Tafuta

2024.02.26 Kardinali  Parolin katika kituo cha matibabu(IDI). 2024.02.26 Kardinali Parolin katika kituo cha matibabu(IDI). 

Ukraine,Kard.Parolin:ni huzuni hakuna matarajio mengine ya mazungumzo!

Kardinali Parolin,Katibu wa Vatican wakati wa uzinduzi wa idara mpya katika Taasisi ya Magonjwa ya Ngozi ya Bikira Mkingiwa(IDI),nje ya tukio alithibitisha afya njema ya Papa.Na kuhusiana na kifo cha Navalny aliakisi umuhimu wa kufafanua kile kilichotokea,wakati kwenye vurugu za hivi karibuni katika maandamano,Italia alitoa mwaliko kila mtu kuwa na busara.

Vatican News

Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican akiulizwa maswali na waandishi wa habari nje ya tukio la  uzinduzi wa kituo kipya cha uchunguzi wa kimatibabu cha  hospitali ya Magonjwa ya Ngozi ya Bikira Mkingiwa(IDI), jijini  Roma jioni tarehe 26 Februari 2024 awali kuhusu maandamano ya Pisa na Firenze nchini Italia yaliyoshuhudia mapigano kati ya polisi na wanafunzi alisema :“Kila mtu anaitwa kuwa mwenye busara. Na kutumia mabango“hakika ni kushindwa” hata hivyo “inaweza kujidhihirisha kwa njia sahihi. Lazima kila wakati tutafute njia sahihi ya kuelezea mahitaji yetu, hata maandamano yetu na wakati huo huo tuwe tayari kuwakaribisha.”

Papa Francisko yuko vizuri

Kadinali Parolin pia alizungumza kuhusu afya ya Papa Francisko na kuthibitisha kwamba Papa yuko Mzima, Alikuwa  na kipindi hiki cha mafua lakini akapona, ilikuwa inanibidi niende kwake jioni ya leo  hii lakini niko hapa, kikao kilikuwa hakijasitishwa. Kwa hiyo ina maana kwamba amepona na kuendelea na shughuli zake za kawaida.”

Inasikitisha kwamba hakuna matarajio ya amani kwa Ukraine

Katika ngazi ya kimataifa zaidi, Katibu wa Vatican alibainisha  kifo cha mpinzani wa Urussi Alexei Navalny, kwamba “ingekuwa muhimu kufafanua kile kilichotokea. Hii ingesaidia kuwahakikishia hata wale ambao kwa hakika wanatoa tafsiri fulani ya kifo hicho.” Lakini pia hali ya Ukraine, uwezekano wa mazungumzo ni katikati ya tahadhari ya Kardinali ambaye, akimaanisha ujumbe wa Kardinali Matteo Zuppi, rais wa Baraza la Maaskofu Italia (CEI,) na kuwa “tunajaribu kufanya kazi ili kufanya utaratibu huu ambao ulianzishwa wakati wa ziara yake huko Kyiv na Moscow kwa ajili ya kurudi kwa watoto na vijana kwa Ukraine rahisi kidogo.” Kwa kuongezea Kardinali alisema “wakati huo kwamba hii inaweza kukuza njia za amani. Kwa sasa inaonekana kwangu kwamba kuna hili tu, kwamba hakuna matarajio mengine ya mazungumzo na hii inasikitisha sana.” Kuhusiana na maandamano ya wakulima, ambao walirudi Brussels kuomba hatua nzuri zaidi kutoka Umoja wa Ulaya (EU), Kardinali Parolin alisisitiza kwamba tu kwa mazungumzo mazito na kusikiliza mahitaji yaliyotolewa na wakulima tunaweza kufikia matokeo, na kufikia  mkutano.”

Mashambulio dhidi ya Wakristo nchini Burkina Faso ni ya kusikitisha

Hatimaye, Kardinali alilezea “hali ya hatari" nchini Burkina Faso, ambapo Wakristo kumi na watano waliuawa wakati wa ibada ya Dominika: Kwa upande wa Kadinali, “ugaidi huu wote ambao umechukua udhibiti wa maeneo mengi unatia wasiwasi. Ilionekana kuwa jeshi lilikuwa likifanya kazi ya kurudisha udhibiti wa Jimbo lakini kwa bahati mbaya hii sio hivyo na vipindi hivi vinaendelea ambavyo ni vya kusikitisha sana.” Alieleza Katibu wa Vatican.

Majibu ya Kardinali Parolin Katibu wa Vatican
27 February 2024, 10:24