Tafuta

Nyumba ya Udugu ya Sacrofano,Roma. Nyumba ya Udugu ya Sacrofano,Roma. 

Toleo la II 2024:udhaifu na jamii,ukarimu&ushirikishwaji,Kard.Parolin na Czerny watazungumza

Udhaifu na jamii.Kati ya ukarimu na ushirikishwaji ni mada ya toleo la 2024 kuanzia Februari 27- 1 Machi katika Ukumbi wa Udugu huko Sacrofano Roma.Mkutano minne ya Mitandao intangulia kuhusu mazingira magumu na umaskini mpya.Wakati wa tukio kutakuwa na mazungumzo kati ya mkurugenzi Garrone na Padre Spadaro.Washiriki watakutana na Papa.

Vatican News

Changamoto ya kuelimisha kuhusu ukarimu inaendelea kwa kuzama katika wasifu wa kianthropolojia na kimaadili wa mojawapo ya vipimo vya kimsingi vya mwanadamu. Kwa kutiwa moyo na Papa Francisko, mashirika ya kuhamaisha - vyama, taasisi, mifuko na jumuiya zinazofanya kazi katika nyanja za ushirikishwaji na mapokezi - wamepanga kufanya mafunzo ya siku nne katika Nyumba ya Udugu huko Sacrofano (RM), kuanzia tarehe 27 Februari hadi 1 Machi 2024.

Toleo la pili la la mafunzo litakaloendeshwa likitanguliwa na mikutano ya mitandaoni minne ya kina juu ya mada ya mazingira magumu na aina mpya za umaskini, wakati wa kozi ya makazi itatoa nuru ya uhusiano kati ya jamii-jumuishi na shida zinazotokana na kudorora na kudhoofika kwa mfumo wa kijamii. Udhaifu wa wanaume, wanawake na maeneo kama changamoto ya dharura, jambo ambalo kwa muda mrefu limekuwa fundisho la  uchambuzi wa kisiasa, kijamii na kiuchumi na kutafakari, kuchambuliwa katika mienendo yake, ili pia kufichua uwezo wake na vipengele chanya.

Wageni kadhaa

Wakati wa kozi, uchunguzi wa kina wa nafasi za mazungumzo na ukaribu, ambapo kuzaliwa upya au kuimarisha uhusiano na mapendo ya kijamii, mabonde ya nguvu ili kujibu mahitaji ya ubinadamu ambayo yanazidi kuhitaji faraja na kuzidi kuchanganyikiwa na mivutano ya kimataifa. Ninapokuwa dhaifu, ndipo ninapokuwa na nguvu” (2 Kor 12,10) ni maneno ya Mtume wa Watu, Mtakatifu  Paulo yatakuwa kiini cha tafakari lilichokabidhiwa kwa wawakilishi wa taasisi, kisiasa, elimu, na wahudumu wa kijamii. Miongoni mwa wageni, makamu wa rais wa Bunge la Ulaya, Pina Picierno, kisha Rosy Bindi, ndugu Luciano Manicardi wa Jumuiya ya Kiekumene ya Bose, Padre Mattia Ferrari, anayehudumu katika Kikundi cha Kibinadamu cha Uokaji cha Mediterranea.

Hotuba za Kardinali Parolin na Kardinali Czerny

Mbali na wataalam na wasomi hotuba za Katibu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin, na Kardinali Michael Czerny, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuhamaisha Maendeleo fungamani ya Binadamu. Wakati wa kozi pia kutakuwa na mazungumzo juu ya mazingira magumu na simulizi yake katika sehemu maalum “Kiroho katika mwendo.” La kukumbukwa ni mazungumzo kati ya Matteo Garrone, mkurugenzi wa filamu ya ‘Io Capitano’  ‘mimi ni kapteni’ na Padre Antonio Spadaro, katibu mkuu wa Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu na wengine miongoni ni mwandishi wa habari Francesca Fialdini na mwandishi wa vitabu Daniele Mencarelli, tafakari ya “mambo machache ambayo ni muhimu” na Padre Luigi Verdi, wa Udugu wa Romena. Toleo hili litafungwa na Mkutano na Papa Francisko kwa washiriki.

22 February 2024, 15:25