Tafuta

2024.02.01 Askofu Mkuu Vincenzo Paglia huko Kerala(India). 2024.02.01 Askofu Mkuu Vincenzo Paglia huko Kerala(India). 

Paglia huko Bangalore:kataa sauti za kutisha dunia kuhusu Akili Mnemba

Safari ya kwenda India ya rais wa Chuo cha Kipapa cha Maisha inaendelea kwa ajili ya mkutano mkuu wa Baraza la Maaskofu wa India likiwa la baraza la kwanza kutia saini Wito wa Roma kwa Maadili ya Akili Mnemba(AI).Julai ijayo hati hiyo itatiwa saini huko Hiroshima na viongozi wa dini za Asia.

Vatican News

Tunapozungumza kuhusu Akili Mnemba (AI), ni lazima tukatae sauti za kuisha kwa duniana  kuzingatia kwa uwazi wa mabadiliko yanayoendelea, faida na changamoto zinazotupatia, ili kuakisi wakati wetu kwa busara. Hayo yamesisitizwa na Askofu Mkuu Vincenzo Paglia, Rais wa Chuo cha Kipapa cha Maisha, akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa Baraza la Maaskofu wa India mjini Bangalore tarehe 2 Februari 2024 uliowaleta pamoja maaskofu 175. Mada ya Mkutano huo ni: Jibu la Kanisa kwa hali ya sasa ya kijamii na kisiasa ya nchi na changamoto za Akili Mnemba.”Mnamo 2020, Askofu Mkuu Paglia alitangaza “Wito wa Roma kwa Maadili ya  Akili Mnemba (AI)”, hati ya dhamira iliyotiwa saini na Microsoft, IBM, FAO, serikali ya Italia na tangu wakati huo iliyotiwa saini na mamia ya vyuo vikuu, vituo vya utafiti na kampuni. Baraza la Maaskofu Katoliki India pia lilitia saini hati hiyo, ikiwa ni Baraza la kwanza kufanya hivyo.

Faida za teknolojia mpya

Katika ripoti yake, Askofu Mkuu Paglia alisisitiza manufaa kwa watu na jamii ambayo mifumo ya AI inaleta, alitoa maoni yake juu ya hilo kwamba  ni changamoto za kuzingatia katika mabadiliko ya kijamii yanayoathiri Kanisa na hivyo akataja kazi inayofanyika kwa  zote mbili katika Chuo cha Kipapa cha Maisha, na kwa hiyo alijikita katika masuala  msingi ya kianthropolojia. “Leo nisingependa kuzungumza nanyi kuhusu 'hatari' ambazo manabii wengi wa maangamizi wanatabiri. Badala yake, ningependa kuvutia umakini wenu kwanza kwa manufaa ya ajabu ambayo teknolojia mpya, na hasa mifumo ya Akili Mnemba, tayari inatoa katika  historia yetu. Katika sekta ya afya, utambuzi umeimarishwa sana na mifumo hii yenye uwezo wa kugundua au kutabiri magonjwa ambayo kwa kweli hayaonekani kwa macho ya mwanadamu. Maendeleo yamerekodiwa katika maabara na mafundisho ya matibabu, ambapo uundaji wa kidijitali umepiga hatua kubwa katika michakato ya mafunzo ya madaktari wa siku zijazo.” Askofu Mkuu alibainisha.

Hatari kwa vijana

Askofu Mkuu Paglia aliakisi jinsi ambavyo kuna matumizi mengi ya Akili Mnemba  katika ulimwengu wa kilimo, pia na zaidi ya yote katika maeneo hayo ambayo bado hayajatumiwa kwa vitendo vikali na vya uharibifu mara nyingi. “ Ikiwa tunatazama ulimwengu wa mawasiliano na usimamizi wa habari, hatuwezi kujizuia kushangazwa na urahisi tulionao katika kushiriki maudhui, kupata data iliyosafishwa, kusoma maandiko katika lugha nyingine. Mtandao na kidijitali, badala yake, unabadilisha kwa kiasi kikubwa miundo ya kijamii na mabadiliko hayo yanahusu Kanisa, ikiwa ni pamoja na taalimungu. Mtandao, angalau kwa kiwango cha juu juu, unachukua nafasi ya maono ya piramidi ya jamii na ya usawa na usio sawa. Ukweli si haki tena ya mamlaka iliyoanzishwa na kutambuliwa bali ni matokeo ya utafutaji wa kidadisi unaoendelea kati ya sauti elfu moja. Mitandao ya kijamii inakuza uwakilishi wa watu binafsi (kwa uangalifu maalum kwa wanawake na watu wanaoishi katika maeneo ya vijijini) ambayo hadi sasa ilikuwa isiyoweza kufikiria (na labda hata isiyofaa kwa baadhi). Askofu Mkuu  Paglia aidha alisema “ Mara nyingi tunahusisha mabadiliko ya kidijitali na ulimwengu wa vijana, na kuvunjika kwa usambazaji wa maarifa na imani kati ya vizazi, na ufikiaji rahisi wa uzoefu mbaya.”

Askofu Mkuu Paglia akielendelea maelezo alisema "Kweli lakini sehemu kubwa ya watumiaji wakubwa picha mbaya za mtandaoni (kwa mfano nchini India) ni watu wazima kati ya miaka 25 na 34 (waume na baba wa watoto, au tuseme waume na wanawake, mababa na wamama, ikizingatiwa kuwa asilimia 33% ya watumiaji ni wanawake). Hata wachezaji wa mtandaoni, zaidi nchini India pekee ni asilimia 59% ya watu wazima kati ya miaka 25 na 44.  Kwa hiyo lazima kuwa waangalifu ili wasipunguze suala hili kuwa suala la vijana, hata kama mtiririko huo wa  'sumu' unaweza kuwa na athari mbaya zaidi kwa vijana na barubaru.  Ya pili ni ya kitaalimungu  zaidi. Mpito kutoka kwa mamlaka hadi mamlaka, kutoka elimu hadi ushuhuda (nini tena washawishi?), kutoka juu  hadi sinodi, zote ni hatua zinazorejesha (au angalau kudokeza) mienendo ya kiinjili. Kwa nini waziwazie tu katika kukubalika kwao kwa uharibifu?”.

