Sauti za wanawake watawa zinasikika kwa vitendo katika mawasiliano
Na Salvatore Cernuzio na Angella Rwezaula – Vatican.
Kuanzia na historia za msichana mdogo kutoka Amerika Kusini akiwa amekatwa miguu na treni iliyokuwa ikisafiri kuvuka Mexico, mbele ya mama yake. Msichana mwingine mwenye umri wa miaka 8 nchini Ufilipino alijifungia katika chumba chenye giza na shangazi yake aliyekuwa akiuza mwili wake mdogo mtandaoni. Mwanamke huyo, au tuseme, wanawake wengi wajawazito wa watesi wao nchini Uganda, walikataliwa na familia zao na kufunzwa kutengeneza silaha. Wakimbizi, watu wasio na makazi, vijana waathiriwa wa vurugu, familia maskini, watoto wenye utapiamlo, wasio na elimu au matibabu. Uzuri wa picha za karne ya kumi na sita katika Ukumbi wa Sistine haukutosha kulainisha mambo mazito tumboni kuhusiana na historia zilizokuwa zikisimuliwa na shuhuda zilizoripotiwa na watawa kutoka ulimwenguni wakati wa Mkutano wa Jubilei ya Watawa wa Mawasiliano uliofanyika asubuhi tarehe 23 Januari 2025, katika Maktaba ya Kitume ya Vaticani.
Kwa njia hiyo katika tukio, lililohamasishwa na Baraza la Kipapa la Mawasiliano kwa msaada wa Mfuko wa Hilton (pamoja wanashirikiana kwa Mpango wa Pentekoste) kama sehemu ya Jubilei unaojikita kwa wawasilianaji, kuanzia tarehe 24 hadi 26 Januari 2025, lakini katika sehemu hii ya watawa ilitaka kuwa jukwaa na maonesho ya uzoefu, kazi na misheni ya Watawa duniani kote. Hawa walikuwa ni wanawake kutoka pembe tofauti na jinsi gani njia za mawasiliano ya zamani na mpya ni zana ya msingi kwa uzoefu huu, kazi na misheni.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Dk. Paolo Ruffini, katika salamu yake ya kwanza katika mkutano huo alisisitiza kuwa "Shukrani kwa vyombo vya habari vya kijamii, radio, tovuti au kusikiliza tu, msichana wa Amerika Kusini alipelekwa kwenye kituo cha mapokezi ya wahamiaji, kisha Tennessee na ambako alipoteza viungo vyake, alipata tena tabasamu yake; Msichana wa Kifilipino aliyeokolewa kutoka katika hofu ya wavuti; Wanawake wa Uganda wamejifunza kushona mabegi na nguo, kuwapatia mahitaji yao binafsi lakini pia wale wa kijiji kilichowakataa. Na shukrani hizi zote, kwa usahihi, kwa mawasiliano, inayoeleweka kwa maana kuwa pamoja kwa kila mmoja na kwamba Mawasiliano kama zawadi ya pande zote.
Urithi wa Mfuko wa Hilton kwa mjibu wa Mjukuu wake Linda alisema kuwa "hii sawa na jukumu ambalo Conrad Hilton alikabidhi ambalo linachukua jina lake. Katika wosia wake, alikumbuka, kuwa Hilton alisema wazi kwamba: “sehemu kubwa zaidi ya pesa hizo ingeelekezwa ili kuwanufaisha watawa ulimwenguni pote." Baada ya kubaki mwaminifu kwa huduma hii tangu mwaka 1954," Linda Hilton aliongeza, katika miaka hii dola milioni 614 zimetolewa kwa watawa ambao wanatetea jamii, ambao wanahimiza amani na haki, hasa kama wana fursa ya kupata elimu au wana elimu na kuwa sauti kwenye meza ya maamuzi. Wakimama na dada wanaosomesha watoto, wanaowajali wenye uhitaji, wanamama na wale ambao ni wahanga wa dhuluma."
