Tafuta

2024.03.02 Papa akutana na Kamati ya Maandalizi ya Siku ya I ya Watoto Duniani (25-26 Mei 2024). 2024.03.02 Papa akutana na Kamati ya Maandalizi ya Siku ya I ya Watoto Duniani (25-26 Mei 2024).   (Vatican Media)

Papa akutana na Kamati ya maandalizi ya Siku ya Watoto duniani

Jumamosi 2 Machi 2024 alasiri Papa alikutana na Kamati ya maandalizi ya Siku ya Watoto Duniani itakayofanyika tarehe 25 na 26 Mei 2024.Aliyeongoza jopo hilo alikuwa ni Mratibu,Padre Enzo Fortunato,na Monsinyo Cesare Pagazzi,Katibu wa Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu, waliokuwepo Katibu Mratibu wa Kamati hiyo na wengine .

Vatican News

Kwa mujibu wa taarfa kutoka Ofisi ya Vyombo vya habari  mjini Vatican kwa waandishi ni kwamba: “Leo mchana saa 9:00 alasiri katika Nyumba ya Mtakatifu Marta, mjini Vatican Baba Mtakatifu Francisko amepokea Kamati ya Maandalizi ya Siku ya Wtoto Duniani, pamoja na hafla ya kuchapishwa kwa ujumbe wake kwa ajili ya tukio hilo.”

Kwa mujibu wa taarifa  kutoka Ofisi ya Vyombo vya Habari Vatican kwa waandishi wa habari inabainisha kuwa “akiwasalimu waliohudhuria, Papa alitoa baadhi ya maneno ya shukrani kwao, akishangaa juu ya mateso ya watoto, hata katika hali ya migogoro, juu ya unyonyaji wao, na akitumaini kwamba Siku hiyo inaashiria "kuinua ufahamu" kwa maana hiyo pana.”

Papa akikutana na waandaaji wa Siku ya I ya watoto Duniani(25-26 Mei 2024)
Papa akikutana na waandaaji wa Siku ya I ya watoto Duniani(25-26 Mei 2024)

Kamati hiyo iliongozwa na Mratibu, Padre Enzo Fortunato, na Monsinyo Cesare Pagazzi, Katibu wa Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu, na waliokuwepo Katibu Mratibu wa Kamati hiyo, Aldo Cagnoli, na wawakilishi wa baadhi ya vyombo vinavyohusika zaidi vya  maandalizi kama vile  Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, Ushirika wa Auxilium,Shirikisho la Soka la Italia, pamoja na Mkuu wa Ujumbe wa Timu ya Taifa ya Italia, viongozi wa Michezo na Afya, wajumbe wa Manispaa ya Roma, Mkoa wa Lazio, Kundi la Reli ya Taifa(FS) na taasisi mbalimbali zinazopenda kuandaa Siku hiyoMkutano huo baadaye ulihitimishwa mara.

02 March 2024, 18:41