Kuzungumza juu ya wanaume na miili yao

Swali la msingi linahusu maono ya mwanadamu ambayo yanajitokeza na ambayo yanavutia sana Kanisa. Kwa sababu hiyo, Askofu Mkuu  Paglia alibainisha kwamba Mkutano Mkuu ujao wa Chuo cha Kipapa cha Maisha, kuanzia tarehe 12 hadi 14 Februari 2024, utakuwa na mada kuu ya Sula la  kianthropolojia. “Ikiwa tunajali kuhusu mifumo hii ni kwa sababu inaiga michakato fulani ambayo tunahusisha na akili ya binadamu.” Na kwa sababu hiyo  tunafanya kazi kuashiria tofauti, karibu kana kwamba ubinadamu wetu unakaa katika kitivo hiki. Sio kweli: sisi sio akili yetu pekee na mjadala wowote unaokwenda katika mwelekeo huu ni wa kupunguza. Sisi sio peke yetu katika data zetu pia. Data(aina ya kidini ya uwongo inayotokana na uwezo wa ajabu wa kubashiri wa mifumo ya kujifunza kwa mashine) inataka kutupunguza hadi (isitoshe) athari tunazoacha.”

Rais wa Taasisi ya Maisha aliongeza kusema kuwa "Lakini hii sivyo, kwa sababu “Mifumo ya Akili Mnemba (AI), iliyochukuliwa katika changamoto yao ya kina ya anthropolojia, inatuhitaji kurudi kuzungumza juu ya watu na miili yao. Mada ya haraka ni mwili, ikiwa unaweza, sisi ni wataalam juu ya mada hii. Tumejengwa juu ya tukio la kufanyika mwili kwa Mwana wa Mungu, kwenye mwili uliofufuka ambao Mtakatifu Thomas (mwinjili wa India) anaomba aweze kugusa, juu ya ahadi ya ufufuko wa mwili tunayokiri katika imani ya kitume."

Wito wa Roma wa Maadili ya AI

Akizungumzia kuhusu Wito wa Roma kwa Maadili ya AI mwaka 2020, ambapo Chuo cha Kipapa cha Maisha kinaendelea kuhahamasisha Askofu Mkuu  Paglia alibainisha kuwa sifa ya waraka ni katika kipengele chake cha wito wa mbinu ya kubuni maadili. Ni upuuzi wa kufikiria teknolojia kama zisizoegemea upande wowote. Wao, kama kazi nyingine yoyote ya kibinadamu, huleta pamoja nao utamaduni, ujenzi wa kijamii, nia, njia za kuelewa uchumi na ubinadamu. Swali la kimaadili lazima liulizwe mwanzoni, kwa kubuni: tunatakaje kubuni, kuunda na kuuza teknolojia hizi za ajabu? Katika kutoa wito wa udhibiti wa kimataifa wa AI, Askofu Mkuu Paglia alitangaza kwamba “Wito wa Roma kwa Maadili ya Akili Mnemba (AI)” utatiwa saini na viongozi wa dini za Asia Julai ijayo huko Hiroshima. “Kwa sababu wakati masuala ya kitaalimungu yanajadiliwa, dini hugawanyika, lakini wakati wema na mustakabali wa ubinadamu uko hatarini, wanaungana zaidi kuliko hapo awali. Wapendwa, mabadiliko makubwa yanayotokea lazima yasituogopeshe. Badala yake, ni mwito kwa wajibu ambao Injili inaweka juu yetu kuelekea maisha ya binadamu yanayoishi katika sayari hii. Kumbukumbu ya Pasaka ya Yesu hutufanya sisi wanawake na wanaume wanaosimamia siku zijazo.”

Mada ya familia

Mwishoni mwa hotuba yake, Askifu Mkuu  Paglia aliongeza maneno machache juu ya mada ya familia. “Hata hivyo, niruhusu niongeze kiambatisho kidogo kwenye tafakari hizi. Pamoja na kuwa rais wa Chuo cha Kipapa cha Maisha, mimi pia ni Kansela mkuu wa Taasisi ya Kipapa ya Yohane Paulo II ya Ndoa na Sayansi ya Familia. Hivi karibuni  nilitembelea sehemu ya India ya taasisi hii ambayo iko Changanacherry. Nilikuwa na mkutano wa siku mbili wa majukumu ya kichungaji ya familia ya Majimbo yote ya  Kerala. Ninawashukuru ninyi ambao mnawekeza watu na rasilimali katika mpango  huu na ninawaalika kila mtu kuzingatia taasisi hii kwa ajili ya mafunzo ya wale ambao wanapaswa kusindikiza  familia za makanisa yenu. Papa Francisko alitaka kupata tena taasisi hii ili kuiweka familia katikati ya Kanisa, kupanua mtazamo wake. Kiukweli, haiwezekani tena kuwaza kupunguza familia kwenye suala la maadili. Kuzungumza juu ya familia leo hii kunamaanisha kuzungumza juu ya uhusiano wa kijamii, juu ya umakini kwa vikundi dhaifu(watoto na wazee), pia juu ya muundo wa Kanisa, linaloitwa kujulikana zaidi.” Alisisitiza Askofu Mkuu.

Askofu Mkuu Paglia akihutubia Kanisa la India
02 February 2024, 16:26