Tafuta

Askofu Mkuu Gallagher, Katibu wa Vatican wa mahusiano na Nchi na Mashirika ya Kimataifa Askofu Mkuu Gallagher, Katibu wa Vatican wa mahusiano na Nchi na Mashirika ya Kimataifa 

Gallagher:Mazungumzo yanahitajika kukomesha vita&ulinzi unapatikana kati ya makubaliano ya watu!

Katika mahojiano ya Televisheni ya Italia1(Tg1,yaliyotangazwa 26 Machi 2024, Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa alizungumzia juu shambulio la Moscow na kuhusu mustakabali wa Ulaya na ulimwengu,vita vya Ukraine na Mashariki ya Kati,alisisitiza kuwa suluhisho linapswa kuwa kwa wahusika wote wawili na wa Mataifa.

Vatican News

Mashambulizi ya kutisha huko Moscow, ukosefu wa utulivu wa jumla Ulaya na ulimwengu, msisitizo wa kufanya kazi kwa ajili ya amani na kujaribu kukuza amani nchini Ukraine kupitia mazungumzo na utetezi ambao haufanyiki kwa silaha tu, bali kwa makubaliano; kisha juu ya hofu ya kuongezeka kwa nyuklia, na utaratibu mpya wa dunia baada ya kukomesha migogoro; Mtazamo wa Nchi Takatifu  kwa matumaini ya  wahusika wawili na ufumbuzi wa mataifa hayo mawili  na maumivu kwa hali ya janga huko Gaza, haja ya kufanya upya uongozi wa Palestina na suala la mateka wa Israel. Vile vile wazo jingine kuhusiana na Malkia Kate wa Uingereza kuhusu hali ya afya yake, pia  afya ya Papa Francisko, ambaye anaonekana mwenye nguvu na amedhamiria sana lakini ambaye labda"anajaribu kusawazisha juhudi zake kwa maadhimisho ya Juma Takatifu katika siku hizi, na ambaye hata hivyo daima anafanikiwa kutushangaza.  Haya yote yalikuwa mahojiano mapana yaliyotangazwa usiku wa tarehe 26  Machi 2024 kwenye Televisheni ya Italia( Tg1) kati ya  Askofu Mkuu  Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa na taalamu wa Masuala ya Vatican. Akiwa amerudi kutoka safari ya Montenegro na,hata kabla ya hapo, hadi Jordan, Askofu mkuu alitoa  maoni juu ya matukio ya sasa ya kimataifa akielezea juu ya mtazamo wa Vatican.

Shambulio huko Moscow

Mazungumzo na mtaalam wa Vatican na Ignazio Ingrao yaliaanzia kutoka shambulio la hivi karibuni huko Moscow nchini Urusi ambapo alisema “ni jambo la kutisha ambalo lazima litufanye tutafakari, kwa sababu tunaweza kuona kwamba kuna mambo katika jamii zetu ambayo yanataka tu kuharibu na kufanya watu kuteseka.” Aidha alionesha kama kweli hatari kwamba mauaji huko Moscow yanaweza kuchochea zaidi hali ya ulimwengu kwamba  “Nchi ambayo inakabiliwa na kiwewe kama hiki inaweza pia kujibu kwa nguvu sana, kama Israeli ilijibu baada ya 7 Oktoba.” Alieleza kuwa “kukosekana kwa utulivu huu wote ni matokeo ya kuvunjwa kwa amri ambayo tulifikiri kuwa tumeiweka baada ya vita viwili vya dunia, baada ya Vita Baridi ambapo mataifa yalitatua migogoro yao kwa kujadiliana, kuzungumza, kujadiliana, mazungumzo,” alisema Askofu Mkuu kwa Gallagher. Kwa kuongeza: “Leo haionekani tena kwamba kuna kuzingatia sheria, lakini badala yake kutokuwa na imani kwa taasisi zetu, kuanzia na UN, OSCE na Ulaya yenyewe, nguzo za ulimwengu wetu kwa miongo mingi ambayo hata hivyo  sasa haiwezi au haionekani kuwa na uwezo wa kukabiliana na changamoto hizi kubwa.”

