Tafuta

2024.02.29 Kardinali Parolin wakati wa mahojiano na TV2000. 2024.02.29 Kardinali Parolin wakati wa mahojiano na TV2000. 

Kard.Parolin:baadhi ya mwanga wa matumaini katika Mashariki ya Kati,tumaini!

Katibu wa Vatican akizungumza na wandishi wa TV2000,kando Kozi ya "kiti cha Ukarimu" huko Sacrofano,Roma alisema:“Tumeona kwamba diplomasia inafanya kazi ili kupata suluhisho na kwa hiyo pia upatikanaji wa misaada ya kibinadamu ambao ni hatua nyeti zaidi.” Kuhusu afya Papa alisema:“Baba Mtakatifu yuko vizuri,amepona mafua.Nilimuona jana akaniambia hakuna tatizo.”

Vatican News

Matumaini ya kuwepo kwa suluhisho katika mzozo wa Mashariki ya Kati. Yalisisitizwa tena na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican kando ya kazi ya Kozi kuhusu mada ya “Kiti cha Ukarimu” huko Sacrofano jijini Roma. Akiongea na Na waandishi wa Televisheni ya Baraza la Maaskofu Italia CEI (TV2000,) Kardinali huyo alitoa maoni yake kuhusu hali ya Nchi Takatifu.

Wakati wa kuhojiwa Kardinali Parolin Katibu wa Vatican 29 Februari 2024

Kwa upande wake alisema: “Inaonekana kwangu kwamba katika Mashariki ya Kati kuna mwanga wa matumaini, kwa maana kwamba tumeona diplomasia inafanya kazi kupata suluhisho na kwa hiyo pia upatikanaji wa misaada ya kibinadamu, ambayo inaonekana kwangu kuwa ni hatua nyeti zaidi kutokana na kile nilichosikia moja kwa moja kutoka katika vyanzo vya ndani, usambazaji wa chakula, dawa na huduma za matibabu.” Kwa kuongezea alibainisha kuwa: “Lakini naona kwamba ni vigumu,si rahisi. Lakini angalau ninaonekana kuelewa kwamba kuna shughuli fulani, na kuna harakati fulani. Hebu tutumaini kwamba hii inaweza kukomaa na kweli kuwa suluhisho katika eneo hilo linaloteswa sana.”

Papa yuko vizuri

Kardinali Parolin pia alitoa hakikisho juu ya afya ya Papa ambaye Jumatano tarehe 28 Februari 2024 alikwenda katika Hospitali ya Gemelli-Isola Tiberina, mjini Roma mara tu baada ya Katekesi yake kwa ajili ya kufanya “baadhi ya vipimo vya uchunguzi. “ Kwa hiyo Kardinali alisema: “Baba Mtakatifu ni mzima, nilimwona jana tu usiku.” Nilifanya ziara ya kawaida na kuniambia kuwa hakuna shida kabisa na pia amepona mafua. Nilimkuta akiwa mzima sana jana usiku na yeye mwenyewe aliniambia nilipewa hakikisho kwa maana hii.” Alisema Katibu huyo wa Vatican.

01 March 2024, 11:08