Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko tarehe 23 Februari 2024 amemteua Askofu mkuu Giampiero Gloder, kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Romania na Moldova. Baba Mtakatifu Francisko tarehe 23 Februari 2024 amemteua Askofu mkuu Giampiero Gloder, kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Romania na Moldova. 

Askofu Mkuu Giampiero Gloder Balozi wa Vatican: Romania na Moldavia

Askofu mkuu Gloder alizaliwa tarehe 15 Mei 1958. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi, akapadrishwa tarehe 4 Juni 1983. Papa Francisko hapo tarehe 21 Septemba 2013, akamteuwa kuwa Balozi na Rais wa Baraza la Kipapa la Taasisi za Kikanisa na kumpandisha hadhi ya kuwa ni Askofu mkuu na hivyo kuwekwa wakfu tarehe 24 Oktoba 2013. Tarehe 11 Oktoba 2019 akateuliwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Cuba. Tarehe 23 Feb. 2024 Balozi wa Romania na Moldavia

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S., Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko tarehe 23 Februari 2024 amemteua Askofu mkuu Giampiero Gloder, kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Romania na Moldavia. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Giampiero Gloder, alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Cuba.  Askofu mkuu Gloder aliwahi kuwa ni Rais wa Taasisi za Kipapa Kikanisa. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Gloder alizaliwa kunako tarehe 15 Mei 1958. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi, akapadrishwa tarehe 4 Juni 1983. Kunako mwaka 1990 akajipatia shahada ya uzamili katika Sheria za Kanisa kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa cha Mtakatifu Thoma wa Akwino, Angelicum kilichoko mjini Roma. Na mwaka 1992 akatunukiwa shahada ya Uzamivu katika Mafundisho Sadikifu ya Kanisa kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregorian, kilichoko mjini Roma.

Hija ya Kitume ya Papa Francisko nchini Romania
Hija ya Kitume ya Papa Francisko nchini Romania

Utafiti wake wa kisayansi ulijikita zaidi katika taalimungu mintarafu Mtakatifu Paulo VI. Askofu mkuu Giampiero Gloder alianza utume wake wa kidiplomasia mjini Vatican, tarehe 1 Julai 1992. Tangu wakati huo, akabahatika kutekeleza utume huu nchini Guatemala na Vatican. Baba Mtakatifu Francisko hapo tarehe 21 Septemba 2013, akamteuwa kuwa Balozi na Rais wa Baraza la Kipapa la Taasisi za Kikanisa na kumpandisha hadhi ya kuwa ni Askofu mkuu na hivyo kuwekwa wakfu tarehe 24 Oktoba 2013. Tarehe 11 Oktoba 2019 akateuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Balozi wa Vatican nchini Cuba na hatimaye tarehe 23 Februari 2024 akateuliwa kuwa ni Balozi mpya wa Vatican nchini Romania na Moldavia.

Uteuzi

 

03 March 2024, 14:52