Tafuta

2024.04.03 Mkesha wa sala mjini Vatican kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 19 ya kifo cha Yohane Paulo II. 2024.04.03 Mkesha wa sala mjini Vatican kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 19 ya kifo cha Yohane Paulo II.  (© don Paweł Rytel-Andrianik)

Miaka 19 tangu kifo cha Yohane Paulo II,alikuwa mtu wa Sala

Katika fursa ya kukumbuka kifo cha Mtakatifu Yohane Paulo II,kilichotokea tarehe 2 Aprili 2005,yalifanyika matukio kuanzia na ibada za misa katika Kikanisa cha Jasna Góra wa Częstochowa,kwenye groto za Vatican,pia Kanisa la Mtakatifu Stanslaus,Roma na usiku mkesha wa sala katika Uwanja wa Mtakatifu Petro,mjini Vatican kwa kuongozwa na Jumuiya ya Kipoland inayoishi Roma na watalii.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Atakumbukwa sana Papa mwenye nia ya  Kanisa la Milenia ya Tatu ambaye Makardinali, waliokusanyika katika mkutano uliomchagua kuwa Papa tarehe 16 Oktoba 1978, mara baada ya mtangulizi wake kuaga dunia na aliyedumu kwa kipindi cha mwezi mmoja tu. Katika kuchagua jina alipendelea kuitwa Yohane Paulo II na mnamo tarehe 22 Oktoba mwaka huo huo alianza huduma ya Kiti cha Mtume Petro, kama mrithi wa 263. Upapa wake ulikuwa ni mmoja wa kipindi kirefu zaidi katika historia ya Kanisa uliodumu karibu miaka 27.  Mazishi yake yalifanyika siku ya  Ijumaa tarehe 8 Aprili 2005 katika Uwanja wa Mtakatifu Petro na kuongozwa na Kardinali Joseph Ratzinger, aliyekuwa Dekano wa  Makardinali wa wakati huo(na ambaye baadaye atamrithi). Karol Wojtyła (Papa Yohane Paulo II),alizaliwa huko Wadowice, Kracow, mnamo 1920. Ili kutakagazwa kuwa  Mtakatifu Yohane Paulo II, miujiza miwili ilithibitishwa wa kwanza ukiwa ni  uponyaji wa Sr. Marie Simon-Pierre Normand kwa ugonjwa wa Parkinson na uponyaji wa Floribhet Mora. Pamoja naye alitangazwa na Mtakatifu Papa Yohane XXIII.

Mkesha wa sala kwa kukumbuka miaka 19 ya kifo cha Yohane Paulo II 2 Aprili 2024
Mkesha wa sala kwa kukumbuka miaka 19 ya kifo cha Yohane Paulo II 2 Aprili 2024

Kwa njia hiyo ni katika muktadha wa mwaka wa 19 tangu kifo cha Papa Yohane Paulo II ambapo  nchini Poland walimkumbuka Mtakatifu huyo hasa kama Papa wa sala  kwa kufanya matukio mengi sana ya maisha yake. Zawadi ya sala hata hivyo ilikuwa ni tabia ya Papa Karol Wojtyla na ambayo ilizunguzunguzwa katika  tarehe 2 Aprili 2024 katika mahubiri ya  Padre Paweł Rytel-Andrianik, msimamizi wa Idhaa ya Ipoland ya Radio Vatican na Huduma ya Habari Vatican. Akiwa katika Kikanisa kilichopo kwenye Groto za Vatican, kilichowekwa wakfu kwa Bikira Maria mweusi wa Jasna Góra huko Częstochowa, Padre Pawel alisisitiza kwa namna ya pekee ibada kuu ya Bikira na hata roho ya kimisionari ya Yohane Paulo II, upendo mkuu kwa vijana na imani thabiti katika huruma ya Mungu.

Mkesha wa sala tarehe 2 Aprili 2024 kukumbuka kifo cha Yohane Paulo II
Mkesha wa sala tarehe 2 Aprili 2024 kukumbuka kifo cha Yohane Paulo II

Siku hiyo hiyo tarehe 2 Aprili 2024 alasiri, Mtakatifu Yohane Paulo II alikumbukwa tena katika Litutujia iliyoadhimishwa katika Kanisa la Roma la Mtakatifu Stanislaus Askofu na Shahidi. Na usiku huo huo saa  (21.37), katika Uwanja wa Mtakatifu Petro walifanya mkesha maalumu wa sala kwa kushiriki hasa wapoland wanaoshi Italia na wawakilishi wa Makleri na wamashirika ya kitawa lakini pia hata watalii wengi ambao wamefika katika kutalii, ili kukumbuka siku ile ya kuaga dunia mnamo 2005. Na tarehe 27 Aprili 2024 itaadhimishwa miaka 10 tangu kutangazwa kwake kuwa Mtakatifu, ambapo alitangazwa na Baba Mtakatifu Francisko.

