Mazishi ya Kardinali Martino yamefanyika:bidii kwa wanyonge na wanaokandamizwa
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Mtu aliye wazi na mwenye utulivu, na ustadi mkubwa katika mahusiano na mazungumzo, ambaye ametumia maisha yake katika huduma ya Kanisa, Vatican na Papa na daima alikuwa tayari kuwa upande wa kupendelea watu wanaokandamizwa, katika haki zao na kuunga mkono walio dhaifu zaidi, kwa kufuata mfano wa Ndugu Cristoforo kutoka katika Liwaya ya "Promessi Siposi," ambayo alimvutia katika miaka yake akiwa katika shule ya sekondari. Ndivyo Kardinali Giovanni Battista Re, Dekano wa Baraza la Mardinali alivyomfafanua katika kumkumbuka Kardinali Renato Martino, aliyefariki dunia Jumatatu tarehe 28 Oktoba 2024, mjini Roma akiwa na umri wa miaka 91. Hayo yalisikika wakati wa Ibada ya Misa Takatifu iliyoongozwa alasiri Jumatano tarehe 30 Oktoba2024 , kwenye Alatare ya Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican.Misa hiyo iliwaona hata hivyo Wakonselebranti wapatao arobaini wakiwemo makadinali, maaskofu wakuu, maaskofu na mapadre, walikuwapo ambao waliungana na Papa kuongoza ibada ya kumuaga na ambayo ni pendekezo la mwisho kwa Mungu kukaribisha roho ya marehemu katika ushirika mtaktifu wa watakatifu,na kuaga mwili kabla ya maziko.
Katika mahubiri yake Kardinali Re alianza na kifungu cha Mtakatifu Paulo kwa Warumi “ Iwe tunaishi, iwe tutakufa sisi ni wa Bwana (Rm14,12), maneno yaliyosikia katika somo la kwanza, yakitukumbusha maana ya kweli ya maisha yetu na kifo. Hayo yanaangaza imani yetu na kutusaidia tumaini letu katika wakati huu wa kujikusanya katika sala kuzungukia altare ya Bwana, ili kumpatia salamu za mwisho ndugu Kardinali Renato Martino, ambaye Bwana amemwita akikaribia karibu miaka 92. Alikuwa na matatizo ya afya kwa muda mrefu na hakuweza tena kuondoka nyumbani. Hata hivyo, hadi hivi karibunu, aliadhimisha Misa kila asubuhi, akisherehekea pamoja na rafiki padre aliyekwenda kwake. Takriban siku kumi zilizopita, aliomba kupokea Sakramenti ya Mpako wa Wagonjwa. Wakati nguvu zake zilipokuwa zikipungua, Kardinali Martino alikaribisha machweo yake kwa utulivu wa mtu anayejua kwamba kufa kunamaanisha kuingia kwenye furaha ya milele.
Kwa hakika, maisha yetu hayaishii kaburini, bali katika nyumba ya Baba. Mauti ni Mungu wito kwa uzima wa milele. Uhakika huu uliangazia uwepo wake wote, ambao ulitumika kabisa katika huduma ya Kanisa, Vatican na Papa.” Mtu aliye wazi na mwenye utulivu, mwenye ujuzi mzuri wa mawasiliano na mazungumzo. Siku moja aliamini kwamba, akisoma Liwaya ya "Promessi Sposi" katika miaka yake ya sekondari, alivutiwa na sura ya Ndugu' Cristoforo na kwamba tangu wakati huo na kuendelea alishikilia katika maisha yake yote nia thabiti ya kuunga mkono watu kila wakati, wanaodhulumiwa k haki zao na kusaidia wanyonge.
