Tafuta

Vatican News
UNICEF na Shirika la Afya Duniani: Taarifa: Kuna watoto milioni 20 ambao hawajapata chanzo dhidi ya magonjwa yanayoweza kuzuilika kwa njia ya chanjo, hatari kwa maisha! UNICEF na Shirika la Afya Duniani: Taarifa: Kuna watoto milioni 20 ambao hawajapata chanzo dhidi ya magonjwa yanayoweza kuzuilika kwa njia ya chanjo, hatari kwa maisha! 

UNICEF & WHO: Kuna watoto milioni 20 ambao hawajapata chanjo! Hatari kwa maisha!

Inakadiriwa kwamba, kati ya watoto 10 duniani, mtoto mmoja alikosa chanjo ya kuokoa maisha dhidi ya magonjwa kama: Surua, Dondakoo pamoja na Pepopunda. Jumuiya ya Kimataifa imefanikiwa kutoa chanjo ya kuokoa maisha kwa asilimia 86%, lakini kiwango kinachotakiwa ni asilimia 95% kwa dunia nzima. Lengo ni kuimarisha afya za watoto kwa kutoa chanjo kwa magonjwa yanayozuilika.

Na Pauline Mkondya, - Vatican.

Shirika la Afya Duniani, WHO pamoja na Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF, yametangaza kwamba watoto milioni ishirini, walikosa chanjo za kuokoa maisha katika kipindi cha 2018. Inakadiriwa kwamba, kati ya watoto 10 duniani, mtoto mmoja alikosa chanjo ya kuokoa maisha dhidi ya magonjwa kama: Surua, Dondakoo pamoja na Pepopunda. Jumuiya ya Kimataifa imefanikiwa kutoa chanjo ya kuokoa maisha kwa asilimia 86%, lakini kiwango kinachotakiwa ni asilimia 95% kwa dunia nzima. Lengo ni kuimarisha afya za watoto kwa kutoa chanjo kwa magonjwa yanayozuilika. Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, Bwana Tedros Adhanom Ghebreyesus amesisitiza kwamba, huduma ya chanjo ni nyenzo muhimu sana ya kuzuia milipuko ya magonjwa, ili kuiweka dunia mahali salama zaidi.

Bado kiwango cha chanjo kwa watoto hakiridhishi sana kutokana na: vita, kinzani na migogoro ya kijamii, hali inayowafanya makundi makubwa ya watoto wahamiaji na wakimbizi kukosa chanjo muhimu katika maisha. Watoto wengi ambao hawajapatiwa chanjo ni kutoka katika maeneo yaliyoathirika kwa vita. Nchi hizi ni pamoja na: Afghanistan, Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, Chad, Congo DRC, Ethiopia, Haiti, Mali, Iraq, Niger, Nigeria, Pakistan, Somalia, Sudan Kusini, Siria na Yemen.. Watoto kutoka katika nchi hizi wako hatarini kukumbwa na magonjwa yanayoweza kuzuilika kwa kutumia chanjo. Mwaka 2018 idadi ya watoto walioshambuliwa kwa ugonjwa wa Surua ilikuwa ni 350, 000.

Kiwango hiki ni mara mbili ya idadi ya watoto walioshambuliwa katika kipindi cha kwa mwaka 2017. Kwa mujibu wa Henrietta Fore Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF, anasema, kuna haja kwa Jumuiya ya Kimataifa kujizatiti kikamilifu kutoa chanjo ya kinga kwa kila mtoto duniani. Umoja wa Mataifa unakiri kwamba,  Ukraine inaoongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watoto waliothirika kwa ugonjwa wa Surua Chanjo ya HPV hutolewa kwa wasichana ili kuepusha saratani ya shingo ya  mlango wa kizazi. Wazazi na walezi wanahimizwa kuhakikisha kwamba, wanawapeleka watoto wao hospitalini ili kupata chanjo zitakazosaidia kuzuia magonjwa.

Chanjo ya Watoto

 

 

16 July 2019, 11:31