Tafuta

Juma Takatifu litafunguliwa na Dominika ya Matawi  tarehe 24 Machi 2024. Juma Takatifu litafunguliwa na Dominika ya Matawi tarehe 24 Machi 2024.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Ratiba ya maadhimisho ya kipapa mwezi Machi na inaanza na Dominika ya Matawi Machi 24

Dominika ya Matawi 24 Machi,Alhamisi Kuu 28 Machi,Ijumaa Kuu 29 Machi,Jumamosi Kuu 30 Machi mKesha wa Pasaka na tarehe 31 Machi Siku kuu ya Ufufuko wa Bwana ndizo tarehe muhimu za maadhimisho ya Kipapa kwa mwezi Machi zilizochapishwa na Ofisi ya Mshereheshaji wa Liturujia za Kipapa.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kutoka katika Ofisi ya Mshereheshaji wa Liturujia ya Kipapa,  Askofu Mkuu  Diego Ravelli ametoa ratiba ya liturujia za kipapa kwa mwezi Machi 2024 kuanzia na Dominika  tarehe 24  Machi  ambayo ni Siku ya Matawi na kuanza kwa Juma Takatifu la Mateso ya Bwana wetu Yesu Kristo. Katika siku hiyo kwenye Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican saa 10.00 kamili majira ya Italia, Baba Mtakatifu anatarajia kuadhimishwa misa kwa kuanza na  maandamano ya kumbukumbu ya kuingia kwa Bwana huko Jerusalemu.

Siku ya Matawi
Siku ya Matawi

Alhamisi Kuu 28 Machi

Tarehe 28 Machi  2024 ni siku ya Alhamisi Kuu ya Juma Takatifu, ambapo katika Basilika ya Mtakatifu Petro itaona maadhimisho ya Misa Takatifu ya Misa ya Krisma  asubuhi  saa 3.30.

Misa ya Kubariki mafuta ya Crisma
Misa ya Kubariki mafuta ya Crisma

Ijumaa Takatifu 29 Machi

Na  tarehe 29 Machi 2024 ni siku ya Ijumaa Kuu ya Mateso ya na kifo cha Bwana wetu Yesu Kristo katika Juma Kuu. Jioni ya saa 11.00  kamili inatarajiwa kufanyika maadhimisho ya Ibada ya Mateso ya Bwana Wetu Yesu Kristo Katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.

Katika magofu ya Roma walipoteswa wakristo wa kwanza
Katika magofu ya Roma walipoteswa wakristo wa kwanza

Itafuatia usiku huo huo wa Ijumaa Njia ya Msalaba katika Magofu ya Kale ya Kirumi mahali ambapo wakristo wa kwanza waliteswa kwa kutetea imani yao (Colosseo) majira ya saa 3.15, usiku.

Jumamosi Kuu 30 Machi na mkesha

Jumamosi Kuu tarehe 30 Machi 2024 ndiyo mkesha wa Ufufuko wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambapo katika Basilika ya Mtakatifu Petro saa 1.30 usiku kutakuwa na Mkesha Mtakatifu wa Pasaka ili kuingia usiku mtakatifu wa Dominika ya Pasaka ya ufufuko wa Bwana.

Mkesha wa Pasaka huanza kwa kuwashwa mshumaa
Mkesha wa Pasaka huanza kwa kuwashwa mshumaa

Dominika 31 Machi ni Ufufuko wa Bwana wetu Yesu Kristo

Tarehe 31 Machi, ndiyo siku ya  Dominika ya Pasaka ya  Ufufuko wa Bwana ambapo katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, saa 4.00 kamili asubuhi, misa Takatifu ya ufufuko wa Bwana itaadhimishwa na kufuatia saa 6 kamili mchana Baraka ya Urbi et Orbi.

Kupitia dirisha la mbele la Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro,ndipo Baraka ya Urb et Orbi hutolewa
Kupitia dirisha la mbele la Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro,ndipo Baraka ya Urb et Orbi hutolewa
Ratiba ya Misa za Kipapa kwa mwezi Machi 2024
29 February 2024, 15:53