Cerca

Vatican News
Kazi inamsaidia kijana asijiingize katika makundi maovu na kukimbia nchi yake Kazi inamsaidia kijana asijiingize katika makundi maovu na kukimbia nchi yake  (ANSA)

Afrika ya Kati:Kazi inamsaidia kijana dhidi ya makundi maovu!

Miaka mitano baada ya vita tangu mwaka 2013 katika nchi hii ya Afrika ya Kati , hadi sasa mapigano yanayoendelea kati ya wanamgambo wa Séléka na vikundi vya kupambana na Balaka, ambavyo baada ya muda wamepoteza nguvu katika mapigano japokuwa vijana wengi nao wanajiingiza katika makundi haya kutokana na ukosefu wa kazi

Frt. Titus Kimario – Vatican

Padre Félicien Endjimoyo, wa Kanisa la Mtakatifu Yohani huko Bambari, anaelezea jinsi miezi ya hivi karibuni, baada ya kifo askofu msaidia wa  Firmin Gbagoua mwishoni mwa mwezi Juni, kufuatia majeraha katika shambulio la kundi la waasi, hata mapadre wamelazimika kuhamia "katika eneo salama zaidi kwa maisha yao: Mchana wanaenda kwenye maparokia na kutekeleza huduma yao, wakati wa jioni wanalazimika kwenda maeneo salama zaidi. Kwa mantiki hiyo, kuanzia mwezi Julai mpaka leo shughuli za kichungaji zimekuwa hafifu". Lakini anaongeza kwamba, kwa sababu sasa ndio wakati wa "kurudi katika parokia zetu", kwa sababu wote mapadre  na watawa  pamoja na kwamba hatari ni "kubwa sana" hawataki kwenda.

Miaka mitano baada ya vita tangu mwaka 2013 katika nchi hii ya Afrika kutokana na mapigano yanayoendelea kati ya wanamgambo wa Séléka na vikundi vya kupambana na Balaka, ambavyo baada ya muda wamepoteza nguvu katika mapigano, sasa ni vikundi vya wanapiganaji, anaelezea Padre: "Umoja wa Mataifa umefanya mengi ili waasi watoke  Bambari, lakini kidogo kidogo wanarejea mjini na daima ni wale wale, Séléka na wapinga Balaka. Wanaiba na kupora katika kutafuta chakula, na kuleta hali hali halisi ya vita". Wanashambulia vitongoji vya kati, pamoja na maeneo ya vijijini zaidi, au ambako makambi yamehamishiwa: "Katika Bambari tuna tano, idadi kubwa ya wakazi huishi pale, na wachache tu wanaishi katika vitongoji" vya mji.

Mnamo Mei na Juni mwaka huu, Paroko wa parokia ya Mtakatifu Yohane anaendelea kufafanua kwamba, "hali ni mbaya sana", "katika hofu ya fujo", anathibitisha, "kumekuwa na mikutano mingi kati ya serikali na vikundi vya wapiganaji na hali imetulia kidogo. Sasa wametangaza maandamano ya kitaifa wakati wa Siku ya Chakula Duniani, Oktoba 16. Baadhi ya mashirika ya kibinadamu yameajiri vikundi vya vijana kwa kazi za umma na kwa njia hii, hufanya kazi na hawana fursa ya kujiingiza katika vikundi vya wanamgambo na waasi. Wanafanya kazi ya kurekebisha mitaa au kujenga makumbusho. Kwa njia hii wanaweza kujitoa kwa manufaa ya umma, badala kuiba na kufanya vurugu ".

Alihitimisha Padre Fèlicien kwamba matumaini yaliyoletwa na Papa Francisko katika ziara yake nchini Afrika ya Kati mnamo Novemba 2015 hayataisha, ni “ujumbe unaoongoza kwa usahihi utafutaji wa amani hata leo".

12 September 2018, 09:20