Cerca

Vatican News
Baraza la Maaskofu nchini Mexico,Marekani pia baadhi ya majimbo nchini Marekani wanapinga uamuzi wa Bwana Trump wa ujenzi wa ukuta mpakani mwa Mexico Baraza la Maaskofu nchini Mexico,Marekani pia baadhi ya majimbo nchini Marekani wanapinga uamuzi wa Bwana Trump wa ujenzi wa ukuta mpakani mwa Mexico 

Mexico:Maaskofu wanapinga uamuzi wa Trump juu ya ujenzi wa ukuta

Maaskofu wanaungana na ndugu zao wa Marekani kupinga uamuzi wa Trump kuhusu fedha za ujenzi wa ukuta mrefu katika mpaka na Mexico wakati huo hata majimobo 16 ya Marekani wanafungua mashtaka dhidi ya uamuzi wa ujenzi wa ukuta huo

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Maaskofu katoliki nchini Mexico wametoa tangazo tarehe 15 Februari 2019  wakiunga mkono Baraza la Maaskofu katoliki nchini Marekani ya kuwa wako mbali kabisa na  maamuzi ya Rais Donald Trump ya kutaka kuendelea na ujenzi wa ukuta mpakani mwa Mexico.

Inahitaji kujenga madaraja na siyo kuta

Taarifa za Baraza la Maaskofu nchini Mexico (CEM) waliyoitoa mara baada ya Mkutano wao wa kitaifa kuhusu nyumba za kukaribisha wageni, uliofanyika katika mji wa Mexico tarehe 15 na 16 Februari, wananarudia kwa upya maelezo ya maaskofu wa Marekani kwamba: “sisi tuna dukuduku ya kina  kutokana na matendo ya Rais yanayo lenga fedha za kujenga ukuta mrefu kati ya mpaka wa Marekani na Mexico, tendo ambalo linakwenda kinyume na nia zilizo wazi za Kongresi ya Marekani ya kuzuia uwekezaji wa fedha katika ujenzi wa ukuta. Sisi tunapinga matumizi ya fedha hizo katika kuhamasisha ujenzi wa ukuta huo. Ukuta ambao hawali ya yote ni ishara ya mgawanyiko na vizingiti kati ya nchi mbili rafiki. Sisi tunahaidi kubaki na maamuzi na maono yaliyoelekezwa na Baba Mtakatifu Francisko kwamba: katika kipindi hiki tunahitaji kujenga madaraja na siyo kuta”.

Saini za Ujumbe wa Baraza la Maaskofu wa Mexico

Ujumbe wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Mexico (Cem) umetiwa saini na Rais wa Baraza la Maaskofu, Askofu Mkuu Rogelio Cabrera López, wa Jimbo Kuu Katoliki la  Monterrey, Katibu Mkuu, Askofu  Alfredo Gerardo Miranda Guardiola, msaidizi wa Jimbo Kuu Monterrey na Mkuu wa kitengo cha maendeleo ya binadamu wa Baraza la Maaskofu nchini Mexico, Askofu José Guadalupe Torres Campos, wa jimbo katoliki la  Ciudad Juárez. Wakati huo huo wa mkutano kuhusu nyumba za makaribisho kwa ajili ya wahamiaji (zipo 120 katika nchi yote, majengo yanayoendeshwa na Kanisa Katoliki nchini Mexico) umehitimishwa na ujumbe wa mwisho ambao unathibitisha juu ya jitihada za kuendelea katika nchi zilizoekekeza na  Baba Mtakatifru Francisko  katika mambo makuu manne: kukaribisha, kulinda, kuhamsisha na kushikirikisha. Kati ya malengo ya dhati yaliyoelekezwa wakati wa mkutano wao ni mahitaji ya ushirikiano kati ya majimbo yote  na majengo ya kukaribisha, kuanzishwa kwa mchakato wa mafuzo na uhamasishwaji, shughuli ya kutazama namna ya kuzuia matukio katika mantiki ya biashara ya binadamu.

Yapo majimbo 16 ya Marekani yaliyofungua mashtaka kutokana na uamuzi wa ujenzi wa ukuta

Hata hivyo habari kutoka Marekani zinasema kuwa jimbo la California nchini Marekani pamoja na majimbo mengine 15 yamefungua mashtaka tarehe 18 Februari 2019 dhidi ya uamuzi wa rais wa nchi hiyo Donald Trump wa kujenga ukuta katika mpaka unaozitenganisha nchi ya Marekani na Mexico. Mwanasheria Mkuu wa California Xavier Becerra ametoa taarifa rasmi hapo jana inayosema mashtaka hayo yanapinga hatua ya utawala wa Trump ambayo inakiuka sheria ya nchi hiyo. Becerra ameongeza kwamba Rais Trump anautumia utawala wa sheria kwa kudharau kabisa, anajua hakuna mgogoro wa mpaka, anajua tamko la hali ya dharura ya taifa halikubaliki na anakiri kwamba huenda akashindwa katika kesi hii ikifika mahakamani. Wiki iliyopita akizungumzia ujenzi wa ukuta huo, Bwana Trump alisema kwamba chama cha Democratic kinampinga kwa sababu kinafikiri kufanya hivyo kutakisaidia kushinda uchaguzi ujao. Bwana Trump,amesema."Ninaweza kuujenga ukuta kwa kipindi cha muda mrefu. Sijakuwa na lazima ya kuchukua hatua hii ya haraka. Lakini ningependa kuujenga haraka. Na sina haja ya kufanya hivyo kwa ajili ya uchaguzi. Nishafanya vya kutosha kwa ajili ya uchaguzi wa 2020. Na sababu pekee tunalijadili suala hili ni uchaguzi. Wanatafuta ushindi wa uchaguzi, ambao inaonekana kama watashindwa. Na hii ni moja wapo ya njia wanayodhani inaweza kuwasaidia kushinda, kwa kuleta vipingamizi na mengi yasiyokuwa na maana.

Wanaounga mkono California

Wanaounga mkono jimbo la California ni wanasheria wakuu kutoka majimbo ya; Colorado, Connecticut, Delaware, Hawaii, Illinois, Maine, Maryland, Michigan, Minnesota, Nevada, New Jersey, New Mexico, New York, Oregon, na Virginia. Majimbo yote yanayohusika na kesi hiyo yana wanasheria wakuu wanaotoka chama cha Democratic. Trump alitangaza hali ya dharura ya kitaifa ili kutimiza ahadi yake ya kujenga ukuta wa Mexico. Hatua hiyo itamruhusu rais kulikwepa bunge kutumia fedha kutoka Wizara ya Ulinzi ya Marekani Pentagon na bajeti nyingine. Majimbo hayo yanasema utumiaji wa fedha za jeshi kujenga ukuta utaumiza uchumi na kuzinyima kambi za kijeshi kufanyiwa ukarabati unaohitajika. Majimbo hayo pia yanasema kuchukua fedha zilizotengwa kwa ajili ya juhudi za kupambana na madawa ya kulevya pia kutaleta matatizo. Majimbo ya California na New Mexico, yamesema ukuta anaotaka kuujenga Bwana Trump utawaathiri hata wanyama pori katika eneo hilo la mpakani.

19 February 2019, 15:07