanzoni mwaka idadi ya watu waliokusanyika wameongezeka mara tatu kwa mujibu wa taarifa ya OCHA. Kwa namna ya pekee, suala la kukosa chakula na kusaidia hata huduma msingi imekuwa daima vigumu iwe kwa upande wa jumuiya iliyokimbilia hao na katika jumuiya inayowakaribisha. Kwa mujibu wa Tume ta Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (Cicr) wanatoa taarifa juu ya hali halisi ngumu ya afya nchini Burkina Faso, kwa kuthibitisha kuwa watu laki tano wamekosa mambo msingi ya afya katika miaka ya mwisho kwa miezi sita na kwa sababu ya vurugu za silaha. Katika mwezi wa nane tu ni vituo 125 vya afya vilivyoshambuliwa na kati yao, vituo 60 vimefungwa na wakati huo vituo 65 ndivyo vinafanya kazi kidogo tu, kulinganisha na 10 vya  tangu mwanzo wa mwaka. Na zaidi idadi ya wahudumu wa afya, wamelazimika kuacha maeneo ya vijiji yaliyo shambuliwa na vurugu za kisilaha.

Taarifa aidha inasema kutokana na  vurugu, hata namna ya  kwenda katika vituo vya afya imekuwa changamoto ya kweli katika sehemu ya nchi, kwa mujibu, Rais  wa CICR , Bwana  Peter Maurer, hasa mara baada ya kufanya mkutano na rais wa Burkina Faso Bwana,Roch Marc Christian Kaboré, katika mjini mkuu Ouagadougou, tarehe 5 Septemba 2019. Akieleza pia wasiwasi mkubwa kwa sasa ni baa la njaa, utapiamlo na kuendelea kwa mashambulizi ya vurugu kwa njia ya silaha. Ni karibia milioni 1,2 ya watu wanaoishi katika hali isiyokuwa na usalama kwa chakula, kwa mujibu wa Cic ambapo Shirika la Msalaba mwekundu wanathibitisha juu ya hatua ya kusambaza chakula kwa miezi mitatu kwa watu 22,0000 hata kwa ajili ya afya kwa watu 21,000. Burkina Faso ni moja ya nchi maskini barani Afrika ya Magharibi ambayo inashambuliwa sana  na ambapo kwa miaka karibia 4 na nusu imechangiwa sana na makundi ya kisilaha ya kijihadi.

Hata hiyo ufadhili zaidi unahitajika kukabiliana na changamoto za mara kwa mara anchini  Ethiopia kwa mujibu  Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA. Na hii ni kutokana na kwamba Ethiopia inakabiliwa na changamoto za mara kwa mara na za sura tofauti za kibinadamu na ufadhili zaidi unahitajika kutoka kwa jamii ya kimataifa pia msaada kwa juhudi za serikali kwa ajili ya janga la watu kuondolewa makwao.  Ni katika kauli ya Mkuu wa misaada ya dharura kwenye ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA, Bwana Mark Lowcock kufuatia ziara ya Bwana Lowcock ya siku mbili nchini Ethiopia ambapo katika ziara hiyo amesema watu zaidi ya milioni nane nchini humo wanahitaji chakula, makazi, dawa na misaada mingine wa dharura.  Kadhalika amesema, ukame na mafuriko, milipuko ya magonjwa na ukatili wa kikabila katika miaka ya hivi karibuni vimelazimisha mamilioni ya watu kukimbia makwao. Bwana Lowcock ambaye aliandamana na afisa wa ujenzi wa amani wa Umoja wa Mataifa, Bwana Oscar Fernandez-Taranco, na mtaalum huru wa Umoja huo kuhusu wakimbizi wa ndani Bi Cecilia Jimenez-Damary wamekutana na familia za  waliorejea makwao hivi karibuni na watu katika maeneo yaliyoathirikia na vita ikiwemo watu wa Chitu - Kebele katika wilaya ya Yirgachefe, Gedeo, moja ya eneo linaloathiriwa na machafuko ya kikabila ambayo yamepelekea watu kuhama na wengine kupoteza maisha tangu 2018.

Mkuu wa OCHA amesema kuwa anaunga mkono azma ya serikali kutafuta suluhu ya kudumu kwa ajili ya changamoto ya wakimbizi inatambulika jinsi ilivyo ngumu na wakati watu wengi sasa wameweza kurudi makwao, wengine wanasalia katika njia panda, wakiishi karibu na nyumba zao zilizoharibiwa huku wakisikitika kuona kwamba  hawatakuwa na fursa ya kuanza upya kilimo na vitega uchumi vyao walivyopoteza walipokimbia mwaka jana. Bwana Lowcock aidha amesema kuwa wakati serikali inajaribu kukabiliana na hali hiyo, watu wengi kwenye jamii zinazowahifadhi wanaonyesha ukarimu mkubwa na mashirika ya misaada ya kibinadamu inawaunga mkono , japokuwa  msaada wa jamii ya kimatifa unahitajika! Kufikia sasa ombi la msaada wa kibinadamu kwa Ethiopia linahitaji dola bilioni 1.3 ambapo hadi sasa limefadhiliwa kwa asilimia 51 tu na fedha zaidi zinahitajika kwa jili ya misaada ya lishe, afya, makazi, uhifadhi, elimu na mahitaji mengine. Bwana Lowcock pia ameelezea wasiwasi wake kuhusu usalama wa wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu kufuatia kuuawa kwa wafanyakazi wawili kutoka mashirika yanayotambulika yasiyo ya kiserikali eneo la Gambella wiki iliyopita na kusema  wanalaani shambulio hilo la kikatili na wanajadili athari na wadau wote.

12 September 2019, 14:50