Tafuta

2024.03.02 Askofu Mkuu Giovanni Gaspari ameteuliwa na Papa Francisko kuwa Balozi Mpya wa Korea na Mongolia. 2024.03.02 Askofu Mkuu Giovanni Gaspari ameteuliwa na Papa Francisko kuwa Balozi Mpya wa Korea na Mongolia. 

Askofu Mkuu Gaspari ni Balozi mpya wa Corea na Mongolia!

Papa Francisko amemteua Balozi wa Vatican wa Korea Kusini na Mongolia,Askofu Mkuu Giovanni Gaspari,ambaye ahadi uteuzi huo alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Angola na São Tomé na Príncipe.

Vatican News

Baba Mtakatifu Francisko tarehe 2 Machi 2024 amemteua Balozi wa Vatican wa Korea Kusini na Mongolia, Askofu Mkuu Giovanni Gaspari, ambaye hadi uteuzi huo alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Angola na  São Tomé na Príncipe. Katika mabadiliko hayo ya kibara kutoka Afrika kwenda Asia atakuwa na safari ndegu  Askofu Mkuu huyo ambapo uteuzi huo unakuja kuchukua nafasi ya Askofu Alfred Xuereb, ambaye Baba Mtakatifu Francisko alimteua kuwa Balozi Vatican Nchini Morocco mnamo mwezi Desemba 2023.

Utume wake

Askofu Mkuu  Gaspari alizaliwa mnamo 1963 huko Pescara,Abruzzo, Italia na alipewa daraja la Upadre mnamo 1987. Alihitimu katika Sheria ya Kononi na kupata Leseni katika Taalimungu ya Maadili. Alijiunga na Huduma ya Kidiplomasia ya Vatican mnamo 2001, ambayo ilifuatiwa na utume wake katika uwakilishi wa Kipapa nchini Iran, Albania, Mexico, Lithuania na kisha kipindi cha kazi katika Sekretarieti ya Vatican kwenye kitengo cha Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya kimataifa. Mnamo Septemba 2020, Papa Francisko alimteua kama Balozi wa Vatican nchini Angola na São Tomé na Príncipe, na kumpandisha hadhi ya kuwa Askofu Mkuu. Aliekwa wakfu wa kiaskofu mikononi mwa Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican mnamo tarehe 17 Oktoba 2020 katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican. Anazungumza mbali na Kiitaliano pia lugha ya Kiingereza, Kihispania na Kifaransa.

Balozi Mpya wa Vatican huko Korea Kusini na Mongolia
02 March 2024, 13:46