Na Mwandishi wetu wa habari wa Vatican, Devin Watkins akizungumza na Linda Hilton, Mwenyekiti wa Mfuko wa Conrad N. Hilton, nje ya Mkutano huo, alielezea juhudi za Chama hicho cha mfuko wa kutoa msaada wa kifedha kwa masista wa Kikatoliki katika misheni zao za kuhudumia mambo ya amani, haki, na elimu. Historia zao hazina budi kuinuliwa ili kila mtu aelewe kile kinachotokea kweli duniani, na watawa hawa wanafanya hivyo kwa moyo wao na huruma kwa wengine.” Linda Hilton, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mfuko wa Hilton, alishirikisha imani hiyo katika mahojiano kuhusu kazi ya masista wa Kikatoliki duniani kote. Alizungumza na Vatican News kando ya kongamano lenye kichwa “Kufuma Komunio kupitia Mawasiliano,” lililoandaliwa na Dicastery for Communication (chombo chetu kikuu). Tukio hilo liliwaleta pamoja kina dada 80 wa Kikatoliki ili kuchunguza jinsi wanavyoweza kuwasiliana na kazi yao ili kuinua sauti za wengine. Mfuko huo ulifadhiliwa na Conrad N. Hilton ambao ulianzishwa na mjasiriamali wa hoteli mnamo 1944. Bi. Hilton alishiriki kwamba yeye na wajumbe wengine wa bodi ya mfuko huo walitokwa na machozi waliposikia kuhusu kazi ya Sr. Norma Pimentel, MJ, ambaye anafanya kazi na wahamiaji kwenye mpaka wa Marekani na Mexico huko Texas.
"Kujua kinachoendelea huko kupitia maombi yao [ya ufadhili] kulinifungua macho," alisema Bi. Hilton. Kama Sr. Pimentel, ambaye alizungumza kwenye kongamano siku ya Alhamisi, kuwa kuna mamia ya maelfu ya watawa wengine wanaomtumikia Kristo katika watu kutoka pande zote za jamii, mara nyingi kwa ukimya lakini daima kwa upendo. Katika wosia wake akikabidhi sehemu kubwa ya mali yake kwa Mfuko wa Conrad N. Hilton, mfanyabiashara huyo wa hoteli aliomba kwamba masista wa Kikatoliki wanapaswa kuwakilisha uwekezaji mkubwa zaidi katika Kanuni ya Hilton. "Katika maono yetu, pendaneni, kwa kuwa hiyo ndiyo sheria yote," alinukuu Bi. Hilton, mjukuu wake. "Watu wa ulimwengu wanastahili kupendwa na kutiwa moyo, wasije wakaachwa, kutangatanga peke yao katika umaskini." Alisema bodi ya Mfuko wa Hilton inatafuta kujibu mahitaji yanayoendelea ya ulimwengu. Mradi mmoja unaofadhiliwa na Mfuko huo unatoa malezi endelevu kwa watawa katika mawasiliano na unafanywa kwa ushirikiano na Baraza la Kipapa la Mawasiliano. Kila mwaka, Masisita kadhaa hupokea mafunzo ya mtandaoni katika vyombo vya habari vya kisasa, na kadhaa hutumia miezi mitatu katika Ifisi za Baraza la Kipapa la Mawasiliano Roma kama wahitimu kupokea malezi ya kina.
Kando na kutoa mafunzo watawa vijana, Mfuko wa Hilton pia ulizindua "The Anna Trust for Elderly Catholic Sisters" mnamo tarehe 22 Januari. Ukiwa umeundwa kwa ushirikiano na Umoja wa Kimataifa wa Wakuu Mashirika (UISG), mpango huo utasaidia "mchakato wa kuzeeka wenye afya na heshima" kwa watawa duniani kote. Bi. Hilton na bodi ya wakurugenzi walikutana Jumatano tarehe 22 Januari mjini Vatican na Papa Francisko ambaye kujitolea kwake kwa walio hatarini zaidi na kujali wazee kulichochea msingi wa kuunda The Anna Trust. Alisema kuwa bodi iliona ni muhimu kusaidia masista wa Kikatoliki ambao wamejitolea maisha yao yote kuwahudumia wengine, akitolea mfano ripoti ya mwaka 2009 inayoonyesha kwamba wastani wa umri wa akina dada nchini Marekani wakati huo ulikuwa wa miaka 69. "Madada wa kidini hawahifadhi pesa wanazopata bali huwapa wakubwa wao kwa sababu ya kiapo chao cha umaskini," alisema Bi Hilton. "Kwa hivyo, wakati hakuna kitu kwao, ni muhimu kuingilia kati na kuwatunza."