Tukirudi katika upendo na kuwatia moyo vijana Tunawezaje kusahau katika Waraka wake wa kitume Lettera Apostolica Nuovo Millenio Ineunte, yaani (Mwanzoni mwa milenia mpya) aliywaandikia Maaskofu Wakleri na Waamini Walei, Mwishoni mwa Jubilei ya 2000. Tukiwa katika maandalizi ya Jubilei ya 2025 ni vema kabisa kuusikia. Waraka wa kitume unaeleza vipaumbele vya Kanisa Katoliki kwa milenia ya tatu na kuendelea. Kwa hiyo Mtakatifu Yohane Paulo Aliandika kuwa: “Mikutano mingi ya Jubilei ilishuhudia aina mbalimbali za watu zikikusanyika, zikirekodi ushiriki wa kuvutia sana, ambao wakati fulani uliweka dhamira ya waandaaji na wahuishaji, wa kikanisa na kiraia, kwenye mtihani. Ningependa kuchukua fursa ya Barua hii kutoa shukrani zangu za dhati kwa kila mtu. Lakini zaidi ya idadi hiyo, kilichonisukuma mara nyingi ni uchunguzi wa kujitolea kwa dhati kwa sala, tafakari na ushirika ambao mikutano hii ilidhihirisha zaidi.

Papa Yohane Paulo II wakati wa WYD nchini Poloand 1991
Papa Yohane Paulo II wakati wa WYD nchini Poloand 1991

Na tunawezaje kusahau mkusanyiko wenye shangwe na kusisimua wa vijana? Ikiwa kuna taswira ya Jubilei ya Mwaka wa 2000 ambayo zaidi ya wengine watabaki hai katika kumbukumbu, hakika ni ile ya bahari ya vijana ambao niliweza kuanzisha mazungumzo ya upendeleo, juu ya msingi wa kuhurumiana na kuelewana kwa kina. Imekuwa hivi tangu ukaribisho niliowapa katika Uwanja wa  huko Laterano na Uwanja wa Mtakatifu  Pietro. Kisha nikawaona wakipita katikati ya jiji, wachangamfu kama vijana wanapaswa kuwa, lakini pia wenye mawazo, na hamu ya maombi, kwa "maana", kwa urafiki wa kweli. Haitakuwa rahisi, si kwao wenyewe au kwa wale walioziangalia, kufuta kutoka kwenye kumbukumbu zao juma ambalo Roma ilikuja kuwa "kijana pamoja na vijana". Haitawezekana kusahau adhimisho la Ekaristi ya Tor Vergata. Kwa mara nyingine tena, vijana wamejidhihirisha kuwa ni zawadi ya pekee ya Roho wa Mungu kwa Roma na kwa Kanisa.

Wakati wa sala kwenye mkesha wa kumbukizi ya miaka 19 ya kifo cha Papa Paulo II
Wakati wa sala kwenye mkesha wa kumbukizi ya miaka 19 ya kifo cha Papa Paulo II

Kuna wakati mwingine, tunapowaangalia vijana, wenye matatizo na udhaifu unaowatambulisha katika jamii ya kisasa, mwelekeo wa kukata tamaa... Kristo akionyeshwa uso wake wa kweli kwa vijana, wanahisi kama jibu la kusadikisha. wana uwezo wa kukaribisha ujumbe wake, hata kama unadai na kuwekewa alama na Msalaba. Kwa sababu hii, nikitetemeka kwa shauku yao, sikusita kuwaomba wafanye uchaguzi mkali wa imani na maisha, nikioneesha kazi ya kustaajabisha: ile ya kuwa "walinzi wa asubuhi" (rej. Is 21:11-12) katika mapambazuko ya Milenia mpya".

