Tafuta

Moshi wa tumbaku unasababisha vifo vya watu milioni 8 kila mwaka kwa maana hiyo chagua afya na si tumbaku! Moshi wa tumbaku unasababisha vifo vya watu milioni 8 kila mwaka kwa maana hiyo chagua afya na si tumbaku! 

WHO:Tarehe 31 Mei ni Siku ya Kimataifa ya kupinga matumizi ya tumbaku:Usikubali tumbaku ichukue pumzi yako!

Kaulimbiu inayoongoza Siku ya Kimataifa ya kupinga matumizi ya tumbaku mwaka 2019 ni usikubali tumbaku ichukue pumzi yako.Leo hii ni Siku ya tafakari duniani kote juu ya hathari zinazohusiana na moshi.Saratani ya mapafu kiukweli ni saratani ya nne ambayo inasababisha vifo duniani na milioni nane ya watu wanakufa kila mwaka!

Na Sr Angela Rwezaula – Vatican

Tarehe 31 Mei  ya kila mwaka ni siku ya kimataifa ya kupinga matumizi ya tumbaku ambapo katika fursa ya kilele hiki, Shirika la afya ulimwenguni, WHO  limetoa ujumbe wake kwa kuangazia madhara ya matumizi ya tumbaku katika  mapafu ya binadamu na kuelekeza zaidi kwamba  zaidi ya asilimia 40 ya vifo vinavyotokea vinatokana na utumiaji wa tumbaku na ambapo ni kuhusiana na magonjwa kama saratani, magonjwa sugu ya njia ya hewa na Kifua Kikuu. Ni kwa mantiki hiyo mwaka 2019 WHO inataka serikali na wadau ziongeze hatua za kulinda watu dhidi ya tumbaku kwa kuongozwa na kauli mbiu “Usikubali tumbaku ichukue pumzi yako”.

Naye  Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dk. Tedros Ghebreyesus akifafanua kwa kina juu ya madhara ya matumizi ya tumbaku, amesema, “kila mwaka watu wapatao milioni 8 hufariki dunia kutokana na tumbaku. Mamilioni  ya wengine wanaishi na magonjwa sugu kama vile saratani, Kifua Kikuu, pumu au magonjwa sugu ya njia ya hewa  yanayosababishwa na matumizi ya tumbaku.” Aidha Dk. Ghebreyesus amesema “mapafu yenye afya ni muhimu kwa mtu kuishi maisha yenye afya. Leo na kila siku  unaweza kulinda mapafu yako na  yale ya rafiki zako na familia yako kwa kusema kukataa kutumia tumbaku.” Hata hivyo Shirika la Afya Duniani (WHO) linasema matumizi ya tumbaku hayajaacha watoto salama kwa kuwa, “zaidi ya watoto 60,000 wenye umri wa chini ya miaka 5 hufariki dunia kutokana na kuvuta moshi watu wavutao sigara. Wale wanaoishi hadi kufikia utu uzima wako kwenye nafasi kubwa zaidi ya kupata magonjwa sugu ya njia ya hewa pindi wanapokuwa wakubwa.

Mvuto mmoja tu wa moshi wa sigara una mamia ya kemikali za sumu ambazo uharibu mapafu

Katika kufafanua zaidi  juu ya jinsi gani moshi wa sigara uharibu mamapafu WHO inasema kwamba "mvuto mmoja tu wa moshi wa sigara una mamia ya kemikali za sumu ambazo huanza kuharibu mapafu. Hi ini kwa sababu pindi moshi unapovutwa, mifumo ya kusafisha makohozi na uchafu kutoka kwenye mapafu inadhoofishwa na hivyo kuruhusu sumu iliyomo kwenye tumbaku kuingia kwenye mapafu kwa urahisi." Shirika la Afya  linasema kuwa matokeo yake, uwezo wa mapafu kufanya kazi unapungua na mvutaji anaanza kukosa pumzi na hivyo kusababisha njia za hewa kuanza kuvimba na kujenga makohozi, "na hivi ndivyo ambavyo tumbaku huanza kuharibu mapafu."

Serikali zitokomeze janga la tumbaku na kutekeleza mkataba wa kimataifa

Na kuhusu  nini cha kufanya, WHO inasisi serikali zitokomeze janga la tumbaku kwa kutekeleza kwa kina mkataba wa kimataifa wa kudhibiti matumzi ya tumbaku, FCTC na kuimarisha hatua dhidi ya matumizi ya tumbaku. Hatua hizo ni pamoja na kupunguza matumizi ya tumbaku kwa kuongeza kodi ya bidhaa hizo, kutenga maeneo ambayo kwamo mtu haruhusiwi kuvuta sigara na kusaidia wale ambao wanataka kuondokana na uvutaji wa sigara. Na kwa ngazi ya familia, WHO inasihi wazazi na viongozi wa kijamii kuchukua hatua kulinda afya za wanafamilia kwa kuwaeleza kinagaubaga madhara ya matumizi ya tumbaku na mbinu za kujiepusha na matumizi. Halikadhalika WHO inasisitiza kuwa udhibiti wa tumbaku utasaidia kufanikisha kupunguza kwa theluthi moja ifikapo mwaka 2030 idadi ya watu wanaofariki dunia kabla ya muda wao kutokana na kuvuta tumbaku na kwamba kwa hali ilivyo sasa bado dunia haiko kwenye mwelekeo wa kutimiza lengo hilo.

