Tafuta

Vatican News
Ugonjwa wa TB bado unaendela kuua kwa mujibu wa Ripoti mpya iliyotolewa na  WHO Ugonjwa wa TB bado unaendela kuua kwa mujibu wa Ripoti mpya iliyotolewa na WHO  (ANSA)

Ripoti mpya ya WHO kuhusu ugonjwa wa Kifua kikuu imetolewa !

Wiki moja kabla ya Mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa juu ya Maambukizi ya kifua kikuu (TB) utakao anza tarehe 26 Septemba 2018 Shirika la Afya Duniani WHO limetoa Ripoti kamili juu ya TB kwa viongozi nchi kwa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa tarehe 18 Septemba. Ripoti inaonesha jinsi gani ni aibu dunia kushindwa kuthibiti maambukizi hayo

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Ripoti mpya ya Shirika la afya ulimwenguni WHO kuhusu hali ya ugonjwa wa  kifua kikuu duniani, TB  inasema kuwa  idadi ya watu waliougua kifua kikuu au kufariki dunia mwaka jana  ilikuwa ni ndogo ingawa bado mataifa mengi hayachukui  hatua za kutosha kuweza kutokomeza ugonjwa huo  ifikapo mwaka wa 2030.

Ripoti uliyotolewa tarehe 18 Septemba 2018 mjini New York, Marekani, kuhusa maambukizi ya kifua kikuu kupunguwa kwa mwaka 2017, inasema kuwa licha ya  juhudi duniani ambazo ziliweza kuzuia vifo vya watu milioni 54 kutokana na kifua kikuu tangu mwaka wa 2000, bado  TB inasalia kuwa ugonjwa hatari wa kuambukiza. Mkuu wa mpango wa TB wa Shirika la Afya ( WHO) Bi Tereza Kasaeva amewaambia waandishi wa habari kuwa “ Haikubaliki kwamba  katika karne hii ya 21 watu mamilioni wapoteze maisha yao kutokana na magonjwa ambayo sio tu yanazuilika lakini pia kutibiwa”.

Ameongeza kuwa kifua kikuu ni ugonjwa tegemezi kwa jamii na unahitaji hatua ya kutambua kukabiliana nao akisema kuwa  “Ni ugonjwa wa umaskini na bila kufikia watu maskini , bila kutoa hali muhimu kimaisha bila kutatua tatizo la utapiamlo ugonjwa huu haungeweza kutokomezwa.”Kadhalika Shirika la Afria duniani wamesema ili kuweza kufikia lengo la kutokomeza TB ifikapo mwaka wa 2030, mataifa yanahitaji kuharakisha mbinu za kuelekea mkabiliano na ugonjwa huo hususan  ufadhili wa ndani na nje.

Kwa kuzingazitia zaidi, Ripoti ya WHO inatoa taswira ya ugonjwa huo na pia changamoto na vilevile nafasi vinavyokabili mataifa  katika jukumu la kukabiliana na ugonjwa huo. Kwa ujumla vifo kutokana na kifua kikuu vimepungua mwaka jana ambapo mwaka 2017 kulitokea vifo milioni 1.6 vikijumuisha vifo 300,000 vya watu wenye virusi vya Ukimwi.  Na hiyo inathibitisha kuwa tangu mwaka wa 2000 idadi ya watu wenye Ukimwi wanaofariki dunia kutokana na TB  imepungua kwa asilimia 44 ikilinganishwa na asilimia 29 kwa watu wasio na Ukimwi. Ripoti inaongeza kuwa  mwaka 2017 duniani kote,   watu takriban  milioni 10,  waliugua  kifua kikuu.

Idadi ya maambukizi mapya inazidi kupungua kwa asilimia 2 kila mwaka, ingawa  kasi ya upunguaji kwa Ulaya ni asilimia 5 kila mwaka na Afrika asilimia 4 kila mwaka kati ya mwaka wa 2013 na 2017.  Ripoti inasema pia kuwa kuna wasiwasi wa kuwepo kwa aina ya  kifua kikuu ambacho ni sugu kwa dawa.

Mwaka jana 2017 watu 558,000 walikadiriwa kupata usugu kwa dawa aina ya rifampicin, moja yadawa madhubuti ya kutibu kifua kikuu. Ripoti inatoa wito kuhamasisha kujitolea katika pande za kitaifa na kimataifa na kuhimiza viongozi wa nchi na serikali ambao watakutana wiki ijayo kwenye mkutano wa kwanza wa Umoja wa Mataifa wa hali ya juu kuhusu kifua kikuu, wachukue hatua madhubuti.

19 September 2018, 16:07