Tafuta

Vatican News
Tarehe 10 Desemba ni kumbukumbu ya kupitishwa azimio la haki za binadamu duniani Tarehe 10 Desemba ni kumbukumbu ya kupitishwa azimio la haki za binadamu duniani 

Siku ya haki za binadamu Kimataifa:bado kufikia malengo yaliyokubaliwa!

Tarehe 10 Desemba 1948 ilitangazwa Azimio na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa juu Tamko la Haki za Binadamu na tangu mwaka 1950 kuanza rasmi kufanyika Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu. Tamko hili lina Ibara 30, ambapo ibara ya kwanza ni “Watu wote wamezaliwa huru hadhi na haki zao ni sawa wote wana akili na wana dhamiri

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Leo ni siku ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa ikiwa ni tarehe ya kukumbuka ya  kupitishwa kwa azimio la haki za binadamu duniani. Shirika la Haki za Binadamu (LHRC) la Umoja wa Mataifa kwa maana hiyo linatimiza miaka 70. Azimio hilo lilipitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, kunako  tarehe 10 mwezi Desemba mwaka 1948 huko Paris mji mkuu wa Ufaransa. Kutokana na hili lilipatiwa jina la tamko la haki za binadamuna na wakati huo huo  hati hiyo ikaweka viwango vya pamoja vya haki za binadamu kwa wote na mataifa yote. Azimio hilo, kwa mara ya kwanza liliweka misingi ya haki za binadamu inayokubalika kimataifa na inayopaswa kulindwa popote pale duniani. Hadi sasa Azimio hilo limetafsiriwa zaidi ya lugha 500 ikiwemo hata Kiswahili. Maadhimisho haya yanaambatana na shughuli mbalimbali kuanzia kuhusiana  na haki msingi kwa maana hiyo kunzia Suva barani Asia, hadi Johannesburg Afrika, Mexico hadi Los Angeles Marekani, kwa lengo la kuendeleza, kushirikisha na kutathmini Azimio hilo na umuhimu wake katika maisha ya kila siku!

Tarehe 10 Desemba 1948 ilitangazwa Azimio na Mkutano Mkuu wa Umoja

Tarehe 10 Desemba 1948 ilitangazwa Azimio na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa juu Tamko la dunia la Haki za Binadamu na kunako mwaka 1950 kuanza rasmi kufanya Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu. Katika siku hii huko Oslo wanatunuku Tuzo ya Nobel ya Amani na wakati huko mjini New York  nchni Marekani, kila baada ya miaka mitano wanatoa Tuzo ya Haki za Binadamu ya Umoja ya Mataifa. Kiini cha Siku hiyo ni kuelimisha na kuhamasisha watu kulingana na binadamu alivyo na kukumbusha hatua zilizopigwa na jamii katika kutekeleza sula la heshima ya binadamu wote, dhidi ya utumwa na kukandamizwa kwa  haki binafsi. Hiyo haijalishi wewe ni mwanaume, mwanamke, au mtoto, iwe ni kuzungumza lugha yoyote kama vile kiswahili, Kichina au kijerumani; haijalishi una rangi ya ngozi njano, nyeupe kama theruji au nyeusi, kila mmoja anayo haki ya kuwa binadamu aliyezaliwa huru na sawa, mwenye hadhi na haki sawa. Tamko hili lina Ibara 30, ambapo ibara  ya kwanza ya tamko hilo inaanza na kusema: “Watu wote wamezaliwa huru hadhi na haki zao ni sawa  wote wana akili  na wana dhamiri hivyo yapaswa watendeane kindugu. Kadhalika zipo ibara zinazohusu raia, siasa, uchumi, kijamii na utamaduni ambapo inazuia kabisa kutesa na hali isiyostahili katika magereza, haki sawa na mchakato sawa, bila kushutumu hadi kufikira ibara inayohusu  haki ya uzalendo na uhuru wa kuzunguka kwa binadamu mahali popote ali mradi havunji sheria. 

