Tafuta

2024.02.26 Kampeni katika Mitandao ya Kijamii kwa ajili ya Mwaka 5 tangu kuchapishwa Wosia wa  Christus Vivit 2024.02.26 Kampeni katika Mitandao ya Kijamii kwa ajili ya Mwaka 5 tangu kuchapishwa Wosia wa Christus Vivit 

Februari 25-Aprili 25 ni Kampeni ya waraka wa Christus Vivit baada ya miaka 5 ya kuchapishwa kwake

Miaka mitano ya “Christus Vivit,”ni kampeni ya kijamii ya kugundua tena Wosia wa Papa ambayo imeanza tangu tarehe 25 Februari hadi 25 Aprili,mpango wa majuma 12 katika wa mtandao wa kijamii unaohamasishwa na Baraza la Kipapa la Walei,Familia na Maisha iliyozindiliwa kugundua upya umuhimu wa Wosia wa kitume wa Papa kwa vijana wote na kuweka huai wa mang’amuzi ya Siku ya Vijana Duniani.

Vatican News

Mwaka huu 2024, Kanisa linaadhimisha miaka mitano tangu kuchapishawa kwa Wosia wa Kitume wa ‘Christus Vivit’, yaani ‘Kristo anaishi’ wa Baba Mtakatifu Francisko wa tarehe 25 Machi 2019 mara baada ya Sinodi ambapo alitia saini katika “Wosia” huo kwa ajili ya vijana katika Nyumba Takatifu ya Madhabahu ya Kimataifa ya Loreto, uliofunga kazi ya Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya vijana iliyofanyika mjini Vatican mwezi Oktoba 2018 na kutanguliwa kwa mara ya kwanza na Sinodi iliyotangulia kwa ushiriki wa vijana kutoka sehemu mbalimbali za dunia, na pia kutokana na tafakari zilizofanywa katika Makanisa mahalia pamoja na wawakilishi wa vizazi vya vijana.

Majukwaa ya kijamii ya Facebook na Instagram

Kwa sasa, katika kuadhimisha miaka mitano ya Waraka huo wa Christus Vivit, Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha linaambatana na kikundi cha wawasiliani vijana wanaoshiriki katika mpango wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano lenye kauli mbiu: “Mawasiliano ya Imani katika Ulimwengu wa kidijitali,” katika kutunga na kutengeneza kampeni ya kijamii kwa akaunti rasmi za Facebook na Instagram za Siku ya Vijana Duniani (WYD).

Kuanzia Februari 25 hadi Aprili 25

Kampeni hiyo iliyoanza Dominika  tarehe 25 Februari na itamalizika tarehe 25 Aprili 2024, inakusudia kuwaleta pamoja vijana kutoka sehemu mbalimbali za dunia kwa takribani majuma kumi na mbili ili kushiriki maana na roho ya sasa ya Wosia wa Christus Vivit pamoja na matunda ya Kanisa ya hivi karibuni ya  Siku ya Vijana Duniani ( WYD) huko  Lisbon 2023. Kwa njia hiyo kuanzia neno kuu ‘hai’ na kupitia video za msukumo, wito kwa hatua na ushiriki, matumaini ya washiriki katika mpango wa “Mawasiliano ya Imani katika Ulimwengu wa Kidijitali” ni kwamba mpango huu, kwa mchango wa vijana ambao wameshiriki katika Siku za Vijana Duniani (WYD), wahuishaji wao na wasimamizi wa kichungaji wa vijana  wanaweza  kuweka uzoefu wa Siku ya Vijana Duniani hai pia katika jukwaa la kidijitali na kuufanya mwaliko wa Baba Mtakatifu kuwa wao wenyewe usemao: “Ninyi sasa ni wa Mungu,ambaye anataka mpate kuzaa matunda”(ChV 178). Mpango huo, unaopatikana katika lugha nyingi,na unaweza pia kupitishwa na vyombo mbalimbali vya Kanisa mahalia ambao wanataka kusambaza tafakari ya kiroho katika mazingira yao ambayo yawafikie vijana kupitia mitandao ya kijamii. Msikose kusambaza na kutembelea majukwaa hayo

Miaka 5 ya Christus Vivit:shiriki Kampeni ya majuma 12 kuanzia Feb 25 hadi Aprili 25,2024
26 February 2024, 16:27