Tafuta

2024.03.02 Papa amekutana na Olaf Scholz, Kansela wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani. 2024.03.02 Papa amekutana na Olaf Scholz, Kansela wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani.  (Vatican Media)

Papa amekutana na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz

Mkuu wa serikali ya Ujerumani alifanya mazungumzo na Papa na baadaye akakutana na Katibu wa Vatican,Kardinali Parolin na Monsinyo Mirosław Wachowski,Katibu Msaidizi wa Mahusiano na Mataifa.Alizungumzia suala la uhamiaji na haja ya kutafuta suluhisho la kidiplomasia ambalo litawezesha kusitishwa uhasama haraka iwezekanavyo nchini Ukraine na Israel na Palestina.

Vatican News

Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Kansela wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani, Olaf Scholz, Jumamosi tarehe 2 Machi 2024  katika Jumba la Kitume. Baadaye, Scholz, kwa mujibu wa  taarifa kwa vyombo vya habari kutoka Ofisi ya Waandishi wa Habari ya Vatican  ilivyoarifu, “alikutana na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican, akifuatana na Monsinyo Mirosław Wachowski, Katibu  Msaidizi wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa.”

Papa na Kansela wa Ujerumani
Papa na Kansela wa Ujerumani

Wakati wa mazungumzo katika Sekretarieti ya Vatican, wameonesha kuridhika kwa uhusiano mzuri na ushirikiano wenye manufaa uliopo kati ya Vatican na Ujerumani, huku wakionesha umuhimu wa imani ya Kikristo katika jamii ya Ujerumani. Kisha waliakisi "baadhi ya masuala ya maslahi ya pamoja, kama vile hali ya uhamiaji na marejeo  maalum yalitolewa kuhusu migogoro ya Ukraine na Israeli na Palestina, na dhamira iliyofuata ya amani, katika kutafuta bila kuchoka suluhisho la kidiplomasia ambayo itawezesha kusitishwa kwa uhasama haraka iwezekanavyo.”

Kansela wa Ujerumani baadaye alikutana na Sekretarieti ya Vatican
Kansela wa Ujerumani baadaye alikutana na Sekretarieti ya Vatican

Wakati wa ubadilishanaji wa zawadi za kiutamaduni, Scholz alimpatia Papa mpira rasmi wa Kombe la Ulaya 2024 (UEFA EURO 2024) na sanamu ya udogo ya dubu na nembo ya Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani.

Wakati wa kubadilisha zawadi
Wakati wa kubadilisha zawadi

Na kutoka kwa Baba Mtakatifu alimpatia, kazi ya shaba yenye kichwa “Upendo wa Kijami”, inayoonesha mtoto akimsaidia mwingine kuamka, na imeandikwa: “Msaada wa Upendo;” aidha wingi wa hati za upapa; Ujumbe wa Amani wa mwaka huu 2024; kitabu Njia ya Msalaba(Statio Orbis ya 27 Machi  2020), kilichohaririwa na LEV.

Papa akutana na Kansela wa Ujerumani
02 March 2024, 14:47