Tafuta

Askofu mkuu Raphael P’Mony Wokorach, M.C.C.J.  wa Jimbo kuu la Gulu, Uganda Askofu mkuu Raphael P’Mony Wokorach, M.C.C.J. wa Jimbo kuu la Gulu, Uganda 

Askofu Mkuu Raphael P’Mony Wokorach, M.C.C.J. Jimbo Kuu la Gulu, Uganda

Kabla ya kuteuliwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Nebbi alikuwa ni Kamishna wa Kitume wa Shirika la Mitume wa Yesu, AJ. Askofu mkuu Raphael P’Mony Wokorach, M.C.C.J. Alizaliwa tarehe 21 Januari 1961 huko Ojigo, Jimbo Katoliki la Arua. Baada ya masomo na majiundo yake ya kitawa katika Shirika la Wamisionari wa Wacomboni wa Moyo Mtakatifu wa Yesu akaweka nadhiri zake za daima tarehe 12 Oktoba 1992. Kunako tarehe 25 Septemba 1993 alipewa Upadre.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S., Vatican

Baba Mtakatifu Francisko tarehe 22 Machi 2024 amemteua Askofu Raphael P’Mony Wokorach, M.C.C.J. wa Shirika la Wamisionari wa Comboni wa Moyo Mtakatifu wa Yesu kuwa Askofu mkuu wa Jimbo Kuu la Gulu nchini Uganda. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Raphael P’Mony Wokorach, M.C.C.J. alikuwa ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Nebbi, Uganda. Kabla ya kuteuliwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Nebbi alikuwa ni Kamishna wa Kitume wa Shirika la Mitume wa Yesu, AJ. Askofu mkuu Raphael P’Mony Wokorach, M.C.C.J. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Raphael P’Mony Wokorach, M.C.C.J., alizaliwa tarehe 21 Januari 1961 huko Ojigo, Jimbo Katoliki la Arua, Uganda. Baada ya masomo na majiundo yake ya maisha ya kitawa katika Shirika la Wamisionari wa Wacomboni wa Moyo Mtakatifu wa Yesu akaweka nadhiri zake za daima tarehe12 Oktoba 1992. Kunako tarehe 25 Septemba 1993 alipewa Daraja takatifu ya Upadre.

Askofu mkuu Raphael P'Mony Wokorach, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Gulu
Askofu mkuu Raphael P'Mony Wokorach, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Gulu

Tangu wakati huo kama Padre amefanya utume wake wa kimisionari katika nchi mbalimbali kama vile: DRC na Togo. Na kati ya mwaka 2003 hadi mwaka 2007 alitumwa nchini Marekani, kuwa ni mlezi kwenye Chuo cha Wacomboni Kimataifa. Kati ya mwaka 2007 hadi mwaka 2015 alikuwa nchini Kenya kama mlezi na jaalimu kwenye Chuo Kikuu cha Tangaza. Kati ya mwaka 2011 hadi mwaka 2013 alichaguliwa kuwa ni kati ya Washauri wa Kanda ya Shirika la Wamisionari wa Wacomboni wa Moyo Mtakatifu wa Yesu nchini Kenya. Kati ya Mwaka 2015 hadi mwaka 2018 aliteuliwa na Vatican kuwa ni Kamishna wa Kitume wa Shirika la Mitume wa Yesu, AJ. Na hadi kuteuliwa kwake ameendelea kuwa ni Kamishana wa Shirika la Mitume wa Yesu, AJ., lenye Makao yake makuu Lang’ata, Jijini Nairobi. Tarehe 31 Machi 2021, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Nebbi. Na ilipogota tarehe 22 Machi 2024 Baba Mtakatifu akamteuwa kuwa Askofu mkuu wa wa Jimbo kuu la Gulu, nchini Uganda.

Jimbo kuu la Gulu, Uganda.
Jimbo kuu la Gulu, Uganda.

Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu mstaafu John Baptist Odama wa Jimbo kuu la Gulu, Uganda alizaliwa tarehe 29 Juni 1947. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 14 Desemba 1974 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Mtakatifu Yohane Paulo II tarehe 23 Februari 1996 akamteuwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Nebbi nchini Uganda na kuwekwa wakfu kuwa ni Askofu. Tarehe 22 Januari 1999 Mtakatifu Yohane Paulo II akamteuwa kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Gulu, Uganda. Na ilipowadia tarehe 22 Machi 2024 Baba Mtakatifu Francisko akaridhia ombi lake la kutaka kung’atuka madarakani. Kimsingi Askofu mkuu mstaafu John Baptist Odama wa Jimbo kuu la Gulu amelitumia Kanisa kama Padre kwa muda wa miaka 49 na Askofu akiwa na dhamana ya: kufundisha, kuongoza na kuwatakatifu watu wa Mungu, kwa muda wa miaka 27 na Ushehe.

Jimbo kuu la Gulu
26 March 2024, 13:46