Tafuta

Wakati za Siku ya Vijana huko Lisbon nchini Ureno 1-6 Agosti 2023. Wakati za Siku ya Vijana huko Lisbon nchini Ureno 1-6 Agosti 2023.  (Vatican Media)

Vijana kuelekea Sinodi,Jubilei na WYD huko Seuol,Korea Kusini

Kongamano la kimataifa lilillohamaishwa na Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha kuhusu mada ya uongozi lilifunguliwa na Kardinali Farrell na Askofu Mkuu Fisichella.Kutakuwa na WYD ijayo huko Seoul mnamo 2027. Zaidi ya hayo,kuna Sinodi na Jubilei ya vijana 2025,walioitwa Roma na Papa Francisko tarehe 28 Julai-3 Agosti 2025.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Njia panda ya matukio matatu muhimu ya uinjilishaji wa vijana yaani: Vijana kuelekea Sinodi, Jubilei na Siku ya Vijana Duniani (WYD) huko  Seoul nchini Korea Kusini  ndivyo Kardinali Kevin Farrell, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha (DLFV), alivyofafanua Kongamano la Kimataifa la Kichungaji la Vijana lililoanza Alhamisi tarehe 23 Mei 2024 kwenye makazi ya Carmelo, kilomita chache kutoka jijini Roma.Mkutano huo, unaohusisha takriban wajumbe 300 kutoka Mabaraza ya Maaskofu kutoka nchi 110, utahitimishwa  Jumamosi tarehe 25 na Mkutano na  Papa asubuhi na kwa mazungumzo ya wazi na Sekretarieti Kuu ya Sinodi, shukrani kwa mkutano wa alasiri watakuwa na katibu msaidizi Sr Nathalie Becquart.

Kwa shauku ya wale wanaotoka mbali

Washiriki, kwa shauku ya wale wanaotoka mbali, walianza kazi kwa maombi, na kisha wakajitayarisha kwa ajili ya kusikiliza kwa makini. "Kwanza kabisa - Kardinali alisema katika salamu yake ya utangulizi - tunajikuta kati ya Siku ya Vijana Ulimwenguni huko Lisbon na WYD ijayo huko Seoul mnamo 2027". Zaidi ya hayo, maadhimisho ya pili ni Jubilei ya vijana, walioitwa Roma na Papa Francisko kuanzia tarehe 28 Julai hadi 3 Agosti 2025 ili kuwa “mahujaji wa matumaini.” Hatimaye, Kongamano linafanyika katika mwaka ambapo maadhimisho ya miaka mitano ya kuchapishwa kwa Waraka wa Kitume baada ya sinodi wa Christus vivit ambapo  kumbukumbu yake inatupatia  fursa kwa mara nyingine tena kusisitiza baadhi ya vipengele vya msingi kwa huduma ya vijana, mhusika mkuu wa vijana, sinodi, mafunzo na usindikizwaji wa kiroho,” Alisisitza Kardinali Farell

Sikiliza maneno ya  Fisichella

Tafakari ya Kardinali ilianza, kwa hakika, kutokana na uzoefu wa sinodi na vijana aliokuwa nao mwaka 2018, baada ya -sinodi na katika kikao cha kawaida kuhusu mada "Vijana, imani na mang’amuzi ya miito”. "Katika hafla hiyo mchango wa vijana ulikuwa wa msingi kwa uandishi wa Christus vivit". Alisisitiza Kardinali Farrell.  Sinodi ya 2018 pia iliashiria mtindo mpya wa kufanya kazi na kusikiliza, unaofafanuliwa na Farrell kama "mfano kwa wote, kisha kupanuliwa kwa Kanisa zima" na ambayo, kama ilivyooneshwa katika Hati ya Mwisho ya Sinodi "ilichangia kwa sinodi ya kuamka", ambayo ni mwelekeo wa Kanisa" (Df 121): “Tunapitia "mwamko huu wa sinodi", katika ngazi mbalimbali, pamoja na Sinodi ya sasa ya sinodi," na pia inajumuisha siku za Kongamano linaloendelea, "lililofikiriwa kama uzoefu wa sinodi ya kusikiliza na kushiriki katika mwanga wa utambuzi  kiroho".

Ushuhuda kutoka kila nchi na kuwakilisha kama fursa adhimu ya kujifunza

Kardinali Farrell alichunguza mada ya njia ya "mazungumzo ya kiroho", iliyopendekezwa mara nyingi sana na Papa Francisko na kupitishwa katika Kongamano hili, ambalo wajumbe wawili kutoka kila nchi walialikwa: mkurugenzi wa huduma ya vijana au meneja mwingine na kijana. Kwa hivyo inawakilisha "fursa adhimu ya kujifunza kutoka kwa kila mmoja wetu na labda itatupa fursa ya kugundua viongozi wapya wachanga wenye uwezo wa kufungua upeo mpya wa matumaini katika miaka ijayo", alisema. "Vijana, kiukweli, wanaweza kuwa wahusika wakuu wa kufanywa upya ili Kanisa "lifunguliwe" na kuwa kijana tena". Zaidi ya hayo, wakati wa kazi ya kongamano, mada ya “Kwa huduma ya vijana ya sinodi: mitindo na mikakati mipya ya uongozi" inachunguzwa kwa kina, kuanzia Waraka wa  Christus vivit, hadi mgawanyiko ambao Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha wanajikita nao kwa mwaka 2024.

