Tafuta

2024.02.22 'Kutoka Utalii kuwa Mhujaji katika Tovuti ndiogo kuhusu makanisa makuu ya Kipapa. 2024.02.22 'Kutoka Utalii kuwa Mhujaji katika Tovuti ndiogo kuhusu makanisa makuu ya Kipapa. 

Tovuti ndogo ya kusimulia uzoefu wa Hija katika Basilika za Kipapa imezinduliwa

Tovuti yenye kichwa:“Kutoka Utalii hadi Mhujaji”imezinduliwa ikiwa ni matokeo ya uzoefu ulioshirikishwa na kikundi cha wawasiliani vijana waliochaguliwa na Baraza la Kipapa la Mawasiliano.Kusudi ni kuwasindikiza waamini katika safari ambayo wanajigundua kama mahujaji zaidi ya kuwa watalii.

Vatican News

Kama matokeo ya uzoefu ulioshirikishwa na kikundi cha wawasilianaji vijana waliochaguliwa na Baraza la Kipapa la Mawasiliano, limezindua tovuti ndogo yenye kichwa: “Kutika Mtalii kuwa Mhujaji” tarehe 22 Februari 2024, kwa lengo la kuwasindikiza waamini katika safari ambayo wanaweza kujitambua kuwa  mahujaji zaidi ya kuwa  watalii. Kama sehemu ya Mpango wa “Mawasiliano ya Imani katika Ulimwengu wa Kidijitali, wataalamu vijana 16 kutoka nchi 10 tofauti, wakifuatana na wataalam, waliweza kugundua Basilika, sio tu kama minara ya usanifu, lakini kama ushuhuda hai wa imani. Kwa njia hiyo Tovuti ndogo ya lugha nyingi ni jibu la changamoto ya kutafsiri uzoefu huu kuwa pendekezo la kidijitali ili kusaidia hadhira ya vijana katika kugundua Makanisa makuu (Basilika).

Kuhusika kwa kina

Ili kuiweka katika maneno yao: “Tuliguswa moyo tulipotembelea makanisa. Kila mmoja wetu amepitia ushiriki wa kina na angalau mmoja wao. Baadhi yetu hata tumegundua jambo muhimu sana katika maisha yetu. Tunataka wageni wapate matumizi sawa, lakini katika ulimwengu wa kidijitali. Kadiri tunavyoweza kuelewa asili ya imani yetu, ndivyo tunavyoweza kuwasilisha Ujumbe vizuri ili kugusa mioyo ya watu.

Takwimu za watakatifu na wasanii, ambao maisha na kazi zao zimeunda maeneo haya ya mfano, kuwakaribisha wale wanaoipata tovuti, na kuwaalika kuketi mezani nao. Eneo hili kama nafasi ya kawaida ya kushiriki, sio tu ya chakula, lakini ya maoni, historia, uzoefu, kwa hiyo kualika kuacha kwa muda kwa kutoa muda wa kutafakari kwa ufupi.”

Sehemu Takatifu zenye sanaa

Lugha kuu iliyochaguliwa kuhamasisha uzoefu wa mtu wa kwanza ni sauti: nafasi takatifu zilizo na kazi zao za sanaa uelezwa na wale wanaotembelea maeneo haya kila siku na kuwakaribisha mahujaji: wasimamizi wa sanaa, wasimamizi wa uchimbaji na ukarabati, walimu na  watawa mashahidi ambao, kwa uchangamfu wa sauti zao, wanaweza kuwasilisha upendo wao kwa yale ambayo Makanisa manne Makuu ya Kipapa yanawakilishwa:(Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, Mtakatifu Maria Mkuu, Mtakatifu Yohane wa Laterano,na Mtakatifu Paulo Nje ya Ukuta.)

Kwa hivyo “Kutoka kuwa Mtalii hadi kuwa Mwanahija pia inakuwa podcast na wazo la kuwasindikiza na Hija kwa mkono kupitia sehemu muhimu zaidi za Hija Jijini Roma, na hatua na ufahamu maalum unaohusishwa na maeneo muhimu zaidi ya Makanisa makuu haya(Basilika): “Kile cha kuwa  mtalii kinaweza kuonekana kama kwa ujumla, machoni pa msafiri hubadilika kuwa jukwaa, ratiba, ishara za kimungu. Ziara hizi ndogo zimeundwa ili kuonesha uzuri uliofichwa wa Roma, unaofichuliwa kupitia lenzi ya Hija.” Wanaeleza wahusika wakuu wa uundaji wa Tofuti hiyo.

Kutoka Utalii kuwa Mwanahija ni kifuniko pia cha Podcast
Kutoka Utalii kuwa Mwanahija ni kifuniko pia cha Podcast

Kutia moyo kwa Jubilei

Hatimaye, kama vile “mahujaji-wawasiliani wanavyotoa ushuhuda wao wa kibinafsi, kwa atakayetembelea tovuti pia anaalikwa kushiriki, kupitia akaunti zao za kijamii, uzoefu wao na kuacha ushuhuda wa hija yao, halisi au ya kidijitali, kupitia: hashtag #KutokaMtaliiKuwamhujaji. Ni matumaini kwamba, katika mtazamo wa njia itakayoongoza kuelekea Jubilei ya 2025, uzoefu huu utachangia na kututia moyo kuzindua upya historia ya utamaduni wa miaka elfu ya hija “Ad Limina Apostolorum.”

Tovuti ndogo ya wanahija katika Mtandaoni

 

23 February 2024, 12:00