Wasifu wake
Kardinali Re alianza kueleza wasifu wake kwamba: “Alizaliwa huko Salerno mwaka 1932, akapewa daraja la Upadre mwaka 1957. Baada ya kupata shahada ya Sheria ya Kanisa, mara moja aliingia katika huduma ya Vatican na kufanya kazi katika Ubalozi wa Vatican Nchini Nicaragua, Ufilipino, Lebanon, Canada na Brazil. Kisha akawa mkuu wa Sehemu ya Sekretarieti ya Nchi kwa Mashirika ya Kimataifa. Mwaka 1980 aliteuliwa kuwa Balozi nchini Thailand na Mjumbe wa Kitume kwenda Singapore, Malaysia na Laos. Baadaye, kwa muda wa miaka 16 alikuwa kwenye Umoja wa Mataifa huko New York kama Mwakilishi wa kudumu wa Vatican, ambapo hakuacha nguvu yoyote ya kushuhudia wasiwasi wa Papa kwa hatima na uzuri wa ubinadamu. Hotuba zake mbalimbali katika Mabaraza ya Umoja wa Mataifa zilikuwa na msukumo mkubwa, zilizohusu mada muhimu, kutoka kwa kupokonywa silaha hadi maendeleo, kutoka katika umaskini hadi kukuza haki za binadamu, kutoka katika ulinzi wa uhuru wa kidini hadi uokoaji wa wakimbizi, kutoka katika amani hadi maadili ya kibinadamu. Mnamo Oktoba 2002 aliitwa na Papa Yohane Paulo II kuongoza Baraza la Kipapa "Justitia et pax". La haki na amni. Alikuwa na wasiwasi wa kukamilisha na kisha kuchapisha Muhtasari wa Mafundisho Jamii ya Kanisa, ulioanzishwa na Mtangulizi wake, Kardinali Francois-Xaver Van Thuan.
Katika miaka hiyo alionesha kwamba alikuwa na usikivu mkubwa kwa matatizo ya kijamii na utetezi wa haki za binadamu, na alifunga safari nyingi kutoa mchango wake katika mikutano mbalimbali, akijitolea kwa furaha hasa katika kulinda familia na amani. Kunako mwaka 2005, kwa ushirikiano na taasisi mbalimbali za vyuo vikuu vya Kikatoliki, aliendeleza Kongamano la Kimataifa mjini Vatican kuadhimisha miaka 40 ya Katiba maridhiano “Gaudium et spes”. Kufuatia kuunganishwa kwa Baraza la Kipapa la wahamiaji na wasafiri na ile ya "Justitia et pax", Haki na Amani alifanya kazi kwa shauku kwa niaba ya wahamiaji, akikuza mipango mbalimbali. Alisimamia uchapishaji wa hati ya Maelekezo kwa ajili ya uchungaji wa mitaani. Aliundwa kuwa Kardinali na Papa Yohane Paulo II katika Baraza la Makardinali kunako 2003. Tangu 2014 alikuwa Kardinali Protodeacon.
Katika aina mbalimbali za shughuli zilizotekelezwa, roho iliyomfufua na bidii katika huduma ya Papa na Vatican zilifanana kila wakati, kama vile kujitolea kwa kuendelea katika kutafuta mema ya ubinadamu. Mazuri ya Kanisa na wema wa ubinadamu vilikuwa lengo na shauku ya maisha yake yote. Na tumaini katika uzima wa milele lilikuwa ni mtazamo wa furaha ambao aliishi nao siku zake. Sisi, tukiwa tumeuzunguka mwili wake, tunamsihi huruma ya Mungu kwa ajili ya Kardinali Martino, ambayoealiamini na kuitumaini daima. Katika Injili tulisikia maneno ya Yesu Kristo: “Mwaminini Mungu na kuwa na imani na mimi pia ninakwenda kuwaandalia makao...kisha nitakuja tena niwachukue pamoja nami, ili nilipo mimi nanyi mwepo." Ni maneno yaliyotamkwa wakati wa Karamu ya Mwisho, wakati mitume walipokuwa karibu kukutana na kushindwa dhahiri kwa Yesu kutokana na kifo chake msalabani. "Nikikuandalia mahali nitarudi na kukuchukua pamoja nami."
Sisi nasi tunashikamana na maneno haya ya Injili, tunapotoa Misa Takatifu kwa ajili ya marehemu Kardinali, tukimwomba Mwenyezi Mungu atujalie sisi pia kuendelea na safari yetu ya hapa duniani kwa uaminifu usio na kikomo katika huduma ya Kanisa na ndugu zetu. Mwishoni mwa adhimisho hili la Ekaristi, baada ya baraka ya mwili, ambayo itatolewa na Baba Mtakatifu, kwaya itaimba hivi: "“In Paradisum deducant te Angeli, in tuo adventu suscipiant te martyres et perducant te in sanctam civitatem Jerusalem”. Haya pia ni maombi yetu kwa mpendwa Kardinali Raffaele Martino ambaye, kwa kulitumikia Kanisa kwa uaminifu, alimtumikia Kristo.