Vita vya Ukraine

Mtazamo uliahamia huko  Ukraine na wito wa hivi karibuni wa  Papa Francisko kwenye njia ya mazungumzo.  Askofu Mkuu Gallhaere alisema: “Papa amekuwa akisema kwamba vita vinaishia kwenye meza ya mazungumzo. Ninaamini kwamba Papa alitaka kuhimiza upande wa Kiukraine kufanya mazungumzo kwa manufaa ya nchi.” Wakati huo huo, ninaamini kuwa Vatican daima imekuwa wazi sana na upande wa Urusi, ikiomba kwamba wao pia wanapaswa kutuma ishara kwa maana hii, kuanzia na kuacha kurusha makombora kwenye eneo la Kiukraine . Na migogoro, silaha na migogoro yote ya kila siku lazima ikome.”

Ulinzi sio suala la silaha tu

Tena akikumbuka mawazo ya Papa Francisko, Askofu Mkuu Gallagher alijibu swali juu ya kuanzishwa upya kwa mpango  wa ulinzi wa Ulaya na kusema kwamba: “Ulaya lazima ichukue jukumu la ulinzi wake lakini wakati huo huo ulinzi sio tu suala la silaha, lakini badala yake ulinzi muhimu ambao unafanywa kupitia taasisi, kukuza makubaliano kati ya watu.” Hofu ya nguvu za nyuklia na mpangilio mpya wa ulimwengu baada ya migogoro kutokana na hali hiyo, Katibu wa Mahusiano na Mataifa alisema kwamba"lazima tufanye kila kitu ili kuepuka kushindwa kwa Ukraine, kwa sababu hiyo itabadilisha mambo kwa kiasi kikubwa.” Kile ambacho Kanisa, Vatican na Papa wanaendelea kusisitiza ni “kufanyia kazi  ya amani na kujaribu kukuza amani. Hatuwezi kufikiria kufikia suluhu kwa ushindi au kushindwa.” Kwa njia hiyo kiongozi huyo hakushindwi kusisitiza tena hofu ya kuongezeka kwa nyuklia kwamba: “Hii inatufanya tuelewe kwamba lazima tujenge ulimwengu bila silaha za nyuklia na kwamba kwa kweli umiliki wa silaha hizi unatufanya kuwa hatari zaidi na haitoi dhamana ya usalama wetu. Ikiwa shambulio la nyuklia linabaki kuwa uwezekano mkubwa, kwa  upande wa Askofu Mkuu Gallagher ni badala ya kuepukika kwamba wakati migogoro itaisha kutakuwa na utaratibu mpya wa dunia na sio tu mgawanyiko wa Magharibi-Mashariki lakini makundi washirika zaidi duniani.”

Suluhisho  la mataifa mawili kwa Israeli na Palestina

Nafasi ya kutosha katika mahojiano kuhusu vita katika Mashariki ya Kati, kuanzia hali ya mbaya, janga, na kutisha huko Gaza. Kama vile Katibu wa Vatican Kardinali  Pietro Parolin, alivyokuwa amefanya katika hafla zingine, Askofu Mkuu  Gallagher pia alisisitiza suluhisho la watu wawili, na mataifa  mawili kwa mustakabali wa Israeli na Palestina. Suluhisho ambalo linahitaji juhudi na sadaka na ambayo ilionekana iliyohifadhiwa, lakini sasa kuna mazungumzo mengi zaidi juu yake katika jumuiya ya kimataifa. Hili linatupatia tumaini, alisema: “Vatican imeendelea kusisitiza juu ya suluhisho hili, lakini kwa wengi halikuzingatiwa tena kuwa inawezekana. Sasa tunaona matatizo makubwa yaliyopo katika Ukanda  wa Magharibi, tatizo la mustakabali wa Gaza yenyewe, lakini angalau watu sasa wanaona kwamba ni lazima suluhisho la kisiasa litafutwe.” Kuhusiana na Ukanda wa Magharibi, tatizo kubwa la walowezi wa Israel limesalia, labda tatizo kubwa zaidi la kusuluhishwa katika siku zijazo ili kusimamisha mzozo huo. Hakuna suluhu za kimazingaombwe kutokana na idadi kubwa ya watu waliotawanywa katika eneo lote na mahusiano yaliyokasirisha; pia katika kesi hii njia ni kuzungumza na mazungumzo pia na mamlaka ya Israeli na kutafuta ufumbuzi kwa manufaa ya wote.” Alisisitiza Mkuu wa mahusiano ya Kimataifa.