Shughuli za leo ni kilele cha harakati zilizoanza mwezi desemba mwaka jana

Kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani kumekuwapo mjadala kuhusu umuhimu wa tamko hilo, halali la “tuzo kwa washindi wa tuzo ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa kwa mwaka huu wa 2018 lakini ambayo itatolewa tarehe 18 mwezi huu.  Hayo yametoka katika  ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa. Huko Geneva, Uswisi kwenye ofisi ya Umoja wa Mataifa ambako kunafanyika shindano la "Haki zangu ndani ya sekunde 180" , watoto walitakiwa kutuma video ya sekunde 180, ikifafanua haki zao. Mbinu mbalimbali zimetumika kufafanua yaliyomo kwenye tamko hilo ikiwemo uchambuzi wa ibara kwa ibara, sambamba na video inayoonyesha baadhi ya watu akiwemo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Antonio Guterres, na wametaja haki zilizomo kwenye tamko hilo kwa lugha nane, ambazo ni kiswahili, kireno, kiarabu, kispanyola, kichina, kirusi, kifaransa na kiingereza.

Tamko hili lilipitishwa baada ya vita Kuu ya Pili ya Dunia limekuwa mwongozo wa kusimamia haki na ulinzi wa kijamii,

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu Bi Michelle Bachelet kupitia ujumbe wake wa siku hii amesema amesema, “tamko hili lililopitishwa baada ya vita vikuu vya pili vya dunia limekuwa mwongozo wa kusimamia haki na ulinzi wa kijamii, kupatia watu fursa za kiuchumi na ushiriki kwenye siasa.” Kadhalika ameongeza kusema kuwa popote pale ambapo azimio hilo lenye ibara 30 limeheshimiwa, utu wa mamilioni ya watu umeinuliwa na machungu yaliyoonea na kwa hiyo “katika zama za sasa za misukosuko, tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa ni mbinu sahihi ya kutuongoza.”

Naye mshindi wa tuzo ya haki za binadamu 2018, Rebeca Gyumi anasema changamoto za maisha zilinisukuma kuwa mchechemuzi, hiyo ni mshindi wa tuzo ya mwaka huu haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa Rebeca Gyumi kutoka Tanzania ambaye atakabidhiwa tuzo hiyo na  amezungumzia kile kilichomsukuma kuwa mchechemuzi wa  haki hususan za watoto wa kike kwenye taifa lake hilo la Afrika Mashariki.Rebeca Gyumi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya ‘Msichana Initiative’ nchini Tanzania kwa miaka 8 amekuwa akihoji uhalali wa ibara ya 13 na 17 ya sheria ya ndoa ya mwaka 1971 nchini humo ambayo inahurusu mtoto wa kike kuolewa akiwa na umri wa miaka 14 na 15 kwa ridhaa ya wazazi au mahakama.

Kutokomeza ndoa za utotoni 

Akihojiwa na mwandishi wa habari wa umoja wa Mataifa nchini Tazania, Rebeca ameeleza kile kilichomvutia kutetea haki za binadamu hususani katika kutokomeza ndoa za utotoni. Bi Rebeca anasema: “nafikiri kilichonisukuma ilikuwa ni changamoto ambazo niliziona wakati nikifanya kazi kama mtetezi wa vijana katika shirika linalowalenga vijana la FEMINA lakini ninaweza kusema hata katika makuzi yangu vilevile, niliona changamoto mbalimbali ambazo kimsingi zilikuwa zinawakwamisha wasichana wengi kupata elimu.” Na baada ya kugundua tena  kuwa changamoto alizokuwa anaziona katika eneo lake, zilikuwa pia katika maeneo  mengine mengi  nchini Tanzania anasema: “nafikiri kama msichana mara zote huwa ninajiuliza ni nini zaidi ninachoweza kufanya na namna gani naweza kuwa sauti katika mahali pengine na  siyo kumaliza kabisa, lakini angalau kuionesha jamii yangu ielewe kuwa ndoa za utotoni si jambo zuri na uwekezaji mzuri kwa mtoto wa kike ni kuwekeza katika elimu yake.”

