Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko ameteua Askofu mkuu Martin Krebs kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Monaco na Uswisi na ataendelea kuwa ni Mwakilishi wa Vatican kwenye utawala wa Liechtenstein. Baba Mtakatifu Francisko ameteua Askofu mkuu Martin Krebs kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Monaco na Uswisi na ataendelea kuwa ni Mwakilishi wa Vatican kwenye utawala wa Liechtenstein.   (Vatican Media)

Askofu mkuu Martin Krebs, Balozi Mpya wa Vatican Nchini Monaco, Uswiss na Liechtenstein

Askofu mkuu Martin Krebs kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Monaco na Uswisi na ataendelea kuwa ni Mwakilishi wa Vatican kwenye utawala wa Liechtenstein. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Martin Krebs alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Uruguay. Alizaliwa tarehe 2 Novemba 1956, huko Ujerumani. Tarehe 10 Oktoba 1983 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tarehe 8 Septemba 2008 akateuliwa na Papa Benedikto XVI kuwa Askofu mkuu na Balozi wa Vatican Mali na G.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S., Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko ameteua Askofu mkuu Martin Krebs kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Monaco na Uswisi na ataendelea kuwa ni Mwakilishi wa Vatican kwenye utawala wa Liechtenstein. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Martin Krebs alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Uruguay. Amewahi pia kuwa Balozi wa Vatican nchini Guinea na Mali; Balozi wa Vatican kwenye Visiwa vya Marshall na Nauru; New Zealand Visiwa vya Cook, Fiji, Kribati, Palau, Samoa, Shirikisho la Micronesia, Tonga, Vanuatu na pia mwakilishi wa kitume kwenye Bahari ya Pacific. Tarehe 3 Machi 2021 Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa ni Balozi wa Vatican nchini Uruguay na Ufalme wa Liechtenstein.

Askofu mkuu Martin Krebs, Balozi Monaco, Uswisi na Liechtenstein
Askofu mkuu Martin Krebs, Balozi Monaco, Uswisi na Liechtenstein

Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Krebs alizaliwa kunako tarehe 2 Novemba 1956 huko Essen, Ujerumani. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, akapewa Daraja Takatifu ya Upadre hapo tarehe 10 Oktoba 1983. Tarehe 8 Septemba 2008, akateuliwa na Baba Mtakatifu Benedikto XVI kuwa Askofu mkuu na Balozi. Tarehe 16 Novemba 2008 akawekwa wakfu kuwa Askofu mkuu katika Ibada iliyoongozwa na Kardinali Tarcisio Bertone, aliyekuwa Katibu mkuu wa Vatican kwa wakati ule.

Uteuzi Uswisi

 

19 April 2024, 15:04