Tafuta

Vatican News
Ni muhimu kushiriki katika shughuli zote za kibinadamu, kama vile kuwa afisa polisi, kwani hakuna utofauti wa kuishi kati ya wanaume na wanawake katika dunia ya kijeshi Ni muhimu kushiriki katika shughuli zote za kibinadamu, kama vile kuwa afisa polisi, kwani hakuna utofauti wa kuishi kati ya wanaume na wanawake katika dunia ya kijeshi  

UNPOL:je wajua kwamba Maafisa wa Polisi wanawake wanahitajika katika ulinzi wa amani?

Hivi karibuni Maafisa wa polisi wa Umoja wa Mataifa (UNPOL) hivi karibuni walikusanyika kujadili jukumu muhimu la wanawake maafisa wa polisi katika operesheni za Umoja wa Mataifa kote duniani na jinsi gani ya kuongeza idadi yao kwenye operesheni hizo

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Je wajua kwamba Maafisa wa Polisi wanawake wanahitajika kwenye ulinzi wa amani kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa? Ni muhimu kushiriki katika shughuli zote za kibinadamu, hata zile ngumu, hakuna utofauti wa kuishi katika wanaume na wanawake katika dunia ya kijeshi kulingana na jamii ya raia; kuishi katika ya wanaume na wanawake, haijawahi kuwa matatizo, badala yake imeonesha kuwa ni rahisi ndani ya nguvu za kijeshi. Katika hilo, kuna karibu maafisa wa polisi 11,000 wa Umoja wa Mataifa kutoka nchi 88 wanaohudumu kwenye operesheni za ulinzi wa amani. Asilimia 21 waliotumwa na nchi wachangiaji wa vikosi ni wanawake.

Katika makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York, Maafisa wa polisi wa Umoja wa Mataifa (UNPOL) hivi karibuni walikusanyika kujadili jukumu muhimu la wanawake maafisa wa polisi katika operesheni za Umoja wa Mataifa kote duniani na jinsi gani ya kuongeza idadi yao kwenye operesheni hizo.  Hata hivyo Wanawake maafisa wa polisi wa Umoja wa Mataifa wanaweza kuwa kiungo muhimu baina ya mpango wa ulinzi wa amani na wenyeji, hususan wanawake ambao kwa sababu ya mila na desturi itakuwa vigumu kushirikiana kwa karibu na wanaume kama ilivyo Darfur ambako mpango wa pamoja wa Muungano wa Afrika na Umoja wa Mataifa.  Jimboni Darfur nchini Sudan, maafisa wa polisi wanawake kutoka Yordan wanajihusisha na shughuli za kuelimisha jamii. Na hata wakati wa kufanya sherehe mbalimbali angalau kuwakaribia kwa mfano hata hivi karibuni wakati wa  siku ya wanawake duniani maafisa hao waliungana nao.

Nchini Sudan Kusini, maafisa wa polisi wanawake wanaohudumu katika mpango wa UNMISS mara kwa mara wanakuwa karibu na wanawake waliotawanywa na machafuko ya takriban miaka mitano ya vita vya wenyewe kwa wenyewe. Mahusiano hayo yanaweza kuwawezesha watu wa jamii hiyo kuelewa haki zao na kupata fursa ya huduma. Maafisa wa polisi wanatumwa na nchi zao kufanya kazi maalumu, lakini pia wanawasili kikosi, kinachojulikana kama kikosi maalumu cha polisi kilichoundwa au FPU’s. Nchini Sudan Kusini karibu nusu ya kikosi maalum cha maafisa wa polisi kutoka Rwanda ni wanawake. Kimataifa idadi yao katika operesheni za ulinzi wa Amani ni asilimia 7 tu.

Kikosi cha kwanza na maafisa wa polisi wanawake watupu kutoka India kilipelekwa kwenye mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Liberia, UNMIL. Mpango huo hivi sasa umefungwa baada ya mafanikio ya kukamilisha operesheni zake. Hivi sasa kuna wanawake wawili tu ambao ni makamishina wa polisi katika operesheni 14 za Umoja wa Mataifa kote duniani. Unamisi Vuniwaqa kutoka Fiji ndiye mkuu wa operesheni za polisi kwenye mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, (UNMISS).

30 November 2018, 14:27