Tafuta

Vatican News
Rais Sergio Mattarella wa Italia amemtumia Papa Francisko salam na matashi mema wakati wa hija yake nchini Morocco, 2019 Rais Sergio Mattarella wa Italia amemtumia Papa Francisko salam na matashi mema wakati wa hija yake nchini Morocco, 2019 

Hija ya Papa Francisko Morocco 2019: Salam na matashi mema!

Ni matumaini ya Rais Mattarella wa Italia kwamba, Baba Mtakatifu katika hija yake ya kitume nchini Morocco, ataweza kuwapatia ujumbe wa matumaini wale wote watakaobahatika kumsikiliza. Ni ujumbe unaotia hamasa kwa familia ya Mungu nchini Morocco kujenga na kudumisha majadiliano, kusikiliza na kuthaminiana.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Rais Sergio Mattarella wa Italia amemwandikia Baba Mtakatifu Francisko ujumbe wa shukrani na matashi mema wakati wa hija yake ya kitume nchini Morocco kuanzia tarehe 30-31 Machi 2019. Ni matumaini ya Rais Mattarella kwamba, Baba Mtakatifu ataweza kuwapatia ujumbe wa matumaini wale wote watakaobahatika kumsikiliza. Ni ujumbe unaotia hamasa kwa familia ya Mungu nchini Morocco kujenga na kudumisha majadiliano, kusikiliza na kuthaminiana.

Wakati huo huo, Baba Mtakatifu katika salam na matashi mema kwa familia ya Mungu nchini Italia, akiwa njiani kuelekea nchini Morocco kwa hija ya kitume, amemwambia Rais Sergio Mattarella kwamba, anakwenda nchini Morocco ili kukutana na Jumuiya ya Waamini wa Kanisa Katoliki, ili kusali na kujenga umoja; sanjari na kuwatia shime kuendeleza majadiliano ya kidini nchini Morocco. Baba Mtakatifu amewahakikishia sala zake, ili Italia iweze kutoa kipaumbele cha kwanza kwa tunu msingi za maisha kiroho na kiutu; kwa kujikita katika utulivu na maridhiano, daima mshikamano wa kidugu ukiwa ni njia ya kukabiliana na changamoto zinazojitokeza.

30 March 2019, 11:42