Tafuta

Shambulizi kwenye Kituo cha Kuzuia Wakimbizi nchini Libya, limesababisha zaidi ya watu 44 kupoteza maisha yao1 Huu ni uhalifu wa kivita! Shambulizi kwenye Kituo cha Kuzuia Wakimbizi nchini Libya, limesababisha zaidi ya watu 44 kupoteza maisha yao1 Huu ni uhalifu wa kivita! 

Shambulizi la Kambi ya Wakimbizi Libya, watu 44 wamefariki dunia

Shambulio limesababisha watu zaidi ya 44 kufariki dunia na watu wengine zaidi ya 130 kujeruhiwa vibaya na majengo kubomolewa. Kuna wakimbizi zaidi ya 3, 500 wanaopewa hifadhi kwenye Vizuizi vya wakimbizi nchini Libya. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa amezitaka pande zinazosigana nchini Libya kuhakikisha kwamba, zinalinda na kudumisha: utu na haki msingi za binadamu.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Antonio Guterres, amesikitishwa sana na shambulio dhidi ya Kituo cha Kizuizi cha Wakimbizi kilichoko huko Tajoura nje kidogo ya mji wa Tripoli nchini Libya na kutaka uchunguzi wa kina na huru ufanyike ili kubaini waliohusika na tukio hili ambalo kwa sasa linachukuliwa kama ni sehemu ya uhalifu wa kivita! Shambulio hili limefanyika, Jumatano tarehe  3 Julai 2019 na kusababisha watu zaidi ya 44 kufariki dunia na watu wengine zaidi ya 130 kujeruhiwa vibaya na majengo kubomolewa. Kuna wakimbizi zaidi ya 3, 500 wanaopewa hifadhi kwenye Vizuizi vya wakimbizi nchini Libya. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa amezitaka pande zinazosigana nchini Libya kuhakikisha kwamba, zinalinda na kudumisha haki msingi za binadamu, kwa kuepuka mauaji ya raia pamoja na mashambulizi kwenye miundo mbinu.

Kimsingi ameita Serikali ya Umoja wa Kitaifa kuendeleza majadiliano katika ukweli na uwazi na wapinzani, ili amani na utulivu viweze kurejeshwa tena nchini Libya. Wakimbizi na wahamiaji wapewe makazi salama hadi pale maombi yao yatakapokuwa yameshughulikiwa kikamilifu. Libya imekuwa ni kitovu cha wakimbizi na wahamiaji wanaotafuta: hifadhi, usalama na maisha bora zaidi Barani Ulaya. Juhudi za kupatanisha pande zinazosigana nchini Libya zinaonekana kushindwa na matokeo yake ni watu wasiokuwa na hatia wanaendelea kushambuliwa. Hii ni vita inayokuzwa na biashara haramu ya silaha, kiasi hata cha kukiuka sheria, kanuni na taratibu za biashara hii nchini Libya kadiri ya mwongozo wa Umoja wa Mataifa.

Maafa Libya

 

04 July 2019, 15:14