Tafuta

Jimbo la Eldoret (Kenya)limempanta askofu msaidizi Mheshimiwa Padre   Kiplimo. Jimbo la Eldoret (Kenya)limempanta askofu msaidizi Mheshimiwa Padre Kiplimo. 

Papa amemteua Padre John Kiplimo Lelei kuwa Askofu msaidizi wa Eldoret,Kenya

Padre John Kiplimo Lelei alizaliwa mnamo tarehe 15 Agosti 1958 huko Soy,katika Jimbo katoliki la Eldoret.Alisoma falsafa katika Seminari Kuu ya Mtakatifu Agustino huko Mabanga na Taalimungu katika Seminari Kuu ya Mtakatifu Thomas Aquinas jijini Nairobi.Alipewa daraja Takatifu la Upadre mnamo tarehe 26 Oktoba 1985 kwa ajili ya Jimbo la Eldoret.Hadi uteuzi huo alikuwa ni makamu Askofu Jimbo.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Jumatano tarehe 24 Machi 2024, Baba Mtakatifu amemteua Askofu Msaidizi wa  Jimbo la katoliki la Eldoret nchini Kenya, Mheshimiwa sana  Padre  John Kiplimo Lelei, wa Jimbo hilo la  Eldoret, ambaye hadi uteuzi huo alikuwa ni makamu Jimbo  hilo na kupewa makao ya Monte ya  Numidia.

Nyadhifa na masomo

Padre John Kiplimo Lelei alizaliwa mnamo tarehe 15 Agosti 1958 huko Soy, katika Jimbo katoliki la  Eldoret. Alisoma falsafa katika Seminari Kuu ya Mtakatifu Agustino huko Mabanga na Taalimungu  katika Seminari Kuu ya Mtakatifu Thomas Aquinas jijini Nairobi. Alipewa daraja Takatifu la Upadre mnamo tarehe 26 Oktoba 1985 kwa ajili ya Jimbo la Eldoret. Alishikilia nyadhifa mbali mbali pamoja na kuendelea na masomo zaidi: Shahada ya Uzamivu katika Taalimungua, aliyebobea katika Liturujia, katika  Chuo Kikuu ha Wien(Viena Austria); Paroko wa  Parokia ya Suwerwa na Chepterit (1985-1987); Paroko wa Parokia ya Yamumbi, Suwerwa, Chepterit na Tachasis, na Makamu wa Forane wa Dekania ya Kitale na Nandi (1987-1996);

Mhesmiwa Padew Lelei aidha amekuwa mshiriki Parokia ya Mtakatifu Brigitta na Zum Gottlichen Erloser, katika Jimbo kuu la Vienna (1996-2002); Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Patrick huko Kapcherop (2002-2003); Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Boniface huko Tindinyo (2003-2007); Mwalimu katika Taasisi ya Kichungaji ya AMECEA ya Gaba (2003-2004); Taasisi ya Mafunzo ya Maendeleo huko Kobujoi (2004-2009) na katika Seminari Kuu ya Mtakatifu Matthias Mulumba-Tindinyo (2003-2008); Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Petro huko Kapsabet (2007-2008); Mwalimu na mkufunzi katika Seminari Kuu ya Mtakatifu Matthias Mulumba iliyopo Tindinyo (2008-2017); Mkuu wa Seminari Kuu ya Mtakatifu Thomas Aquinas jijini Nairobi (2017-2023). Na hadi uteuzi alikuwa makamu wa Jimbo la Eldoret.

Papa amemteua Askofu Msaidizi wa Jimbo la Eldoret nchini Kenya
27 March 2024, 16:08