Tafuta

Vatican News
Marekani imefungua tena ubalozi wake nchini Somalia baada ya kuvunja uhusiano wa kidiplomasia kwa muda wa miaka 28. Marekani imefungua tena ubalozi wake nchini Somalia baada ya kuvunja uhusiano wa kidiplomasia kwa muda wa miaka 28. 

Marekani yafungua tena ubalozi wake nchini Somalia!

Donald Yamamoto nguri wa diplomasia ya Marekani na mtu ambaye anaifahamu vyema Somalia, ndiye aliyepewa dhamana na Rais Donald Trump wa Marekani kuwa Balozi wa Marekani nchini Somalia. Itakumbukwa kwamba, Marekani ilivunja uhusiano wa kidiplomasia na Somalia kunako mwaka 1991 kutokana na kufumuka kwa vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Serikali ya Marekani baada ya kuvunja uhusiano wa kidiplomasia na Somalia kwa muda wa miaka ishirini na nane, imeamua tena kurejesha uhusiano huo na Somalia, ili kuimarisha juhudi ambazo zimeoneshwa na pande hizi mbili tangu mwaka 2013. Ufafanuzi huu umetolewa na Heather Nacurt, Msemaji wa Serikali ya Marekani. Kwa muda wa miaka ishirini na nane, shughuli zote za kidiplomasia kati ya Marekani na Somalia zilikuwa zikifanyika mjini Nairobi, nchini Kenya.

Donald Yamamoto nguri wa diplomasia ya Marekani na mtu ambaye anaifahamu vyema Somalia, ndiye aliyepewa dhamana na Rais Donald Trump wa Marekani kuwa Balozi wa Marekani nchini Somalia. Itakumbukwa kwamba, Marekani ilivunja uhusiano wa kidiplomasia na Somalia kunako mwaka 1991 kutokana na kufumuka kwa vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini humo. Wachunguzi wa masuala ya kivita wanasema, Marekani haitasahau kipigo kutoka Somalia, kilichotokea mwaka 1993, pale Elikopta zake mbili zilizokuwa zimebeba wanajeshi wa kikosi maalum zilipotunguliwa na kusababisha vifo vya wanajeshi kumi na nane!

USA: Somalia: Diplomasia
06 December 2018, 13:41