Kuhusiana na ushindi wa tuzo ya 2018 ya haki za binadamu

Bi Rebeca Gyumi anasema ingawa alikuwa anaona matatizo mengi yanayo wakumba vijana, lakini matatizo dhidi ya wasichana yalikuwa ni mengi zaidi na hasa hilo la ndoa za utotoni lilikuwa linamuumiza zaidi kwani alishiriki mikutano mingi ya kujadili namna ya kuhakikisha umri wa chini wa ndoa unakuwa miaka 18, lakini baada ya hapo hakuna hatua kubwa iliyokuwa inachukuliwa na hivyo: “ nilijiuliza ni nini ninachoweza kufanya kama mwanasheria na kama kijana mdogo ambaye ninahisi sauti yangu ni kitu ninachoweza kuweka katika harakati hii ili kuongeza kasi ya mchakato wa kuongeza umri wa ndoa. Na hapo ndipo hata lalamiko lilipokuja ili kushinikiza umri wa kuolewa ufike miaka 18. Mwezi Oktoba mwaka huu wa 2018, Rebeca Gyumi alitangazwa mshindi wa tuzo ya mwaka huu ya haki za binadamu ambakohii inatanguliwa na tuzo nyingine ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF kwa mchango wake wa kukomesha ndoa za utotoni nchini Tanzania aliyoipata mwezi septemba mwaka 2016.

Hata hivyo malengo yaliyokusudiwa ya haki za binadamu bado kutimia

Wataalamu huru wa haki za binadamu  wa Umoja wa Mataifa hivi karibuni wamesisitiza haja ya kuamsha tena ari ya utekelezaji wa tamko la haki za binadamu lililozinduliwa yapata miaka 70 iliyopita. Katika taarifa ya kuelekea maadhimisho ya miaka 70 ya tamko hilo iliyotolewa na wataalamu hao wanaoteuliwa na Baraza la Haki za Binadamu walisema ingawa kuna mafanikio mengi duniani tangu kupitishwa kwa tamko hilo ikiwemo kushuhudia maendeleo ya kukua kwa viwango vya haki za binadamu katika nchi mbalimbali duniani lakini bado kuna changamoto nyingi katika utekelezaji wa tamko hilo kwani wamesema “Leo hii tunashuhudia vita, machafuko na ukiukwaji wa utu wa binadamu kila siku katika sehemu mbalimbali duniani, baadjhi ya nchi na viongozi wa kisiasa wakijihusisha na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.”

Mambo mengi yanayodhihirisha mmomonyoko kwa utekelezaji wa tamko la haki za binadamu

Taarifa yao imeongeza kuwa mifano ya karibuni ni mauaji ya kimbari, uhalifu wavita unaoendelea k atika migogoro mbalimbali ,uhalifu dhidi ya ubinadamu na ukwepaji wa sheria ukishamiri katika nchi nyingi zilizoghubikwa na vita vinavyoendelea au machafuko ya kisiasa ukichangiwa na malengo ya kitaifa, siasa na changamoto za kisiasa kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Msataifa. Wataalamu hao wamesema kuna mambo mengi yanayodhihirisha mmomonyoko kwa utekelezaji wa tamko la haki za binadamu mbali ya vita kama vile changamoto kubwa hivi sasa ya uhamiaji iliyosababishwa navita, masuala ya kiuchumi, umasikini, utawala wa kiimla, chuki dhidi ya wageni, sera za utaifa na mengineyo hali inayosababisha kutia dosari mafanikio yaliyopatikana kutokana na ushirikiano wa kibinadamu wa kimataifa kwa miaka takriban 70 iliyopita. Wamesema nchi nyingi haziwatendei watu wote sawa kwa missing ya utu na usawa ulioainisha kwenye ibara za tamko hilo, hivyo wamekumbusha kwamba tamko hilo lilipitishwa baada ya migogoro kwa lengo la kumaliza na kudumisha amanihivyo ni muhimu kukumbuka mnepo wa ujumbe huona kuwa na haja ya kila mtu kutimiza ahai upya ya tamko hilo kwa miaka mingine 70.

10 December 2018, 12:22