Azimio la kusitisha mapigano Gaza: ujumbe mzito

Maneno ya Papa na msisitizo wake juu ya kuachiliwa kwa mateka, juu ya upatikanaji wa misaada ya kibinadamu na juu ya kusitisha mapigano kurudi tena alisisitiza kwamba suluhisho hili la mwisho linaonekana kuwa haliwezekani kwa sasa; kwa sababu “tunahitaji kufanya kazi,ili silaha zinyamaze si kwa miezi michache, lakini mara moja, katika siku hizi. “ Kwa hakika ukurasa mpya umefunguliwa na azimio la kusitisha mapigano lililoidhinishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kujiepusha na Marekani: kwa mujibu wa askofu mkuu, ni “ujumbe mzito sana na dalili kwamba utawala wa Marekani hauwezi daima kuendelea sawa na msimamo, kwa kutumia haki yake ya kura ya turufu kuzuia hatua zozote za Umoja wa Mataifa”. Kwa hakika, azimio hilo linaonesha kuwa msimamo wa nchi nyingi za Umoja wa Mataifa ni kumaliza vita hivi, kuleta amani, kuokoa kile kinachoweza kuokolewa.” Kuhusu mchezo hasa wa mateka wa Israel mikononi mwa Hamas, Askofu Mkuu Gallagher alithibitisha mawasiliano mbalimbali ya wanafamilia ambao wametuomba msaada na tunajaribu kufanya kila tuwezalo.”

Kufanya upya uongozi wa Palestina

Akizungumzia kuhusu Hamas, Katibu wa Mahusiano na Mataifa alisema kwamba shirika la kigaidi halina mustakabali kama chombo cha kisiasa:"Wao lazima waachane na uharibifu wa Nchi ya Israeli. Wao pia wanapaswa kuwa na manufaa ya watu wa Palestina katika moyo zaidi.”Alisema. Kwa upande wa Askofu Mkuu Gallagher, alisema “tunahitaji kufanya upya taasisi za Palestina na kusikiliza zaidi matakwa ya watu kwa siku zijazo, na hamu yao ya kuweza kuelezea kujitawala kwao katika uchaguzi. Hatimaye, askofu mkuu alisisitiza msaada wote unaowezekana kwa Wakristo wa Gaza, ambao ni wachache sana na sasa wakimbizi karibu na parokia ya Kikatoliki na Waorthodox na Waislamu katika hali ya kushangaza katika suala la rasilimali na maisha ya kila siku.”

Mke wa Mfalme mdogo William Kate Middelton

Katika mahojiano na Tg1 alikuwa  bado anatarajia kwenda “Montenegro kuanzia tarehe 21-24 Machi, 2024 eneo ambalo liko katika hali tete na ambalo linastahili umakini ya jumuiya ya kimataifa. Kwa ujumla, nchi hizi zote zilizo na maisha magumu ya nyuma “zinajaribu sana kusonga mbele, kujitangaza. Wengi wamechagua Ulaya na wanastahili faraja yetu yote.” Hatimaye, Askofu Mkuu Gallagher alionesha upendo na maombi kwa ajili ya  Kate Middleton Mke wa Mfalme  William amba hivi karibuni alitangaza juu ya ugonjwa wake wa saratani na matibabu. Askofu Mkuu ni mzaliwa wa Uingereza hivyo ni wazi kuulizwa swali kama hilo ambapo alijubu kwa kusema kwamba: “Mtu anapomwona mwanadamu katika udhaifu wake wote, hii haiwezi kushindwa kuamsha upendo wetu wote na msaada wetu.”

27 March 2024, 17:09