Tafuta

Papa  Francisko amekutana na Rais wa  Seychelles Bwana Wavel Ramkalawan. Papa Francisko amekutana na Rais wa Seychelles Bwana Wavel Ramkalawan.  (ANSA)

Papa akutana na Rais wa Jamhuri ya Seychelles

Papa amekutana na Rais wa Jamhuri ya Seychelles,Bwana Wavel Ramkalawan na mara baada ya mkutano huo pia amekutana na Kardinali Parolin,Katibu wa Vaican,akiambatana na Askofu Mkuu Gallagher,Katibu wa Vatican wa Mhusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Jumamosi, 16 Machi 2024, Baba Mtakatifu Francisko amekutana katika Jumba la Kitume Vatican na Rais wa Jamhuri ya Seychelles, Bwana Wavel Ramkalawan, ambaye mara baada ya mkutano huo pia Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican, akiambatana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa Mhusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa

Kwa mujibu wa Taarifa kutoka Ofisi ya Vyombo vya Habari Vatican inabainisha kuwa wakati wa mazungumzo yao na Sekretarieti  wameonesha kwa uhai wote pongezi za  mahusiano mema yaliyopo uzote mbili kati ya Vatican na Jamhuri ya watu wa Seychelles, ambapo ni pamoja na mchango wa Kanisa Katoliki katika Huduma kwa jamii hasa, katika mantiki ya utunzaji na Elimu.

Rais wa Ramkalawan na Sekretarieti ya Vatican
Rais wa Ramkalawan na Sekretarieti ya Vatican

Hatimaye, katika mazungumzo hayo wamebadilishana mitazamo juu ya hali ya kijamii na kisiasa katika Nchi. Kwa kusisitiza kwa namna ya pekee mada muhimu za pamoja, miongoni ni ulinzi wa watoto na mapambano dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya, na vile vile kuzungumzia juu ya hali za kimataifa.

Mkutano wa Rais wa Jamhuri ya Sychelles na Sekretarieti ya Vatican
Mkutano wa Rais wa Jamhuri ya Sychelles na Sekretarieti ya Vatican

Katika ziara hiyo rais alifika mjini Vatican kuanza mkutano saa 2.25 hadi 2.40 na  kuondoka karibu  saa 2.50 asubuhi. Lakini pamoja na hayo hawakukosa kubadilishana zawadi ambapo Baba Mtakatifu amemzawadia Rais, Sanamu ya shaba, yenye kauli mbiu: “Utunzaji wa Uumbaji”; Hati za kipapa; Ujumbe wa Amani wa 2024; kitabu cha Njia ya Msalaba(Statio Orbis cha tarehe  27 Machi  2020, kilichohaririwa na Nyumba ya Vita Vatican ( LEV); na hatimaye kitabu cha Nyumba ya Kipapa chenye katekesi , kilichohaririwa na Mkuu wa Nyumba ya Kipapa.

Wakati wa kubadilisha zawadi za kiutamaduni
Wakati wa kubadilisha zawadi za kiutamaduni

Kwa upande wa Rais wa Seychelles: Mchono  wa shaba wa Kombe   kwenye mchanga; Muanzi wa Jadi uliochorwa picha ya Bikira Maria.

Kubadilishana zawadi
Kubadilishana zawadi
Papa amekutanza na Rais wa Seychelles
16 March 2024, 17:39