Mtakatifu Yohane Paulo II aliendelea kukazia kuwa: “Akieleweka katika fumbo lake la kimungu na la kibinadamu, Kristo ndiye msingi na kitovu cha historia, yeye ndiye maana yake na lengo kuu.... Umwilisho wake, unaofikia kilele katika Fumbo la Pasaka na zawadi ya Roho, ni moyo wa wakati unaovuma, saa ya ajabu ambayo Ufalme wa Mungu ulitujia (rej. Mk 1:15), kwa hakika ulitia mizizi katika historia yetu, kama mbegu iliyokusudiwa kuwa mti mkubwa (taz. Mk 4:30-32).  Mpango tayari upo: ni mpango unaopatikana katika Injili na katika Mapokeo hai, ni sawa na milele. Hatimaye, ina kitovu chake katika Kristo mwenyewe, ambaye anapaswa kujulikana, kupendwa na kuigwa, ili kwamba ndani yake tuweze kuishi maisha ya Utatu, na pamoja naye kubadilisha historia hadi utimizo wake katika Yerusalemu ya mbinguni. Huu ni mpango ambao haubadiliki na mabadiliko ya nyakati na tamaduni, ingawa inachukua nafasi ya wakati na utamaduni kwa ajili ya mazungumzo ya kweli na mawasiliano ya ufanisi. Mpango huu wa nyakati zote ni mpango wetu wa Milenia ya Tatu.”

“Tunatamani kumwona Yesu” (Yh 12:21). Ombi hili, lililoelekezwa kwa Mtume Filipo na baadhi ya Wagiriki waliokuwa wamehiji Yerusalemu kwa ajili ya Pasaka, linasikika kiroho katika masikio yetu pia katika Mwaka huu wa Jubilei. Kama wale mahujaji wa miaka elfu mbili iliyopita, wanaume na wanawake wa siku zetu - mara nyingi labda bila kujua - huwauliza waamini sio "kuzungumza" tu juu ya Kristo, lakini kwa maana fulani "kumwonesha" kwao. Na je, si kazi ya Kanisa kuakisi nuru ya Kristo katika kila kipindi cha kihistoria, kuufanya uso wake uangaze pia mbele ya vizazi vya milenia mpya? Hata hivyo, ushahidi wetu ungekuwa duni ikiwa sisi wenyewe hatungeutafakari uso wake kwanza. Jubilei Kuu hakika imetusaidia kufanya hili kwa undani zaidi. Mwishoni mwa Jubilee, tunaporudi kwenye utaratibu wetu wa kawaida, tukihifadhi ndani ya mioyo yetu hazina za wakati huu wa pekee sana, macho yetu yamewekwa kwa uthabiti zaidi kuliko wakati mwingine wowote juu ya uso wa Bwana.(NMI 16). Kwa hiyo katika Waraka huo Mtakatifu Yohane Paulo II aliandika: “ Kujitolea kwa pekee kunahitajika kuhusiana na vipengele fulani vya ujumbe mkali wa Injili ambavyo mara nyingi havieleweki vizuri, hata kufikia hatua ya kufanya uwepo wa Kanisa kutopendwa na watu, lakini ambao hata hivyo lazima uwe sehemu ya utume wake wa upendo.

Papa Yohane Paulo II akiwa katika uwakilishi wa Katekesimu ya Kanisa katoliki 1992
Papa Yohane Paulo II akiwa katika uwakilishi wa Katekesimu ya Kanisa katoliki 1992

Ninazungumza juu ya jukumu la kujitolea kuheshimu maisha ya kila mwanadamu, tangu kutungwa mimba hadi kifo cha kawaida. Vivyo hivyo, huduma ya wanadamu hutuongoza kusisitiza, katika msimu na nje ya msimu, kwamba wale wanaotumia maendeleo ya hivi karibuni ya sayansi, haswa katika uwanja wa teknolojia ya kibayoteki, kamwe wasipuuze matakwa ya kimsingi ya kimaadili kwa kukaribisha mshikamano wenye kutiliwa shaka ambao hatimaye unasababisha kubagua kati ya maisha moja na mengine na kupuuza utu ambao ni wa kila binadamu. Ili ushuhuda wa Kikristo na kuwa na ufanisi, hasa katika maeneo haya tete na yenye utata, ni muhimu jitihada za pekee zifanywe kueleza ipasavyo sababu za msimamo wa Kanisa, huku akisisitiza kwamba si suala la kuwawekea wasioamini maono yanayojikita katika misingi ya imani,bali ya kufasiri na kutetea maadili yaliyokita mizizi katika asili ya utu. Kwa njia hii upendo ni lazima uwe huduma kwa utamaduni, siasa, uchumi na familia, ili kanuni za kimsingi zinazotegemea hatima ya wanadamu na mustakabali wa ustaarabu ziheshimiwe kila mahali. Akielezea Changamoto za leo Mtakatifu Yohane Paulo II alisema “

