Tafuta

2022.04.23 Makaburini nchini Ukraine. 2022.04.23 Makaburini nchini Ukraine.  Tahariri

Mpaka lini?

Baada ya miaka miwili ya vita nchini Ukraine,vya milipuko na mateso,tunajiuliza ni nini bado kinapaswa kufanywa ili uchokozi usitishwe na kujiweka katika meza ya kujadili amani ya haki?

Andrea Tornielli

Hata kama habari za kutisha ambazo zimefika kutoka Nchi Takatifu katika miezi ya hivi karibuni, na sasa kifo cha mpinzani wa Urussi Navalny, kimefunika habari za vita vya Ukraine, leo hii tunataka kukumbuka. Tunafanya hivyo siku hizi, tukitoa sauti kwa mashahidi, kwa wale ambao hawakubaliani na mantiki ya chuki, kwa wale wanaoendelea kuomba na kuendelea kuchukua hatua ili kupunguza mateso ya watu walioangamizwa kwa miezi ishirini na nne ya mabomu. Tulifanya hivyo kwa kuruhusu idadi ya kubwa izungumze, kwa sababu ukweli mkali wa kile kinachotokea, ambacho mara nyingi sasa kinakuwa mbali na uangalizi, inaelezea unyama wa kipuuzi wa vita hivi. Makumi ya maelfu ya maisha ya wanadamu yametolewa sadaka ili kushinda kilomita chache za eneo, makumi ya maelfu ya vijana na wazee wamejeruhiwa au kulemazwa, miji yote ya Kiukraine imeharibiwa kabisa, mamilioni ya watu waliokimbia makazi yao wanaishi nje ya nchi, maelfu ya migodi yamekusudiwa kudhoofisha maisha ya baadaye ya watu wasio na hatia... Ni nini bado kinapaswa kufanyika ili uchokozi ukome na ili wapate kukaa kuzungukia meza kwa ajili ya kujadili amani ya haki?

Maombi mengi ya Papa Francisko ya kutaka umakini juu ya “Ukraine inayoteswa” yameachwa kuanguka kwenye utupu. Vita na jeuri inaonekana kuwa njia ya kusuluhisha mizozo. Mashindano ya silaha kwa mtazamo wa vita vya siku zijazo sasa ni ukweli, hii pia inakubaliwa kama isiyoepukika. Pesa ambazo haziwezi kupatikana kujenga shule za chekechea na sekondari, kufadhili huduma ya afya inayofanya kazi, kupambana na njaa au kukuza mpito wa ekolojia na ulinzi wa sayari yetu moyoni, zinapatikana kila wakati linapokuja suala la silaha. Diplomasia inaonekana kimya mbele ya ving'ora vya vita. Maneno kama vile amani, mazungumzo, mapatano, mazungumzo yanatazamwa kwa kutiliwa shaka. Ulaya ilisikika kidogo sana,  zaidi ya viongozi binafsi waliomstari wa mbele. Haijawahi kutokea hitaji kama hilo la kutokubali mantiki ya vita. Kuna haja ya kuendelea kuomba zawadi ya amani kutoka kwa Mungu, huku Mrithi wa Petro akiendelea kufanya bila kuchoka, akijua jinsi ya kuona mwanga wa matumaini unaofuka chini ya blanketi linalozidi kuwa nene la majivu ya chuki.

Kuna haja ya uongozi mpya wa kinabii, ubunifu na huru, wenye uwezo wa kuthubutu, wa kuweka jitihada  juu ya amani, na kuchukua jukumu la mustakabali wa wanadamu. Tunahitaji dhamira ya kuwajibika ya kila mtu ili kutoa sauti ya wale ambao hawajisalimishi katika mantiki ya “Kaini” ya "wababe wa vita" iliyosikika kwa nguvu na uamuzi, ambayo inahatarisha kutupeleka kwenye maangamizi ya kibinafsi.

Tahariri ya Mwariri Mkuu wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano kuhusu vita nchini Ukraine
24 February 2024, 16:16