Jambo la kuthaminiwa sana katika siku hii ya kwanza ni uingiliaji kati wa Askofu Mkuu Salvatore Fisichella, Mwenyekiti Mwakilishi wa Baraza la Kipapa la uinjilishaji, ambaye alionesha maandalizi yanayoendelea kwa Jubilei ya Vijana. Askofu alisema kuwa hakutakuwa na katekesi wakati wa Jubilei hiyo, kwa sababu maandalizi yatafanyika katika kipindi kilichopita katika kila dayosisi yenye maaskofu, mapadre na makatekista wake.  Watakuwa vijana wa Roma  ambao watawakaribisha mahujaji kutoka pande zote za dunia, kwani "jimbo la Roma lina Papa kama askofu na ni jambo la kupendeza sana kwamba vijana wanaweza kuhudhuria kuwakaribisha vijana kwa tukio la pekee sana.

Askofu Mkuu Fisichella alieleza kuwa wakati huu pengine utafanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, lakini Uwanja wa Mtakatifu Yohane Laterano pia unaweza kufaa, kutokana na umuhimu wa mahali  hapo palipo na  Kanisa Kuu la Roma. Zaidi ya hayo, safari ya hija inayohusisha milango yote minne mitakatifu ya jiji imepangwa. Liturujia ya toba itafanyika kwenye Uwanja wa (Circus Maximus) na moyo wa maadhimisho hayo  utakuwa mkutano na Baba Mtakatifu Francisko katika  Uwanja wa  Tor Vergata, kama ilivyotokea miaka 25 iliyopita.”

“Tumejaribu kuwahimiza vijana waliokusanyika hapa kutoka pande zote za dunia, kutoka katika Mabaraza mbalimbali ya Maaskofu, kuchangamkia fursa ya kichungaji ya Jubilei”, alisisistiza Askofu Mkuu Fisichella kwa vyombo vya habari vya Vatican na kwamba “ hii ina maana ya kutafakari, katekesi, uwezo kufika Roma ukiwa  tayari umejiandaa kiroho."  Askofu mkuu aidha aliwataka wale waliohudhuria kwenye Kongamano kuwa sio tu watangazaji wa matumaini, lakini pia kuunda ishara thabiti za matumaini", ili kutekelezwa katika jumuiya zao. "Matumaini, ambayo ni tunda la teknolojia, pia ni muhimu sana kwa sababu yanatusaidia kuishi vizuri zaidi, lakini hayawezi kutoa wokovu, hayawezi kutoa maana ya maana ya maisha na kwa hivyo lazima tujaribu kutoka kwa matumaini hadi tumaini. Na tumaini tulilo nalo ni tumaini la Kikristo. Kwa hiyo njia ya kuelekea Jubilei ya vijana inapitia “ugunduzi upya wa imani” na “matumaini kama maandalizi ya kweli ili vijana wawe na wajibu wa kuinjilisha”.

 

Kujiandikisha

Kwa kujiandikisha katika Jubilei ya Vijana kutawezekana katika Mabaraza yao wenyewe ya Maaskofu, kwa vijana wenye umri wa miaka 18 hadi 30, kuanzia mwezi Novemba  24 hadi tarehe 31 Machi 2025.

Naye Paul Metzlaff, wa Baraza la Kipapa la Walei, Familia  Walei, Familia na Maisha, aliviambia vyombo vya habari vya Vatican kwamba katika miaka hii 40 tangu mkusanyiko wa kwanza na vijana - waliotafutwa na Papa Yohane Paulo II - Siku za Vijana Duniani zimekuwa nyingi na tofauti, huku zikidumisha baadhi ya vipengele  kwa pamoja: kupitia Njia ya Msalaba , mkesha, na misa ya mwisho. “Kila WYD ni sawa, lakini daima ni mpya, kulingana na utamaduni wa nchi mwenyeji". Utamaduni wa wenyeji, kwa kweli, una uzoefu katika familia na parokia na ndio unaoboresha uzoefu wa vijana. Kwa kuzingatia mkutano uliofuata huko Seoul, wakati huohuo, Baraza la Walei, Familia na Maisha tayari limeanza kutayarishwa, tukikumbuka kwamba lengo ni la uchungaji.  "WYD huko Lisbon ilikuwa tukio la ajabu kwetu sote, ambalo lilitufanya tujisikie wapya kabisa" na "njia tuliyojitayarisha ilikuwa kuomba na kujaribu kuwashirikisha vijana wengi iwezekanavyo".

Wakati Sara Angelucci, mmoja wa vijana waliokuwepo katika Kongamano hilo, akiwakilisha shirika la Kikatoliki la Denmark, alieleza kile ambacho mkutano wa kimataifa wa 2023 ulimaanisha kwa vijana wa Denmark. Katika nchi ambayo Wakatoliki ni asilimia 1% tu ya idadi ya watu, kukusanyika pamoja na kukua pamoja katika imani ni mwanzo mpya unaotarajiwa. Hatua ya kuwasili ni kuona tena tabia ya “ulimwengu ya Kanisa, katika Jubilei ya Vijana ya 2025 na kwenye Siku ya Vijana Duniani (WYD) huko Seoul mnamo 2027.

Kongamano la vijana kuelekea WYD na Jubilei 2025
24 May 2024, 18:14