Gharama za Magonjwa yatokanayo na matumizi ya tumbaku ni kubwa mno

Gharama za magonjwa yatokanayo na matumizi ya tumbaku kila mwaka ni dola trilioni 1.4 kote ulimwenguni kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la afya duniani, WHO iliyotolewa tarehe 31  Mei wakati wa kuadhimisha siku ya kimataifa ya kupinga matumizi ya tumbaku. WHO imesema gharama hii ni kubwa lakini faida za kuacha uvutaji wa tumbaku kwa asilimia 20 ya watu duniani kote ambao wanatumia bidhaa hii ni kubwa zaidi, huku mapafu ya mvutaji tumbaku yakirekebika katika muda wa wiki mbili tu. Shirika hilo limeongeza kuwa safari ni ndefu katika kutokomeza matumizi ya tumbaku kwani kufikia sasa ni asilimia 20 tu ya nchi ndizo zimefikia malengo ya kupunguza matumizi ya tumbaku.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswisi Dk. Kerstin Schotte afisa wa kiufundi kitengo cha kuzuia magonjwa yasiyo ya kuambukizwa, NCDs amesema kuna hatua ambazo nchi zinaweza kuchukua ili kupunguza matumizi ya tumbaku ikiwemo “Kutokomeza aina zote za matangazo ya tumbaku na kampeni, kutoa tarifa kwa umma kuhusu hatari za kuvuta tumbaku, sote tunajua kwamba uvutaji wa tumbaku ni hatari lakini cha kushangaza utafiti wa kukabiliana na matumizi ya tumbaku unaonyesha kwamba watu wengi hawafahamu athari za tumbaku. Kuongeza bei ya bidhaa za tumbaku kutapunguza matumizi hususan miongoni mwa vijana kwani vijana hawataanza matumizi ya tumbaku iwapo hawataweza kugharamia na watumiaji wa tumbaku watapunguza matumizi ya bidhaa hizo.” Vile vile WHO imesema inategemea ushirikiano wa nchi wanachama kuweka mikakati hiyo kwa ajili ya kukabiliana na matumizi ya tumbaku.

Ongezeko la vijanawenye tabia ya kuvuta Italia,wanaume milioni 7,1, wanawake milioni 4,5

Aidha katika uchunguzi zaidi, inaonesha kuwa kuna ongezeko kubwa zaidi la vijana wenye tabia ya kuvuta na kati ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 wenye asilimia kubwa ya uvutaji. Hii ni kwa mujbu wa Ripoti kuhusu uvutaji nchini Italia, iliyo wakilishwa katika Taasisi Kuu ya Afya katika fursa hii ya Siku kupinga matumizi ya tumbaku 2019 kwa kuongozwa na kauli mbiu Tumbaku na Afya ya mapafu: Usikubali tumbaku ichukue pumzi yako”. Kwa hakika ni siku ya kutafakari kwa pamoja duniani kuhusu hatati zinazohusiana na moshi wa tumbaku. Nchini Italia haioneshi katu maana ya kupungua wavuta sigara, na hata kushuka kwa idadi ya sigara zinazotumiwa kila siku. Ni milioni 11,6 ya watu wanaopenda sigara, hiyo ikiwa na maana ya  kwamba ni mtu 1 kati ya watu 5 nchini Italia. Wanaume ni milioni 7,1 na wanawake milioni 4,5. Kufuatia na toleo hili la kuhamasisha juu ya Tumaku na afya ya mapafu, wanasema kuwa Saratani ya mapafu kwa hakika ndiyo saratani ya nne ambayo ni hata lakini zaidi inayosababisha kifo.

Kusini mwa Italia wanavuta sigara zaidi ya Mikoa ya Kati na Kaskazini

Kusini mwa Italia, wavuta sigara wanaonezaka kwa mujibu wa  ripoti na zaidi wanasema ni maradufu kulingana na wavuta sigara wanaoishi katika mikoa ya Kati na Kaskazini (ikiwa ni asilimia 22,4 Kusini na visiwani,  dhidi ya asilimia 12,% katika mikoa ya  Kati na asilimia 14% Kaskazini). Zaidi ya nusu ya vijana wavuta sigara kati ya umri wa miaka 15 na 24 wanavuta zaidi ya sigara 10 kila siku na zaidi ya  asilimia 10% ya vijana wakubwa zaidi wanavuta zaidi ya sigara 20 kwa siku. Hata hivyo ripoti inabainisha kwamba ni vijana wadogo ambao kawaida wanaanza kuvuta kidogo kidogo na wasichana zaidi ambao hawajafikisha miaka 20. Mantiki nyingine inayo jionesha katika Ripoti ni kwamba, kati ya wavuta sigara zinazotengezwa mikono, bado inaonesha mwendelezo kwa upande wa wavulana huko Kusini ambapo asilimia 90% wanapendelea kununua sigara za jadi.

Naye Mkurugenzi wa Kitaifa kuhusu madawa ya kulevya na uvutaji wa sigara  amesema, "licha ya kufanya kampeni za mafunzo, hakuna mabadiliko yoyote katika miaka ya mwisho kuhusu uvutaji wa sigara kwa waitaliani. Hii ni ishara ya kuonesha  kwamba kunahitaji  hatua ya zaidi za kufanya  kampeni za mafunzo hasa kwa upande wa vijana ambao ndiyo walengwa muhimu kwa ajili ya ufahamu wa janga la tumbaku  na zaidi  wanawake ambao vifo vya saratani ya mapafu vinazidi kuongezeka". Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo amesisitiza kuwa , "ni muhimu kuingilia kati kwa haraka iwezekanavyo kwa maana kama inavyoonesha kadi yao juu ya hatari ya mapafu ni kwamba kadiri mtu anavyovuta mapema sigara lakini ni  hatari pia kuugua kwa wale ambao hawajawahi kuvuta.

 

31 May 2019, 16:28