Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Sana Padre Godfrey Jackson Mwasekaga, wa Jimbo kuu la Mbeya, Tanzania kuwa Askofu msaidizi wa Jimbo Kuu la Mbeya. Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Sana Padre Godfrey Jackson Mwasekaga, wa Jimbo kuu la Mbeya, Tanzania kuwa Askofu msaidizi wa Jimbo Kuu la Mbeya. 

Askofu Msaidizi Godfrey Jackson Mwasekaga Jimbo Kuu la Mbeya, Tanzania

Askofu msaidizi mteule Godfrey Jackson Mwasekaga alizaliwa tarehe 7 Machi 1976 huko Kyela, Mbeya. Alisoma katika Seminari kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho, Jimbo kuu Katoliki la Songea na hatimaye, akapewa Daraja Takatifu ya Upadre tarehe 14 Julai 2005 kwa ajili ya Jimbo kuu la Mbeya. Hadi kuteuliwa kwake alikuwa ni Makamu Askofu Jimbo kuu la Mbeya, Mkurugenzi wa Idara ya Katesi Jimbo la Mkurugenzi wa Kituo cha Katekesi na Paroko wa Mwanjelwa!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S., Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Sana Padre Godfrey Jackson Mwasekaga, wa Jimbo kuu la Mbeya, Tanzania kuwa Askofu msaidizi wa Jimbo Kuu la Mbeya. Kabla ya uteuzi huu, Askofu msaidizi mteule Godfrey Jackson Mwasekaga, alikuwa ni Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Francisko wa Assisi, Mwanjelwa, Jimbo kuu la Mbeya na pia Makamu Askofu Jimbo kuu la Mbeya. Itakumbukwa kwamba, Askofu msaidizi mteule Godfrey Jackson Mwasekaga alizaliwa tarehe 7 Machi 1976 huko Kyela, Mbeya. Alisoma katika Seminari kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho, Jimbo kuu Katoliki la Songea na hatimaye, akapewa Daraja Takatifu ya Upadre tarehe 14 Julai 2005 kwa ajili ya Jimbo kuu la Mbeya.

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania
Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania

Tangu wakati huo kama Padre aliteuliwa kuwa Paroko-usu Parokia ya Mtakatifu Claver, Mlowo kati ya Mwaka 2005 hadi Mwaka 2008. Mkurugenzi wa Idara ya Katekesi Jimbo na Mkurugenzi wa Kituo cha Katekesi kati ya Mwaka 2006 hadi mwaka 2008. Baadaye akatumwa na Jimbo kuu la Mbeya kujiendeleza kwa masomo katika Taalimungu katika Taasisi ya “Salesiano San Tommaso Messina” nchini Italia. Baadaye akazama zaidi katika Taalimungu na kujipatia Shahada ya Uzamivu katika Taalimungu kutoka katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Wasalesian, kilichoko Roma, kati ya Mwaka 2008 hadi mwaka 2017.

Askofu msaidizi mteule Godfrey Jackson Mwasekaga, Jimbo kuu la Mbeya
Askofu msaidizi mteule Godfrey Jackson Mwasekaga, Jimbo kuu la Mbeya

Baada ya masomo yake, alirejea Jimboni Mbeya na kuteuliwa kuwa Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Petro Claver, Mlowo kati ya Mwaka 2018-2019. Kuanzia mwaka 2017 ni Mkurugenzi mkuu wa Idara ya Katekesi Jimbo kuu la Mbeya, Mkurugenzi wa Kituo cha Katekesi na Mratibu wa Liturujia ya Kanisa. Na pia kuanzia mwaka 2019 akateuliwa kuwa ni Makamu Askofu Jimbo kuu la Mbeya na Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Francisko wa Assisi, Mwanjelwa, Jimbo kuu la Mbeya.

Uteuzi Mbeya
09 March 2024, 13:35