Tafuta

Vatican News
Tume ya uchaguzi Ceni) ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo imepeleka mbele uchaguzi kwa baadhi ya kanda kutokana na migogoro ya silaha na mlipuko wa Ebola Tume ya uchaguzi Ceni) ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo imepeleka mbele uchaguzi kwa baadhi ya kanda kutokana na migogoro ya silaha na mlipuko wa Ebola  (AFP or licensors)

Congo DRC:Wasiwasi wa Kanisa kuhusu uamuzi wa Tume ya uchaguzi

Maaskofu Katoliki wa Congo wana wasiwasi juu ya uamuzi wa Tume ya uchaguzi wa kitaifa ambayo inapaleka mbele zaidi kupiga kura kwa baadhi ya maeneo ambayo ni ngome ya upinzani kutokana na migogoro ya silaha na janga la Ebola lililoshambulia kanda hiyo

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ( Cenco) Padre Donatien N’shole, wakati wa mazungumzo na vyombo vya habari amethibitisha wasiwasi wake juu ya uamuzi uliotangazwa na Tume ya uchaguzi (CENI) nchini humo unaotarajiwa kufanya Jumapili tarehe 30 Desemba na kwa badhi ya maeneo hadi machi 2019 katika majimbo ya Beni Yumbi na mji wa Betembo, maeneo ambayo anasema ni ngome ya upinzani.

Maswali  kwa upande wa Kanisa  la Congo DRC

Kufuatia na uthibitisho wa Tume hiyo, Katibu  Mkuu wa Baraza la Maaskofu Congo DRC anauliza  maswali kwanini hawakuzuia katika mkoa wa kampeni ya uchaguzi mahali ambapo watu hawakuwa tayari? Licha ya hayo kwanini hawakuzuia kwenda Kanisani  mahali ambapo watu wengi wanakusanyika? Ni kwa sasa wanazuia wakati wa kupiga kura? Je kuna sehemu ambamo wameficha ajenda? Ndiyo maswali ya Padre N’shole.

Sababu za Tume ya uchaguzi kuahirisha uchaguzi katika baadhi ya maeneo

Tume ya uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo imetangaza kuwa imeahirisha uchaguzi wa Disemba 30 kwenye maeneo kadhaa nchini humo hadi  mwezi Machi mwakani kutokana na mlipuko wa Ebola na mapigano. Tume hiyo inaandika: Huko Yumbi, mashariki ya nchini zaidi ya watu 50 wameuwawa katikati ya mwezi Desemba katika  jumuiya za  Banunu na Batende. Tume ya uchaguzi inathibitisha kuwa, ajali hizi zimepelekea wimbi la watu kuhama, uharibifu wa vifaa na nyaraka za uchaguzi na kuibiwa kwa vitu mbalimba katika jengo la tume.  Na zaidi hata ongezeko la mlipuko wa Ebola unaoshambulia kwenye miji iliyo hatarini la eneo la Ben na mji wa Butemba umesababisha vifo vya watu tayari 350. Kwa mujibu wa Ceni aiyo rahisi kuvumilia mivutano katika hali hii ya uchaguzi, haiwezekani kuendesha uchaguzi wa amani kama ulivyokuwa unatazamiwa.

Hata hivyo taarifa kutoka Tume ya Uchaguzi  CENI

Tume ya uchaguzi CENI imetangaza tarehe 26 Desemba 2018 kuwa uchaguzi umesogezwa mbele kwenye miji ya mashariki ya Beni na Butembo na mji wa magharibi wa Yumbi lakini uamuzi huo hautaathiri uchaguzi wa rais uliopangwa Jumapili ijayo. Upigaji kura katika uchaguzi unaopangwa kufanyika tarehe 30 Desemba tayari umeharishwa kwa wiki moja baada ya tume kusema moto uliozuka kwenye ghala la kuhifadhi vifaa vya uchaguzi mjini Kinshasa na kuleta matatizo ya kuendelea na zoezi. Kulingana na tume hiyo ucheleweshaji huo wa uchaguzi kwenye maeneo hayo hautaathiri ratiba ya uchaguzi wa  rais ambao unafanyika kwa pamoja na uchaguzi wa bunge na majimbo. Kwa mujibu wa CENI Matokeo ya uchaguzi wa rais yatatangazwa Januari 15 na rais mteule ataapishwa Januari 18 mwaka 2019. Hata hivyo tume hiyo haikutoa maelezo yoyote juu ya ni vipi matokeo ya kura ya urais yatajumuishwa na yale ya majimbo ambayo hayatapiga kura Jumapili ijayo ambayo uchaguzi umepangwa miezi miwili yaani mwezi machi.

Viongozi wa Afrika waelezea wasiwasi kuhusu machafuko DR Congo

Marais watano wa mataifa ya Afrika wameelezea wasiwasi wao mkubwa kuhusu vitendo vya machafuko wakati wa kampeni za uchaguzi wa rais katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambako upigaji kura umeahirishwa katika majimbo mawili yenye ghasia. Mataifa manane ya kusini na Afrika ya Kati yalifanya mkutano mdogo mapema wiki,mjini Brazzaville katika nchi jirani ya Jamhuri ya Congo na kuijadili hali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, nchi ambayo imekuwa uwanja wa kikanda wa mapambano. Mwakilishi wa Congo hakuhudhuria, lakini viongozi wa mkutano huo waliamua kuwa ujumbe wa mawaziri wa kigeni utawasilisha wa mapendekezo yao kwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila. Nchi zilizohudhuria mkutano huo ni Angola, Botswana, Congo, Namibia, Rwanda, Afrika Kusini, Uganda na Zambia. Nchi tano ziliwakilishwa na marais wake, wakati nyingine ziliwatuma mawaziri wa mambo ya kigeni au maafisa wa ngazi za chini. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo itaandaa uchaguzi wake Desemba 30.

Wakazi wa Kivu Kusini washerehekea Noeli kwa hofu

Wakazi wa mji wa Bukavu ulioko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wanazidi kuhofia hali ya kisiasa ya sasa kuhusu uchaguzi ulioahirishwa mara kadhaa na unaopangwa kufanyika siku za hivi karibuni zijazo. Watu wanajiuliza iwapo tume ya uchaguzi CENI iko tayari kwa uchaguzi huo wa Jumapili tarehe 30 Desemba, pia wanatafakari je ikiwa hautafanyika ni kipi kitatokea? Wagombea wa Bukavu wanasema wameshangazwa na tangazo lililotolewa na meya wa mji huo akiwataka walipe kiasi fulani cha pesa kwa kuwa wamebandika picha na mabango ya kampeni kwenye maeneo ya umma mjini Bukavu. Pesa hizo zitachangia kwa usafi wa mji, amesema meya wa Bukavu Meschac Bilubi. Ameongeza kusema fedha hizo zinapaswa kulipwa hadi ifikapo Januari 15, mwaka ujao wa 2019 na kwamba atatangaza kwenye vyombo vya habari na kubandika kwenye ofisi yake majina ya wale waliolipa na wale ambao hawatafanya hivyo. Hatua hii ya meya wa Bukavu imepuuzwa na wanaharakati wa asasi za kiraia pamoja na wagombea, wakisema kwamba hakuna sheria yoyote inayowalazimu walipe malipo hayo wakati wa kampeni.

27 December 2018, 14:35