Na tunawezaje kubaki kutojali matarajio ya mgogoro wa kiikolojia ambao unafanya maeneo makubwa ya sayari yetu kuwa yasiyokaliwa na yenye uadui kwa wanadamu? Au na matatizo ya amani, ambayo mara nyingi yanatishwa na mzuka wa vita vya misiba? Au kwa kudharau haki msingi za binadamu za watu wengi hasa watoto? Isitoshe ni dharura ambazo kila moyo wa Mkristo lazima uwe mwangalifu kwazo. (Rej. NMI51.)

Watawa wa familia ya Kipapa
Watawa wa familia ya Kipapa

Moja ya matashi mema katika ujumbe aliowatumia vijana kwenye jukwaa la kimataifa la vijana kuanzia tarehe 31 Machi hadi 4 Aprili 2004 aliwambia kuwa “Vijana na vyuo vikuu: kushuhudia Kristo katika mazingira ya chuo kikuu" ambayo ilikuwa ni mada. Uwepo wenu ni chanzo cha furaha kubwa kwangu, kwa kuwa ni ushuhuda unaong'aa kwa uso wa Kanisa zima, na wachanga daima. Kwa kweli, unatoka katika mabara matano na unawakilisha zaidi ya nchi 80 na harakati 30 za kimataifa, vyama na jumuiya. Vijana marafiki! Ninyi ni wanafunzi na mashahidi wa Kristo katika vyuo vikuu. Basi ninaomba wakati wenu wa chuo kikuu, kwenu nyote, muw wakati wa ukomavu mkuu wa kiroho na kiakili, ambao unawaongoza kuimarisha uhusiano wenu binafsi na Kristo. Lakini ikiwa imani yeny inahusishwa kwa urahisi na vipande vya mila, hisia nzuri au itikadi ya jumla ya kidini, hakika hamtaweza kuhimili athari za mazingira. Kwa hiyo, mjaribu kubaki imara katika utambulisho wenu wa Kikristo na uliokita mizizi katika ushirika wa kikanisa. Kwa hili, mjiridhisheni kwa maombi ya bidii.

Mchague, inapowezekana, walimu wazuri wavyuo vikuu. Msibaki pekee katika mazingira ambayo mara nyingi ni magumu, lakini mshiriki kikamilifu katika maisha ya vyama, harakati na jumuiya za kikanisa zinazofanya kazi katika mazingira ya vyuo vikuu. Mwende kwenye parokia za vyuo vikuu na mjiruhusu msaidiwe na wachungaji. Ni lazima tuwe wajenzi wa Kanisa katika Vyo vikuu, yaani, jumuiya inayoonekana inayoamini, inayosali, inayoleta matumaini na inayokaribisha kwa upendo kila dalili ya mema, ukweli na uzuri wa maisha ya Vyuo vikuu. Haya yote sio tu kwenye vyuo vikuu, lakini popote wanafunzi wanaishi na kukutana. Nina hakika kwamba Wachungaji hawatakosa kuweka uangalizi maalum kwa mazingira  ya vyuo vikuu na watateua mapadre watakatifu na wenye uwezo katika utume huu.

Siku ya Vijana 1993
Siku ya Vijana 1993

“Haitoshi "kuzungumza" juu ya Yesu kwa wanafunzi vijana  wa vyuo vikuu: lazima pia tuwafanye "kumwona" kupitia ushuhuda wa maisha ulio wazi (rej. Novo millennio ineunte, 16). Ninatumaini kwamba mkutano huu huko Roma utachangia katika kuimarisha upendo wako kwa Kanisa la ulimwengu wote na kujitolea kwako kutumikia ulimwengu wa chuo kikuu. Nategemea kila mmoja wenu kuwapitishia Makanisa yenu ya mahali pamoja na makundi yenu ya kikanisa utajiri wa karama mnazopokea katika siku hizi kali.”

Kumbukizi ya miaka 19 tangu kifo cya Mtakatifu Yohane Paulo II
03 April 2024, 15:01